Njia gani zitumike kulisafisha Jeshi la polisi dhidi ya yanayoendelea?

Ukiona hata wao wenyewe polisi hawajaita kauli za Gwajima ni uchochezi au kumtaka akathibitishe.

Yaani polisi wameingilia kati baada ya amri kutoka ya kufungwa kwa kanisa.

Akili kichwani
 
Acha tu watu wameumizwa wanalalamika wameteswa na SIRIKALI ta TIZIII halafu j4 anakwambia ni MAONI tu.....watu kama hao wanakuja kuwa na MWISHO MBAYA sana.
Wamevuka mipaka,

Najiuliza, palikuwa na ulazima gani kumlawiti mtu yule na kumwambia aseme Asante Samia?
 
Wamevuka mipaka,

Najiuliza, palikuwa na ulazima gani kumlawiti mtu yule na kutwambia aseme Asante Samia?

Mimi naona watu hawaamini UCHAWI lakini ungekuwepo ni DHAHIRI wanaowafanyia watu ukatili ,wanaowateka watu wangekuwa washaonyeshwa CHA MTEMA KUNI.
 
No Reforms No Election
 
🤣🤣 Kulivunja tu
 
Ili kurudisha imani ya wananchi kwa jeshi la polisi, lazima turejeshe misingi ya uwajibikaji, uwazi, na kuheshimu haki za binadamu.

Kufuta sheria zinazowapa mamlaka 'wasiojulikana' bila uwajibikaji ni hatua muhimu, lakini haitoshi peke yake. Inahitajika mabadiliko ya kiutamaduni ndani ya jeshi lenyewe,, kurudi kwenye dhamira ya awali,, kulinda, si kutisha. Bila hilo, hata tukifuta sheria, "kinyago" bado kitaendelea kututisha.
 
Police huwa wanatumwa tu na kupewa maagizo na kwao kauli ni moja tu sawa mkuu,wakulaumiwa ni hawa viongozi wanaowatuma sio police.
 
Aisee polisi wetu hawajitambui, Kuna jamaa kapigwa marungu kisa kaenda kusikiliza kisa ya lissu.
Aisee polisi aje ajichanganye napita nae, anipige rungu aisee
 
Andika kero zako kwenye Bango kesho nenda mbele ya kituo cha polisi ulishikilie watapokea maoni yako watajirekebisha
 
Aisee polisi wetu hawajitambui, Kuna jamaa kapigwa marungu kisa kaenda kusikiliza kisa ya lissu.
Aisee polisi aje ajichanganye napita nae, anipige rungu aisee
Mbwa kumuuma mtu bila kuamrishwa na mwenye mbwa,

Hapo ni muhimu kupeleka mbwa wodini akapimwe akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…