Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
- Thread starter
- #101
Wabongo bado tuko busy na maisha ya watu. Unakuta dume zima linatumia nusu siku nzima kusoma na kufuatilia habari za wanaume wenzie kama vile kina Mwijaku, baba levo nk.Sijui tunakwama wapi aisee,jamaa atakua na darasa tarehe 1 okt ubungo plaza nadhani kufundisha namna ya kuomba green card,muitiko ni sifuri bado,naona wakenya wamemuita kabisa aende kenya kuwafundisha,jana jamaa nimeona amepost youtube yupo kenya aisee!
Wakimaliza hapo wanaingia kwenye habari za simba na yanga au masumbwi, wakibadili kidogo basi wataongelea habari za kina zito kabwe, Lisu, CCM, CUF nk. Yani wabongo elimu hatuna, maarifa ya kutafuta maisha kama wenzetu wakenya na waganda hatuna, i mean sisi tupo tupo tu ilimradi tunalala na kuamka basi. Mengine eti tunamuachia Mungu 😂😂😂