Mungu (mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote) angekuwapo, watu wasingehitaji kusema yupo.
Ukiona watu wanatetea sana hoja za kusema Mungu yupo, ujue ni kwa sababu Mungu mwenyewe hayupo na hivyo hawezi kujisemea kwamba yupo.
Mjadala mzima wa kubishania uwepo wa Mungu ni ushahidi kwamba huyo Mungu hayupo.
Angekuwapo, kila mtu angejua kwa uhakika yupo kiasi ambacho mjadala huu usingewezekana.
Hapa JF ushawahi kuona watu wanajadiliana hewa ipo, au maji yapo?
These are things that are so obvious we don't need to argue over.
Sasa kwa nini Mungu naye asingejidhihirisha kwa uwazi bila utata kwa watu wote hivyo na kutuepusha na mizozo hii?
Kutojidhihirisha hivyo ni ukatili. Watu wanauana kwa ubishi wa mambo ya Mungu.
Mungu huyo angekuwapo, asingekuwa mkatili hivyo.
Kuwapo kwa mzozo huu ni ushahidi kwamba Mungu huyo hayupo.