Nyakati hizi, wadada wanatongoza sana wanaume

Nyakati hizi, wadada wanatongoza sana wanaume

Nadhani sio kwa sasa, hata hapo nyuma walitongoza sana pia. Labda tuseme aina za utongozaji kwa sasa zimebadilika.

Kihistoria, wanawake walikuwa wakitongoza wanaume kwa ishara za macho, na wakati mwingine rangi za mdomo walizopaka.

Mfano, rangi ya mdomo nyekundu ilikuwa ikitumika kwa kupeleka ujumbe kwamba wamezidiwa na hamu za kukutana kimwili.

Na wale waliotumia rangi nyeusi walikuwa wakipeleka ujumbe kwamba wao ni 'watundu' sana kwa mambo ya kitandani.

Na rangi ya 'pinki' ilibeba ujumbe wa 'nakupenda ila siwezi kukutamkia'. Hivyo, si wakati huu tu, ni nyakati karibu zote.

Na Waswahili husema, ukiona hali ya kutongozwa imezidi, basi ujue una umri wa utu uzima. Watoto huwa hawatongozwi.

Kwa hiyo, labda umri wako umesogea ndiyo maana unaona utongozaji wa wanawake umezidi.

Ova
Kuna kitu nimejifunza hapa
 
Siku moja niliamua kutembelea akaunti yangu moja ya mtandao wa kijamii, baada ya kuingia 'inbox' nikakutana na sms (jumbe) nyingi za wadada na wamama mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali za Afrika; nyingi zilikuwa zinasema, 'mambo', 'hallow' n.k

Wengine wakiomba urafiki n.k; nikawa najiuliza kwa nini wote wawe jinsia moja tu, ndipo nilipo gundua, kwa sasa wanaume halisi wanahitajika sana.

Bahati nzuri nilichati nao, na nikawaambia nina wake pamoja na wajukuu; ingawa hiyo kauli haikuwapendeza sana.

Lakini ndio hivyo, ulimwengu umebadilika.​
Huo mtandao ni facebook huko mpaka majini yamo
 
Back
Top Bottom