Sasa Mkuu unaongea nini kiongozi?, ngoja nikupe shule kidogo maana nauhakika itakusaidia. Kwanza mtuhumiwa hana jukumu lakuthibitisha mashtaka dhidi yake yeye ni mtu asiye na hatia hata unapomuona pale Mahakamani sawa.
Pili, Jamhuri au upande.wa Mashtaka ndio wanatakiwa kuthibitisha mashtaka yao yote Mahakamani, kazi ya mshtakiwa ni moja tu kuonesha madhaifu ya madai na ushahidi wa Jamhuri au mshtaki. Na hawa walikuwa na wakili hivyo hakuna wasi wasi kuwa aliufanya hilo jukumu.
Sasa swali gumu hata kwa mtu aliye nje ya hii kesi ni nani aliyesambaza hizo video?, hauwezi kusema ni hao wakina Nyundo sababu hakuna kosa walilotiwa hatiani la kusambaza picha chafu.
Sasa kama halipo, umma ulizipata video hizo kupitianani?, mbona hayupo Mahakamani? Je alisahaulika au aliachwa kwa makusudi ya wazi sababu huyo angekuja kuwatoa wote hatiani?
Hayalabda tuulizane swali rahisi, zile video zilichukuliwa kwa kupitia kifaa gani?, kama ni simu ni simu aina gani? Je ilitolewa Mahakamani kama ushahidi? Ni simu ya nani? Huyo mtu ameshitakiwa kwa kusambaza video za ngono? Kwanini.hajashitakiwa? Au ni simu au kifaa kilichorekodi hakikupatikana?. Na kama hakikupatikana Mahakama imewezaje kuamini uhalali wa video hizo ambazo kwa teknolojia ilipofika inaweza kutengenezeka?, mwisho je Mahakama ilipuuza utaratibu wa kisheria wa kuchukua ushahidi wa kielekroniki unaotaka kifaa cha chanzo cha ushahidi kiweze kutambulika na kuletwa kama ushahidi?