Tatizo sio kuwa na uwezo! Ni wangapi walikuwa na uwezo?! Kama wewe ni mfuatiliaji wa Bongo Flavor huwezi kupinga kwamba Mavoko huyu sio yule wa miaka 4 iliyopita! Jingine ni kwamba watu mnajisahaulisha tu lakini ukweli ni kwamba Mavoko alishapotea kwenye game. Jamaa baada ya kupata mkataba Nairobi watu wakadhani ndo angerudi lakini wapi! Yeyote anayefuatilia BF hawezi kupinga kwamba ni WCB ndiyo ilimrudisha Mavoko kwenye game lakini inaonekana wazi kwamba kasi na taratibu za pale vimemshinda na matokeo yake watu wanakuja na sababu za kipumbavu kama kuhusisha na udini.