Hivi huwa unaamini kuwa una akili timamu? Ungejijua akili yako inapoishia, usingekuwa unaleta haya magazeti yako yaliyojaa ujuha na uwongo.
Kama umebakia na akili japo kidogo ya kujifunzia, fahamu yafuatayo:
1. Ni kweli wakati wa miaka ya 1950, Dar es Salaam na mikoa mingi ya pwani, population kubwa ilikuwa ya waislam.
2. Waislam wa Dar, ambapo palikuwa makao makuu ya nchi, pamoja na jamii nyingine, walimwunga mkono Mwalimu Nyerere, TAA na baadaye TANU.
3. Wakristo wamisionari wakatoliki, walimuunga mkono Mwalimu Nyerere katika kutafuta uhuru, japo ni kwa kificho, kwa kuhofia wakuu wa serikali na kutokiuka miongozo ya Kanisa, kuwa hawatakiwi kujiingiza kwenye masuala ya siasa.
4. Ni wamisionari wakatoliki wa shirika la Consolata Brothers and Sisters ndio waliomnunulia Mwalimu Nyerere ticket ya ndege kwenda UN kudai uhuru.
5. Mwalimu Nyerere alipoambiwa achague kuendelea na TANU, afukuzwe uwalimu, au aachane na TANU ili aendelee na uwalimu, alienda Tosamaganga kwa wamisionari wa Mt. Consolata kuwaomba ushauri, na akaeleza kuwa kwa sababu ya familia, atalazimika kuendelea na kazi aachane na siasa.
6. Wamisionari wa Mt Consolata Tosamaganga, walimshauri mwalimu aendelee na harakati za uhuru, na wao watahudumia familia yake. Mwalimu akaacha uwalimu, Mama Maria Nyerere na wanawe wakakabidhiwa kwa masista wa Mt Consolata Tosamaganga.
7. Kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika ilikuwa ni furaha kubwa kwa hawa wamisionari, na Padre wa Tosamaganga, wa shirika la Mt. Consolata, ndiye aliyeandaa wimbo wa Taifa, ndiyo maana ule wimbo umejaa maneno ya ibada, na tune ya nyimbo za dini.
Ni uwongo mkubwa kudai kuwa eti mwalimu alitengwa na Kanisa. Uhuru wa Tanganyika ulipiganiwa na jamii zote kwa viwango tofauti tofauti. Na hata TAA ilikuwa dhaifu sana, mpaka alipoingia Mwalimu Nyerere na kupewa uongozi. Hata hivyo huwezi kuwadharau au kuwapuuza walioanzisha harakati za kudai uhuru kwa kuanzisha chama cha TAA.