NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Nmb hongereni sana, naombeni mshughulikie idara ya mikopo kwenye matawi yenu. Maafisa mikopo wamezidi kuomba rushwa, hata mkopo wa laki tano anataka naye apewe chochote.

Pia baadhi ya watumishi wenu kutaja salio la mteja tena baa akiwaeleza wanawake sio jambo jema kabisa.

Mimi nilishuhudia hili na ikaniuma sana. Kusema mshahara wa mtu unaoingia benki baa sio maadili ya mtumishi wa benki hata akiwa amelewa hapswi kufanya hivyo.
 
Nmb hongereni sana, naombeni mshughulikie idara ya mikopo kwenye matawi yenu. Maafisa mikopo wamezidi kuomba rushwa, hata mkopo wa laki tano anataka naye apewe chochote. Pia baadhi ya watumishi wenu kutaja salio la mteja tena baa akiwaeleza wanawake sio jambo jema kabisa. Mimi nilishuhudia hili na ikaniuma sana. Kusema mshahara wa mtu unaoingia benki baa sio maadili ya mtumishi wa benki hata akiwa amelewa hapswi kufanya hivyo.

Hii ya kutaja salio la wateja bar ni kiboko... Wakati wanajua confidentiality ndio kila kitu kwa banks vinginevyo mtu anaweza dai fidia ya mamilioni.

Nadhan staff wao wanatakiwa kupigwa msasa aisee itawacost
 
mim naulizia huduma ya nmb mobile inasumbua sana ukituma hela hawatoi feedback kwamba hela imetoka au haijatoka

unajikuta mtu unatuma hela mara mbil au wanakulazimu kuuliza salio ,ambapo lazima ukatwe gharama ya kuuliza salio kwa hapo nashaur boreshen hii huduma mtu akituma hela either kwenda account ya bank au kwenye account either ya mpesa ,tigo pesa au airtel money ,inabid mtoe response mapema kwa maana hela inatumwa ila mteja anasumbuka kupiga simu kuuliia kama hela imefika badala ya mteja kujulishwa kwa ujumbe mfupi ,
asante nawasilisha
 
Kiwango cha kutuma fedha kupitia nmb mobile kiwe huru na sio kuwa limited (kwa sasa unatuma milioni moja tu kwa siku).

Si wengine hatutaki kwenda kupanga foleni ndefu bwana
 
Safi sana.

Ndio uzuri wa kufikisha ujumbe hata kama utapuuziwa ipo siku utafanyiwa kazi, vizuri sana NMB Tanzania
 
NMB Tanzania mimi bado sijafurahishwa na utoaji huduma katika benk zenu au branch zenu, wafanyakazi wenu karibu wote ni wavivu, wanadharau kwa wateja, customer care mbovu. Ukiomba kuonana na Meneja kutoa malalamiko utafikiri unaomba ukutane na vasco da gama wa magogoni. Naomba muwe mnawapa wafanyakazi wenu training kabla hamja waajiri ili kuongeza ufanisi wa kazi.

NMB Tanzania Account zangu zote nilizokuwa nimefunguwa na nyinyi nimezifunga, Nafurahia huduma ninayoipata FNB kwanza hawana longolongo kama za kwenu, nikipoteza kadi nikienda napewa mpya mda huo huo bila ya mizengwe wala kuangaishwa.

NMB Tanzania nendeni mkajifunze kutoa huduma za kibenki halafu ndio uje na pumba zako, mteja akiwa na matatizo anasumbuliwa utafikiri hizo pesa zake ni za kwenu. Pesa zangu halafu mniangaishe kama vile nawaomba mkopo?
 
Hongereni,,lakini tunapenda muanzishe huduma ya Visa Card..pia tatizo la network limeonekana sugu kwenu
 
Fumueni kitengo cha mikopo Tawi la Mbalizi road mbeya.Rushwa imezidi na mbaya zaidi kama mteja n jinsia ya kike loan officers wanadai ngono na pesa pia.mkikawia kujirekebisha Access bank watawachukua wateja wenu
 
nilisahau namba yangu ya NMB mobile nilipoomba wanibadilishie wamenitumia namba mbili tofauti je nitumie ipi kati ya hizo
 
Naomba mniwekee viwango mnavokata kutuma pesa kutoka nmb mobile to mpesa au Tigo pesa
 
Huyu dogo ni mlokole wa kutupwa. Alikuwa nyuma yangu mwaka mmoja chuo kikuu

jamaa anapiga kazi mpaka raha
yaani mchangamfu kwa mweli mwasandube hongera sana

mi nkifika yaani nkimkuta naenjoy sana the guy mzuri mnoo very responsible
ila mlokole yule anapiga maji kidogo
 
Yani NMB Tanzania mmenifurahisha kuja hapa jukwaani!

Kuna huu mtindo wa kuwa na madirisha zaidi ya Manne lakini yanayo Fanya kazi ni mawili na hili ni Tatizo kwenye matawi yenu Mengi na hili swala hukera sana tena sana kuna muda mwingine nashindwa kuelewa kwanimi mnaweka watu wawili wakati foleni ni kubwa na wahudumu ni wawili tuu!

Hili swala naomba mliboresha kabisa maana linakera sana!
 
Last edited by a moderator:
Tatizo foleni, ATM machine zipo bank tuu kwa nini hamuigi wenzenu? ATM ziwekwe sehemu nyingi mfano sheli, stand nk, Mimi ni mteja wa nmb lakini nakereka sana na mnavyotupanga bank. Ahsanteni
 
yaan kwa kero hizi zote zilizoelezwa na wadau mie pia zimenitokea sehem mbalimbali ila kuna dada mmoja apa Tanga tawi la madaraka ana nywele za kipilipili kweli kabisa kama una roho ndogo unaweza mlamba makofi alivyo na dharau, nilitaka kufungua account pale cha ajabu aliikataa barua ya mwajiri wangu na kunipa fomu akapitishe mtendaji wa kijiji eti ndio utaratibu wenu, mko kizamani sana, nikabidi nifungue CRDB, badilikeni acheni kuendesha benk kichama chama.
 
Hawa NMB bure kabisa mi nshalalamika nshatuma e mail saana!! Kipindi naomba mkopo niliupata lakini ilibidi nihonge!! Sidhani kama ntakopa tena NMB, na msipojiangalia TPB atachukua wateja wenu. NMB itabak benk ya kuchukulia mishahara tu.

Malalamiko yangu ni NMB Shinyanga branch. Hamna customer care, wana mapozi sana kuchukua statement tu unaweza ukakaa hata masaa 3, wafanyakaz wako busy kwenda kunywa supu, sometime teller mmoja yaani kero tupu.

Ila ukiwa na vibuku tano tano wanakusaidia kupotisha slip kwa nyuma!! Kwa nini nihonge ili niwekewe hela fasta. Kwani mkiweka matteler madirisha yote mtakufa?? Kwa nini muentertain biashara ya kujuana?? Nmeandika barua kwenye suggestion box ila hamna changes.

Nmb Manonga Branch ni kero!! Hapo bado Kero za ATM
 
Nilikuwa mtumiaji mzuri wa NMB nikiwa hapa Dar kwa kipindi kirefu....tabu nilipopangwa kikazi Bukoba nilijuta na kuhama haraka hadi leo sijaigusa akaunti yangu......kwanza wanahudumia kwa kujuana ......niliwahi kukaripiwa pale huduma kwa wateja nikiwa na cheki mkononi

kisa ni wahudumu kuwa wawili na hawana utaratibu wa kujua nani kafika kwanza apate huduma......kila nikimpa jamaa cheki yangu hapokei anahudumia anaowajua .......nilipomuuliza akanijibu "kwani lazima nikuhudumie mimi?"

.nilimwambia hii si sahihi nikamwambia ngoja nifikishe malalamiko kwa branch manager akajibu "ndugu mlango ule pale nenda".......huyo branch manager nae yupo yupo tu hadi mfanyakazi wa mle anayenijua toka huku Dar alipowaambia mimi ni nani ndio nikaanza kusikilizwa walau kwa adabu kidogo.......Wafanyakazi hawana uoga utafikiri watumishi wa umma......nakumbuka nilihamishia vijisenti vyangu CRDB tawi la Bukoba na pale nilipata huduma nzuri sana hadi naondoka kule.

wafanyakazi wao wachangamfu.....hata kama hawakujui wanakuhudumia kirafiki........toka 2009 sijaigusa NMB tena....
 
Back
Top Bottom