Njombe: Serikali yakasirishwa na Kitendo cha CHADEMA kuzindua Mradi wa Maji, figisufigisu zaanza

Njombe: Serikali yakasirishwa na Kitendo cha CHADEMA kuzindua Mradi wa Maji, figisufigisu zaanza

Wananchi wa Njombe waipa heshima CHADEMA ifanye uzinduzi wa mradi ambao umeanzishwa na wananchi ili kuleta Maendeleo ya Watu.



CHADEMA inasisitiza Maendeleo ya Watu waziwazi katika sera zake 4 za Haki, Uhuru, Demokrasia na Maendeleo ya Watu.

Awali mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Njombe Rose Mayemba amesema wananchi wa kijiji hicho cha Uliwa waliamua kutengeneza mradi wao ili kufikisha maji kwenye makazi kutokana na kukosa huduma hiyo licha ya kuwa na vyanzo vya maji karibu ambapo mpaka sasa kaya 405 bado hazijafikiwa na mradi.

Akizindua mradi huo mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Nyasa Peter Msigwa aliyeongozana na viongozi mbali mbali wa kanda ametoa pongezi kwa wananchi bila kujali itiakdi za vyama kwa kufanikisha mradi huo uliopaswa kutekelezwa na serikali.

"Mmefanya kazi ya serikali kwa hiyo viongozi wenu wasikie kwamba mmefanya majukumu ambayo serikali ilipaswa kuyafanya,nyumba 150 sio haba na kwa hili tunaiambia serikali uwezekano wa kupata maji safi na salama inawezekana" amesema Mchg. Peter Msigwa

Emmanuel Mgulo kwa niaba ya wananchi wa kijiji cha Uliwa Njombe Tanzania amesema mradi huo umetekelezwa kwa takribani mwaka mmoja ambapo ulianza Desember 26, 2022 na kukamilika February 5, 2023 kutokana na fedha zilizopatikana kutoka kwa wananchi kwa njia ya uchangishaji.

HISTORIA YA KUKOSA MAJI ILIWEKWA BUNGENI 2019
Historia ya kukosa maji jimbo la Halmashauri ya Njombe mjini ilifika hadi Dodoma kupitia Edward F. Mwalongo aliyekuwa mbunge kupitia CCM 2015-2020 katika bajeti ya 2019/2020 akiwa bungeni , aliomba bila mafanikio kwa Mheshimiwa Waziri mtusaidie wananchi wa Lugenge wapate maji. Miundombinu ya usambazaji na matenki ya Vijiji vya Lugenge, Kiyaula, Kisilo, Ihalula na Otalingolo yalishakamilika lakini miundombinu ya kuleta maji kutoka kwenye chanzo mpaka leo haijakamilika.
 
ccm walivyo na akili za ajabu huo mradi wote wataubomoa kuwaadhibu wananchi
Huwa wanajifanya kuwaponda wapinzani kuwa eti wanakosoa tu lakini hawafanyi maendeleo yoyote, lakini wakiona wapinzani wanafanya maendeleo yoyote lazima wawahujumu.

Nilikuwa naona jinsi wanawagomea wapinzani kupeleka misaada mahospitalini, au kwenye taasisi mbalimbali za kijamii, kwakuwa wanaona wapinzani watapata nguvu za kisiasa. Hicho chama ni cha wachawi watupu.
 
Mradi wa Maji unaohudumia zaidi ya kaya 150, uliofadhiliwa na kusimamiwa na Chadema, na hatimaye kuzinduliwa na Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa, umesababisha Mtafaruku mkubwa huko Njombe.

Hii ni baada ya viongozi wa serikali kuwakalia kooni wanakijiji na kuwahoji kwanini waliwaleta Chadema kuzindua mradi huo.

Haya hapa ni Mahojiano ya viongozi hao na wanakijiji.

Kula chuma hicho:

View attachment 2631015
Tulishawambia Chadema inaongoza Nchi ccm inatawala tu.
 
CCM nawafananisha na mtu anayemng'ang'ania mwanamke wakati hawezi kumtunza. Lakini ikitokea mtu mwingine akaanza kutoa matunzo kwa huyo mwanaumke analeta nongwa ya hatari.
Kabisa yaani hivyo hivyo.
 
Sisi tupo hapa tunashangilia na kubishana nani alijenga ikulu ya chamwino? Yaani nchi masikini wananchi wake wanabishana uwepo wa IKULU MBILI na wafanyakazi wasiotulia ofisini wakisafiri usiku kucha
Maintenance cost ya ikulu zote mbili zitalemea walipa kodi sana. Huo nao ni ukweli tu.
 
Maintenance cost ya ikulu zote mbili zitalemea walipa kodi sana. Huo nao ni ukweli tu.
Wewe usiwe na wasiwasi kila kitu kipo kwa mantiki yake usihofu! Hata isingejengwa swala la kodi lipo pale pale kwani ni sheria na wajibu wa kila mtanzania kwa manufaa ya nnchi. Tuliza kiwewe chako!
 
Back
Top Bottom