Erick linus
Member
- Dec 1, 2014
- 9
- 0
kwa kweli wanaosema katiba inayopendekezwa ina dosari au kasoro ni wanafiki na hawafai ktk taifa hili,mana katiba imezingatia mambo yote ya msingi kwa mujibu na mustakabari wa maendeleo ya taifa letu la tanzania,nawaomba watanzania wenye lengo la kuendleza nchi yetu tuipokee katiba na muda ukifika tukapgie kura ya ndio,katiba yetu ni nzuri sana naomba tuipokee,kweli sita ni simba dume amehmiri sana kurupushan za bunge la katiba,hongera rahis kikwete kwa jitihada zako za kuwezesha bunge la katiba,
kwa kweli wanaosema katiba inayopendekezwa ina dosari au kasoro ni wanafiki na hawafai ktk taifa hili,mana katiba imezingatia mambo yote ya msingi kwa mujibu na mustakabari wa maendeleo ya taifa letu la tanzania,nawaomba watanzania wenye lengo la kuendleza nchi yetu tuipokee katiba na muda ukifika tukapgie kura ya ndio,katiba yetu ni nzuri sana naomba tuipokee,kweli sita ni simba dume amehmiri sana kurupushan za bunge la katiba,hongera rahis kikwete kwa jitihada zako za kuwezesha bunge la katiba,
Tafuta knywe google play application ya cmu yako andka katiba mpya utaipata
Hii hapa wadau...
KATIBA INAYOPENDEKEZWA NI BORA KULIKO YA SASA, HONGERA MH. RAISI, HONGERA WATANZANIA.
Katika historia ya uandishi wa katiba mpya duniani hakuna nchi yeyote ambayo iliwahi kuandika katiba mpya ikakidhi matakwa ya wananchi wote na taifa kwa 100%. Katiba si msaafu wala si biblia kwamba haiwezi kufanyiwa maboresho. Leo hii jambo ambalo tumeliona lina tija na manufaa kwa taifa na tukaliingiza kwenye katiba, kesho tutaliona halina tija na tutakubaliana kuliondoa au kuliboresha. Vilevile jambo ambalo leo tumeliona halina tija na kutoliingiza ndani ya katiba kesho tutaona umuhimu wake na tutakubaliana kuliingiza ndani ya katiba yetu.
Katiba inayopendekezwa imetambua haki za makundi mbalimbali kama vile wakulima, wafugaji, wafanyakazi, wasanii, vijana, wanawake na wengine. Pia katiba inayopendekezwa imetambua haki bunifu, mgombea, binafsi, maboresho katika muungano wetu sambamba na kuweka mfumo bora wa kusimamia rasirimali za taifa na kudhibiti mianya ya matumizi mabovu ya rasirimali. Kundi pekee ambalo linadhani halijatendewa haki katika katiba hii ni kundi la wanasiasa wachache ambao kwao tafsiri ya katiba bora ni ile inayokidhi maslahi yao ya kisiasa. Hili ni jambo ambalo watanzania hawana budi kulikataa.
Jambo la msingi ambalo kila mtanzania anapaswa kukubali ni kwamba katiba inayopendekezwa ni bora kuliko ile ya sasa. Wakati ambapo baadhi ya watu wakiipinga na kudai kwamba haiwezi kulivusha taifa letu, wapo watanzania tena asilimia kubwa ambao wanaiona katiba inayopendekezwa kuwa ni chombo madhubuti ambacho kitachochea maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hatuwezi kuwa na mtazamo mmoja, na ikifika wakati watanzania wote tukawa na mawazo yanayofanana basi tujue kwamba tunapaswa kujitazama upya. Kutofautiana kimtazamo ni jambo la kawaida na
hiyo ndiyo afya ya demokrasia iache ichukue nafasi yake. Tupingane kwa hoja bila kuhatarisha amani ya taifa letu.
Hongera Mh. Raisi Dr. Jakaya Kikwete kwa kazi kubwa uliyoifanya. Hili ni jambo la kihistoria ambalo halijawahi kutokea katika historia ya Taifa. Hii ni mara ya kwanza kwa Taifa letu kuandika katiba yake kwa kushirikisha wananchi wake. Yapo mataifa ambayo yaliwahi kuandika katiba zao kwa kutumia Bunge la katiba pekee, wapo waliogeuza Bunge la kawaida na kuwa Bunge la katiba. Kwa taifa letu, mchakato umekuwa wa kidemokrasia zaidi kiasi kwamba wapo wanazuoni, wanasiasa na mataifa mbalimbali ambao wameishangaa Tanzania kwa kuruhusu demokrasia kwa kiwango hiki. Kwa hakika Mh. Rais anastahili pongezi na daima watanzania tutakukumbuka na jina lako haliwezi kufutika katika fikra zao.
Bingo movie na bongo flavor za wabeba mzigo sawa poa ndani ya katiba.waislam nusu ya raia wa nchii hii hapana " tutawaundia sheria"
Kwani hakuna sheria ya haki miliki ? Kwani hii nchi ya wapuga vinanda peke yao
Bonge la fisadi sasa si tufanye katiba yetu ndo iwe ya kwanza jamani ya kukidhi matakwa yetu? Mbona unatetea udhaifu kaka
Hayo ni mawazo kama mawazo mengine,Lakini kwa nini baadhi ya vipengele kama kupunguza madaraka na kuwapa wapiga kura meno ya kuwawajibisha viongozi wao mara wanapowaona kutofanya majukumu yao?
Wewe ni mnafiki na hapa umetumwa!?