Njombe: Serikali yakasirishwa na Kitendo cha CHADEMA kuzindua Mradi wa Maji, figisufigisu zaanza

Mradi wa CHADEMA??! Una maanisha nini hapo...? CCM nyie ni hamnazo..
Nyie ndo hamnazo hamna hata ofisi ya mkoa hapo njombe mmepanga sijui kama mzee wetu nyimbo kada wa CCM aliwaachia ofisi au ndo kasepa nayo...
 
Hii ni baada ya viongozi wa serikali kuwakalia kooni wanakijiji na kuwahoji kwanini waliwaleta Chadema kuzindua mradi huo.
Ile intelijensia yao inayonusa mikutano ya wapinzani ilikuwa wapi?
Wao wenyewe walikuwa wapi kugharamia huo mradi?
Wananchi wa Njombe siku zote wako ahead of the government kimaendeleo, kuna mwaka walitaka kuchangishana fedha ili kujenga barabara ya lami toka Njombe hadi Makete iliko hospital ya uhakika ya Mission Ikonda
 
Ni hivi kama mradi ulikuwa ni wa CHADEMA basi kuzindua sio mbaya ila kama Chadema ilishirikiana na jamii basi hata mkurugenzi angejulishwa kwa barua kwani siasa ni vita?
Ingekuwa kila mfadhiri anazindua mradi wake mbona ingekuwa vurugu
Nendeni na mkurugenzi mkauzindue, kwani CDM wamewazuia? Mkiona vipi muombeni mama Samia akauzindue.
 
Shida iko wapi?
 
Viongozi wa serikali na watendaji wao waache ushamba. Kinachotakiwa kwa sasa ni serikali kuboresha na kurasimisha huo mradi na kama kuna mapungufu katika design na ujenzi ni jukumu la serikali kurekebisha ili wananchi waendelee kupata huduma

Katiba mpya, na utawala wa majimbo ni dawa ya mambo aya.
Mtendaji kata, mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa, ded, Ras, wote Hawa ni ushenzi mtupu,
 
"Maridhiano" huko bado hayajawafikia?
 
Wafuate taratibu zipo Sheria za kuchimba visima wafuate
 
si cha wachawi tu ni mumiani pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…