NMB wagoma kurudisha hati ya nyumba, japo deni lao limeshalipwa lote

Status
Not open for further replies.
Shukrani sana na ndio maana tumekuja huku ilo tupate mawazo mbalimbali tupate pa kuanzoa au hao NMB wakiona itakuwa sawa pia
 


Hivi ni kweli kuwa hao jamaa wanakata wateja shilingi 17,000/- kwa kila saving account ya kila mteja kwa kila mwezi ? 🙆‍♂️🤦‍♀️
 
Shukrani sana na ndio maana tumekuja huku ilo tupate mawazo mbalimbali tupate pa kuanzoa au hao NMB wakiona itakuwa sawa pia
Mkuu 'Nyabukika', nadhani tayari mmepata ushauri wa kutosha hapa kuweza kumsaidia huyo mama. 'THE BEEKEEPER' kaweka hata nanmba ya simu.

Mkifanikiwa hili usikose kurudi hapa JF kutoa mrejesho, maana mtandao huu unaweza kuwa na msaada kwa watu wanaoonewa kwa njia mbalimbali.
Mimi nimependa huu hapa.
Mwambieni mama asipoteze sana muda wake mwingi kwenda Benki. Miaka mitano kuzungushwa ni muda mrefu sana; sasa ni kuchukua hatua tu, basi.
THE BEEKEEPER kaweka namba ya simu, wasiliana naye kama anaweza kusaidia.
 
Kwahiyo bank watakuja kukiri kwamba hawajairudisha pamoja na kuwa wamelipwa? Mi ninachojua nimesharudishiwa, nani atapinga?
Mbona hueleweki?
Unamaana Benki ing'ang'ane kuwa walishamrudishia huyo mama hati yake?
Ingekuwa hivyo si wangekuwa walishamtoa njiani tayari kwa madai walisharudisha hati?
Hati inapotolewa Benki kupata mkopo kuna nyaraka zinazowekwa sahihi. Nina hakika pia inaporudishwa baada ya kumaliza deni kutakuwepo na makabidhiano kwa nyaraka. Sasa labda useme Benki waghushi sahihi ya huyo mama. Hili litakuwa swala tofauti kabisa na haya yanayojadiliwa.
 
Shukrani sana na ndio maana tumekuja huku ilo tupate mawazo mbalimbali tupate pa kuanzoa au hao NMB wakiona itakuwa sawa pia
Huyo mama ana barua ya kumaliza mkopo, maana wengine husema wamelipa deni lote kumbe kuna interest zimeongezeka, ikiwa kamaliza na alishawahia kuandika barua ya kuomba hati , basi achukue hiyo barua aandike barua ya malalamiko kwenda BoT akiomba apewe hati yake na benki wanavyomsumbua awacopy na Benki kwenye hiyo barua , apeleke barua customer protection desk(kama sijakosea) . Akifikisha hapo BoT watawaandikia barua tu NMB ambayo responce yake ni kati ya siku 7 au 14 , kama kweli alimaliza atapewa hati yake. Maana huko BoT ukichelewa kujibu tu fine bank inapigwa . Ikifail huko sasa ndio aende kwa wakili maana najua hii njia ya pili inagharama
 
Wewe ndo mjuaji sasa, Hakuna wakili anakupa demand notice ya siku 21, kisheria ni siku 90. Na Takukuru anaenda kudai kwamba anatengenezewa mazingira ya rushwa kabla hajachukua hatua zaidi. Kama mkopo kamaliza, kwanini wanamcheleweshea hati yake..?
Unaleta personal feelings kwenye kazi ambazo tunazifanya kila siku na watu wanasaidika. Hii njia ya wakili kuna gharama ndo maana tunamshauri apite PCCB kwanza then baada ya hapo kuna hatua za kufuata kama kuiandikia BOT au kwenda moja kwa moja mahakamani. Hii ya kupitia BOT ina pro na cons zake ambazo sina tu muda wa kuanza kukuelezea hapa.
 
Watakua wameikopea tena
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…