Ndiyo maana tunakushauri uwe unatumia akili hata kama unayo kidogo.
Unabisha mambo usiyoyajua. Familia ya Nyerere ilikaa kwa Mshume, wakati alipoenda kuanza kazi Pugu sekondari, siyo wakati wa harakati za kupigania uhuru. Wakati wa kupigania uhuru, na mwalimu kuamua kuacha uwalimu, familia yake ilienda kuishi Tosamaganga.
Unapenda sana kupindisha ukweli, na kutumbukiza maneno yako ya uwongo kwa sababu ya uozo wa udini uliopo moyoni mwako. Ufahamu kuwa Mwalimu Nyerere hakuwahi kufukuzwa uwalimu Pugu, bali aliambiwa achague kama anataka kuendelea na uwalimu, aachane na siasa, autumie muda wote kufundisha, au la kama anaona hawezi kuacha masula ya siasa, aamue kuacha kazi ya uwalimu, Mwalimu Nyerere akaamua kuandika barua ya kuacha kazi. Hakufukuzwa bali aliamua kuacha kazi.
Ufahamu pia hiyo inayoitwa Pugu Secondary, wakati huo ikiitwa Saint Francis ilikuwa ikimilikiwa na wamusionari wa Capuchin toka Ujerumani, wakati wale wa kule Tosamaganga walikuwa wamisionari wa Saint Consolata toka Italy, ambao hawakuwa na ukaribu wowote na watawala wa Kijerumani.