Victoire
JF-Expert Member
- Jul 4, 2008
- 24,386
- 57,588
Mimi nilishaishi Paris. Nilikuwa mwanafunzi pale.Kuna saa nilikuwa napenda kwenda kuwasikiliza wakimbizi .Unakuta mtu anatoka Guinea Conakry. Anakuambia alifanya kazi akapata euro elfu 10 za kuwalipa ma mafia kumsaidia kuvuka jangwa Niger huko mpaka Lybia kupanda boti mpaka Visiwa vya Italia huko then kutembea kwa mguu mpaka Nice France then kudandia train mpaka Paris then kujikuta katika hali mbaya. Mpaka nilikuwa ninawaambia hiyo pesa euro elfu 10 ungewekeza ukaendelea kutafuta ungekuwa tajiri hapo hapo Conakry. Tatizo wakisikia Pariiii wanajua ni Paradise kumbe ni Shidaaaa.