Nyumba ya Oscar Kambona sasa ni Feza Primary. Nini kimetokea?

Hivi unajua baada ya tanesco office ya kinondoni mbele yake kuna kiwanja kikubwa kimezungushwa uzio,mmiliki ni mama Maria Nyerere....
Miaka nenda rudi hakiendelezwi
Sasa sijui hana mpango huo au ndiyo
Familia haina mawazo ya biashara kuwekeza

Ova
😀 😀 😀 😀daah yani bi maza kabakia na kiwanja tuu...nyerere itakuwa familia inamlaani sanaa.. Migodi yotee hii
 
😀 😀 😀 😀daah yani bi maza kabakia na kiwanja tuu...nyerere itakuwa familia inamlaani sanaa.. Migodi yotee hii
Ah wameridhika mzee
Hata vijana kinondoni mtoto wa Nyerere mmja smbdy Joseph alikuwaga na eneo kubwa la biashara
Sema nahisi mzee hakuwalea watoto kwenye staili ya kukwea Mali

Ova
 
Kwa eneo lilivyo lile angekuwa mwingine pale angeporomosha maghorofa ya kufa mtu

Ova
sasa mkuu hana kitu yanii anaporomoshea nini... zaid zaid apewe favour hela za kujikim
 
Rashidi akasimamia Harusi ya Kambona?. hii kali.
 
Labda kosa la Mwalimu lilikuwa kuamini Waswahili tunaweza kuijenga nchi yetu wenyewe, Kambona hakuamini.

Sasa mnasafiri vipi na Mtu anayeamini kingine kama sio kuishi kupinduana.

Congo alikuwepo Shombe na Tanzania alikuwepo Kambona...Kambona aliamini na kuukumbatia sana Uzungu, utaona hata mtindo wake wa maisha ni wa kuiga Uzungu kupita kiasi...na aliamini bila Wazungu sisi hatuwezi kinyume kabisa na imani aliyokuwa nayo Mwalimu.

Mwalimu alimuamini Kambona lakini Kambona hakuaminika, na huo ndio ukweli..

Kufaulu au kushindwa kwa muelekeo fulani ni matokeo, na huwezi kufaulu au kushindwa bila kwanza kufanya...na sijui mnavyodhani siasa ilifeli mnatumia kipimo gani, maana sio lazima wote tuwe na mtazamo huo huo...na kama Mwalimu au siasa yetu ilifeli vipi nchi kama Congo wao walifaulu?.

Naona Vijana humu kila mmoja anaandika tu anachokidhania.
 
Hapo umeongea ukweli
 
Mwisho wa siku,leo kila mtu anaishi kama kambona
Mwendo ubepari tu watu kujilimbikizia Mali na fedha

Ova
 
Bora angewaacha wamiliki tu maana kungekua na nafuu mara dufu na tulivyo,Leo tusingekua tunakopa matrillion Ili kujengea matundu ya vyoo
Ni aibu alibanaaaaa mwishowe akaachia mwenyewe Tena Kwa kufail kubaya kabisaa!
Kwa hiyo Wazungu ndio wangetujengea?.

Kuna mambo mnapaswa kujionea aibu kuzungumza hadharani.
 
Mixed information.

Sasa hiyo nyumba bado ni mali ya familia ya Kambona ama?
 
fafanua mkuu,

majasusi wa kitz walimua mtoto wa kambona kwa kosa lipi?. aliwakosea nini?.

alikula chakula chenye sumu alichotegeshewa baba yake?.

alipigwa risasi kwa bahati mbaya baada ya kukosa target ambaye ni baba yake?.
Mkuu taarifa nyingi za humu ni za kupuuza tu wala usiumize kichwa, kila Mtu anatapika anachokifikiria au alichosikia kijiweni.
 
Ujamaa ni laana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…