NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Customer care mbovu sana hasa Mlimani city .Una active dormant account unaambiwa utapigiwa simu ikiwa sawa unakaa week nzima kimya, mpaka unaenda unaambiwa hatuja fungua account ilikuwa na matatizo kidogo.

Hivi kwa hali ya sasa money circulation ni ndogo plus ushindani bado mnakuwa wanzembe! naamisha pesa zangu na kufunga account.
 
Huduma yenu ya salary advance vp,mbona imekua kama bahati nasibu?mara uambiwe masaa 48 utashughuliwa,shida nn wakuu?
 
NAULIZA: je naweza kuchukua fedha kwa NMB wakala ikiwa sina kadi ya benki NMB?
 
kwanini mnachelewesha mikopo pasipo na sababu za msingi???
 
Nilipoteza muda wangu na kuacha kazi zangu siku mzima kujaza fomu ili nipate huduma hii ya nmb mobile lkn yapata mwezi sasa sijaona chochote
 
Kwangu hiyo nmb mobile imekuwa ni kero,nilipoteza line ya simu wakaniambia nikarudishe laini iliyopotea,nikafanya hivyo nikawapelekea ofisini ofisini bado hakuna kitu,fomu nimejaza lkn bado ni yaleyale, sasa sijui ugumu ni nini.ukifika pale MTU anakuambia nenda tu kwenye machine ukajiunge huku fomu tumeshaituma .yaani ni tabu tupu.
 
Salaam Radavi,
Tunajitahidi kukufikia kwa kuweka huduma mbadala za NMB Wakala na NMB Mobile karibu yako zaidi kuwezesha kufanya miamala ya kifedha kwa urahisi.
Gharama za kuhamisha hela Kwa NMB mtupunguzie kidogo aiseee maana ni maumivu
 
Pole sana Evonatus,
Tuandikie PM tufuatilie zaidi na kukusaidia kufuatilia.
 
Pole sana Nyiokunda,
Tafadhali tu PM taarifa zako tufuatilie na kukupa mrejesho
 
kwanini mnachelewesha mikopo pasipo na sababu za msingi???
Hello Mkorinto,
Karibu tukusaidie, ulikuwa unahitaji mkopo upi? na tunaomba taarifa zako kwa PM tukkusaidie kufanya ufuatiliaji na kukupa mrejesho.
 
NAULIZA: je naweza kuchukua fedha kwa NMB wakala ikiwa sina kadi ya benki NMB?
Hello Marashi,
Hii ni huduma ya kuchukua kiasi cha mshara wako kabla ya siku ya mshahara kuweza kujikimu na shughuli mbalimbali
 
Naomba muwe mnawatumia wateja wenu online bank statement kila mwezi kama CRDB Bank. Siyo mpaka mteja afunge safari mpaka branch yenu na kujaza fomu au logbook.so tiresome!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…