Nyakati Hizi Mbili Mwanaume Unatakiwa Umjali Sana Mwanamke

Nyakati Hizi Mbili Mwanaume Unatakiwa Umjali Sana Mwanamke

Vipi na ile hali ya mwanamke kumchukia mume wake wakati akiwa mjamzito, huwa anaweza hata kuondoka nyumbani kabisa, hataki kukuona, unaweza kumzabatua makofi, hapo utafanyaje?
 
Hapohapo tena, kuna wanawake wakiwa wajawazito huwapenda waume zao sana kiasi kwamba mwanamke hataki uende kazini, anataka awe anakuona muda wote nyumbani, hapo napo vipi?
 
Hapohapo tena, kuna wanawake wakiwa wajawazito huwapenda waume zao sana kiasi kwamba mwanamke hataki uende kazini, anataka awe anakuona muda wote nyumbani, hapo napo vipi?
Sasa tena afadhali huyo ambaye anampenda mume wake sana,kuna ambao anatokea anampenda jirani bila kuongea nae hiyo siku hapakaliki

Mtu anaweza asiamini hili lkn yapo sana tu

Kwa kifupi ndio hayo tunayo Sema ni kipindi ambacho kina mitihani sana,wengine hupenda sex sana mpaka karibia bado mwezi mmoja wa kujifungua,na wengine wanaona kero ndio hao ambao wana kwenda nyumbani,kila mwanamke ina namna yake inavyomjia

Tunarudi pale pale kikubwa ni uvumilivu na subira kubwa pamoja na upendo

We fikiria kuna best yangu mmoja ananiambia wakati wa ujazito anakula chumvi kavu kama analamba glucose, ebu jiulize mtu anakula chumvi kama hana akili nzuri,ndio uone ni kipindi Chenye fujo nyingi sana
 
Hebu mnisaidie haya

Wanaobeba mimba vijijini nao wanasumbuaga waume zao wakatafute soda baridi usiku mkubwa? Au ice cream? Au miguu ya kuku?

Umefukuzwa kazi, uanze kumbembeleza mkeo kuhusu matumiz ya kila siku ndani kama ulivyokuwa na kazi!? Au mimi ndio sijaelewa na sio kwamba anatakiwa kuishi kwa namna situation iliyopo?

Asante mwanajukwaa
 
Back
Top Bottom