G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 12,505
- 40,002
Sikuwahi kudhani kuwa itafika kipindi mimi nitoke nikutane na maiti nirudi mchana nikute bado zipo nirudi jioni nikute bado zipo na kesho yake bado nikutane nazo.
Hiki ndicho nilichoshuhudia mimi. Nilikuwa kila nikitoka napishana na maiti mbili zilizotelekezwa njiani kunazia tarehe 30 jioni mpaka tarehe 02 asubuhi yani jana. Hata wale waliojipa jukumu la kuzurura mitaani na magari yao walikuwa wakizopita bila kujali chochote.
Usiombe kuona niliyoyashuhudia. Nimeshuhudia wenye silaha wakipita na kufyatulia watu risasi bila kuwasemesha wala kuwahoji. Nimeshuhudia na nimeona watu wakianguka baada ya kupigwa risasi huku wakiwa hawajui kuwa walikuwa wamekwisha fyatuliwa. Yupo mmoja wakati anakimbia alihamaki "Nasikia baridi kiunoni" huku akiendelea kukimbia kabla ya kuangua hatua mbili tu mbele alizopiga. Ilikuwa ni risasi iliyofuatiwa na kuloa damu!
Mbaya zaidi nimeona maiti zikioza huku nikiwa sina jinsi zaidi ya kupishana nazo pale ninapotoka na kuingia. Najiuliza ilikuwaje sipati jibu. Najiuliza ni kwasababu gani napo pia sipati jibu.
Hali hii inahitaji uchunguzi maana tuliyoyaona yanatisha!