Eeembe dodo moja kwa pesaNamtafuta rafiki rafiki rafikii
Rafiki yako naani naani naanii
Rafiki yangu Meendee Meendee Meendee
Huu mti gani, wa mchongoma
Nikiukata haukatiki
Hata kwa panga, haukatiki
Hata kwa shoka, haukatiki.
Ubarikiwe sana, Na ziwe wenye heri Na baraka siku zako zijazo
ukimaliza hapo, ni kusubiri kuoga kula na kulala. Stress free life.Linanukaje Linanukaje. ...
Fwiii Fwiii kabwelaaaa
Nina ndoo yangu eeeh
Ya kuchoka maji eeeh
Maji ya dhahabu eeeh
Ya kuoga baba eeeh
Pamoja na mama eeeh
Watoto msitizame nyuma.... Yai bovu linapotaa.
ukimaliza hapo, ni kusubiri kuoga kula na kulala. Stress free life.
Mama wa mahaba upo ?Hahahahahahahaaaa looh hizi nyimbo baasi tuu.
Umekosea bwana. Mimi mama yenu sina nguvu tena za kuua simba, simba ni mkali, aliua baba, akaua mama sasa kimbieniiii!!!! Hao mtakimbia mpaka mmoja akamatwe.Mimi mama yenu,ee, ninanguvu tele,ee,zakumua simba ,ee,simbanimkali,ee, du utoto raha sana hapo walishashiba menu ya sambili hahahaha
Mimi mdogoMama wa kambo, mbo
Mbona wanitesa sa
Sasa naondoka ka
Kaa peke yako ko
Koti la babu bu
Bubu asemi mi
Mimi nasema ma
Mwengine aendelee..
Hizi nyimbo hata origin haijulikan..!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wimbo nilikua naupenda huu! Haswa pale kwenye UTAMU!Amina panda mlima
Siwezi kupanda
Kwann huwezi kupanda?
Naumwa na tumbo
Tumbo hilo kakupa nani?
Kijana hassan
Kwann usikatae ?
Naona utamu
Siku ya kwanza Utamu yes yes utamu
Siku ya pili utamu yes yes utamu
Siku ya tatu utamu yes yes utamu
Siku ya nne ng'aa ng'aa
Hivi akiyetunga nyimbo hii alifilia nn? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kwa kweli aisee [emoji23][emoji23][emoji23]mwanangu kua kua nikutume
nikutume wapi kwa mfalme
kuna ng'ombe zetu 12
mmoja kafa kaliwa nyani
nyani mkinda tumkindule
tusole visiga vya bwana chuma
bwana chuma gani simdodo
simkindu dawa kanabuba..
nadhani na kizaramo ndani humo wala tulikuwa hatujui maneno mengine maana ake nini😀
Kha! Ndo umenifungua macho... Sikuwai fikiria hiii! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]hapo si tulikuwa tunasema"tumpeleke mnazi mmoja" (mnazi mmoja hospitali)