Nyakati hizi, wadada wanatongoza sana wanaume

Nadhani sio kwa sasa, hata hapo nyuma walitongoza sana pia. Labda tuseme aina za utongozaji kwa sasa zimebadilika.

Kihistoria, wanawake walikuwa wakitongoza wanaume kwa ishara za macho, na wakati mwingine rangi za mdomo walizopaka.

Mfano, rangi ya mdomo nyekundu ilikuwa ikitumika kwa kupeleka ujumbe kwamba wamezidiwa na hamu za kukutana kimwili.

Na wale waliotumia rangi nyeusi walikuwa wakipeleka ujumbe kwamba wao ni 'watundu' sana kwa mambo ya kitandani.

Na rangi ya 'pinki' ilibeba ujumbe wa 'nakupenda ila siwezi kukutamkia'. Hivyo, si wakati huu tu, ni nyakati karibu zote.

Na Waswahili husema, ukiona hali ya kutongozwa imezidi, basi ujue una umri wa utu uzima. Watoto huwa hawatongozwi.

Kwa hiyo, labda umri wako umesogea ndiyo maana unaona utongozaji wa wanawake umezidi.

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…