Wewehujui unachokiongea Mkuu sikushangai sana ila nataka nikuambie kuwa Mahakama haiendeshwi kwa mihemko.
yaani watu wa download video whatsApp alafu waje kushitaki watu na kuwafunga?, hell no!.
Maana yake ni kuwa hata wewemtu anaweza akaingia adobe photoshop akatengeneza picha zako unavuta fanya matendo ya kiuhalifu alafu wakakukamata wakakupeleka Mahakamani kisha ukapigwa mvua.
Ndio mazingira kama haya yamefangika kwenye hii kesi. Usidhani kuishangilia hiyo hukumu ndio kutenda haki au kuwa salama hapana hata kidogo.
Lazima Mahakama ilipaswa kujidhihirishia bila kuacha shaka kuwa kweli zile video zilichukuliwa na kifaa fulani chenye kameraaina fulani na IMEI namba fulani na kifaa hicho ni ama simu au kamera na lazima iwepo Mahakamani na itolewe na kupokelewa kama ushahidi. Bila hayo madai yote yanaangukia pua.
Sasa watu wamekaa wakaona kesi hiyo kuangukia pua italeta taharuki na aibu na wasi wasi wakaamua kufunga macho bora liende. Sawabora liende ila likifika Mahakama Kuu ambayo ni Mahakama ya rekodi hilo hawatakubali na wakikubali basi hakuna aliye salama hasa kwa dunia ya sasa ya AI ambayo hadi sauti na video za sura yako zinaaeza jitengenwza mtandaoni. Watakukamata na kukufunga wakati wala hujafanya hayo mambo.
Funguka akili, jua kwanini watu wachache wanaoelewa wanapinga hayo maamuzi, sio kwamba wanafurahia kilichosemwa kufanyika ila ni wanaangalia matumizi ya tafsiri za sheria na mihemko ya umma.
Amka Mkuu.