Njia pekee nyepesi ya kuingia Ulaya kwa wale wanaohitaji kujilipua ni hii...

Mimi nilishaishi Paris. Nilikuwa mwanafunzi pale.Kuna saa nilikuwa napenda kwenda kuwasikiliza wakimbizi .Unakuta mtu anatoka Guinea Conakry. Anakuambia alifanya kazi akapata euro elfu 10 za kuwalipa ma mafia kumsaidia kuvuka jangwa Niger huko mpaka Lybia kupanda boti mpaka Visiwa vya Italia huko then kutembea kwa mguu mpaka Nice France then kudandia train mpaka Paris then kujikuta katika hali mbaya. Mpaka nilikuwa ninawaambia hiyo pesa euro elfu 10 ungewekeza ukaendelea kutafuta ungekuwa tajiri hapo hapo Conakry. Tatizo wakisikia Pariiii wanajua ni Paradise kumbe ni Shidaaaa.
 
Mambo ambayo wabongo hawako nyuma

Kufatilia Sinema zetu
Ndondo cup
Mange kimambi
Hamornize na kajala
Kufatilia connection za video /picha za utupu za watu.

Ni ajabu kabisa, kizazi cha kesho kinafikirisha sana.
Umesahau Simba na Yanga.Ila sasa kiwanda cha burudani bongo ndo kinalipa. Hao ndo fursa yenyewe. Si unaona Mange kaamka anauza umbea.
 
Mchongo upi?Kwenda kuteseka Ulaya.Bora mtu utesekee bongo. Ulaya ukiwa regal ndo raha. Yaani ukiwa na makaratasi ni safi utafanya kazi na unaishi vizuri na.nyumbani bongo utawasaidia,shida ni kwenye kupata makaratasi siku hizi ni ngumu sana.
 
Mambo ambayo wabongo hawako nyuma

Kufatilia Sinema zetu
Ndondo cup
Mange kimambi
Hamornize na kajala
Kufatilia connection za video /picha za utupu za watu.

Ni ajabu kabisa, kizazi cha kesho kinafikirisha sana.
Bila ya kusahau kusikiliza stori ya mandonga mtu kazi
 
England mbona super tu? UK ilikataa itifaki ya Sheghen viza na kubaki na UK viza na sterling pound yao walikuwa wanajihami nchi yao dhidi ya wahamiaji holela.

Mpaka Sasa kuna wahamiaji wapo nchi mbalimbali za ulaya wanatamani waingie tu UK.
 
Itakuchukua muda gani kufanikiwa huko unakoenda kwa mara ya kwanza kuliko huku ambapo upo tangu kuzaliwa
Nadhani ungejaribu kuhama kwanza mkoa
Mkuu kuna mtu toka 2010 hadi leo yuko bongo anapambana na hafanikiwi, na kuna mtu kaingia ulaya mwaka 2017 leo hii ana mafanikio mazuri tu na hana stress tena ya maisha.
 
Hahaa mi huwa nacheka Sana [emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38],watu wanaosema kuna fursa ,bongo hi hiii au ya mars na Neptune
Kungekuwa kuna fursa tusingeshuhudia wingi wa panya road mjini na pia isingekuwa rahisi 80% ya vijana kuwa machinga.
 
Sipingani na ulichoandika kuhusu Paris, lkn ulaya huko huko bado kuna zina fursa nzuri. Sio lazima watu wote mkajazane Paris, London nk.

Kuna baadhi ya nchi ambazo hazina refugees na migrant wengi pia zina fursa nyingi ila watu hawaziweki kwenye ramani zao za kwenda kuishi huko. Mfano wa nchi hizo ni Luxembourg, Iceland, Finland nk. Huko refugees na migrants ni wachache afu fursa za kazi ni nyingi, so mwenye akili lazima aende huko.
 
Wewe umeshakata VISA?
Kwahiyo mimi nikiwa na viza ndo itakushawishi na wewe kuitafuta?
Waswahili washasema akili ni nywele kila mtu ana zake. Mimi nimeona mchongo nikauleta hapa, kwahiyo ni juu ya kila mmoja kuamua kuchangamkia mchongo au kuacha.

Wenzetu wa nigeria, wakenya na waganda wametusua kutokana na kupeana michongo kama hivi, lkn wabongo wanapenda michongo ya kina Diamond na Ali kiba.
 
Ni kweli wazungu wenyewe wanakuja bongo kuomba ajira ukienda hoteli za kitalii wazungu wengi wamesajiliwa msharaa wanalipwa dollars 2000 na makwao hawataki kurudi na wanakula kwa mama lishe chapati na maharagwe.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Kwa hali hii hiyo hela ya nauli fanya mtaji baki Dar utatoka tu.
Si bora tubaki nchini tufungue genge au banda la chips usiku tunaenda kulala nyumbani na wife, tunajibana tunanunua kiwanja tunajenga nyumba tunakuwa na kwetu kuliko kwenda kulala barabarani ugenini.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Wanadanganyana hawajui hizo mbinu waarabu washaharibu kila kitu ulaya imekua km kariakoo.
Hizo mbinu zoote zishatumika na Europe kote zinajulikana
 
Upo ulaya au TZ?Na kwa taarifa yako wakimbizi wanakimbilia walau nchi zilizo rafiki kidogo kwa wakimbizi LUXEMBOURG unapasikia au unapajua ?,Kinchi kidogo maisha ghali. Halafu si rafiki kwa wakimbizi ulaya kama hauna legal permit huwezi fanya kazi. Acha kudanganya watu. Watu mpaka wanarun mental maana walitoka nchini mwao wakijua wanafika Ulaya kila kitu poa. Sasa wanakuta ndivyo sivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…