Nyakati Hizi Mbili Mwanaume Unatakiwa Umjali Sana Mwanamke

Nyakati Hizi Mbili Mwanaume Unatakiwa Umjali Sana Mwanamke

"Hapa bwana Pana changamoto sana,hawa viumbe hawa kuumbwa kuangalia au kuhudumia familia,sio asili yao hata ajitutumue vipi lakini ndani yao panawaka moto sana,hizi nyakati haitaji moto mwingine kutoka kwako wa sijui michepuko au mawasiliano na wengine ambao hayaeleweki"

🤔🤔🤔
 
View attachment 3477401

Kuna nyakati mbili mwanamke akipitia basi mwanaume unatakiwa uwe mpole sana na ujue kujali sana

Yani hapa ile haiba ya mamlaka na ushapavu wa kiume unaupunguza kidogo ili uende sambamba na nyakati hizo

Sehemu ya kwanza ni pale mwanamke anapokuwa mjamzito,huwa anapitia mabadiliko makubwa ya kihomoni na kihisia,ambayo yanamfanya asiwe yule mwanamke ambaye umemzoea.

Hivyo kuwa mpole na jitahidi kumuelewa kwamba huyu sasa hivi sio mwenyewe bali mtu mwingine kabisa,jitahidi kumsikiliza na kumliwaza sana,ni kipindi hiki anakuhitaji sana,anaweza kuwa na maudhi mengi lakini tambua anapitia mabadiliko makubwa,huu ndio wakati anaweza kukuagiza chips halafu ukizileta hazitaki,au saa nane usiku ukatafute soda ya baridi

Kwahiyo ni changamoto za msimu zitakwisha tu,ni wakati kumjali sana na kumuonyesha upendo wa hali ya juu sana,hakika anahitaji uwepo wako sana katika kipindi hiki.

Nyakati ya pili ni Pale ambapo mwanamke ndio anasimamia majukumu yote hapo nyumbani,kuna kipindi kwenye maisha unakutana na changamoto kadhaa,biashara inaweza kuyumba au kibarua kikaota majani,hapo itabidi mwanamke au mkeo asimamie show nzima.

Hapa bwana Pana changamoto sana,hawa viumbe hawa kuumbwa kuangalia au kuhudumia familia,sio asili yao hata ajitutumue vipi lakini ndani yao panawaka moto sana,hizi nyakati haitaji moto mwingine kutoka kwako wa sijui michepuko au mawasiliano na wengine ambao hayaeleweki.

Kuwa mpole lakini usipoteze uanaume wako,ila kuwa a loving husband na mjali sana mkeo,appreciate mchango wake walau kidogo unaweza kupunguza joto ndani ya nafsi yake.

Ni hayo tu!
Afande uko wapi....
 
Nyakati ya pili ni Pale ambapo mwanamke ndio anasimamia majukumu yote hapo nyumbani,kuna kipindi kwenye maisha unakutana na changamoto kadhaa,biashara inaweza kuyumba au kibarua kikaota majani,hapo itabidi mwanamke au mkeo asimamie show nzima.
Hapa huwa ni changamoto sana
 
Back
Top Bottom