GE2025 Octoba 30 ya damu. Nilishuhudia maiti zikitelekezwa njiani siku tatu mfululizo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Tunza video hizo
 
Social engineering iliyofanywa na akina Mwalimu Nyerere.
Mnaongopeana. Hayo yanatokea sababu ya umaskini uliopo
South Africa wakiandamana napo huvamia biashara kubwa za watu na kuharibu
Kenya wakiandamana huvamia biashara kubwa na kuharibu.
Huko kote napo ni wajamaa? mwalimu nyererw napo aliwafanyia social engineering? Kwa nini mnapenda kujazana uongo badala ya kujadili ukweli
 
Unatoa uhai wa raia wako kisa madaraka kweli!! 😭
Kwani Nani kaanza vurugu,Askari au waandamanaji?Nakumbuka Watu walijisifia mitandaoni kwa kuvaa mabuti na sare za Askari,Amani ina umuhimu ikishapotea,Tujifunzeni
 
Hii miaka mitano inayokuja ni ya balaa tupu. Huyu mama anaenda kutumaliza. Nilijua tuna jeshi kumbe hakuna kila kitu, kwa Tanzania yetu pesa inanunua kila kitu.

Inauma sana na hapo bado kina Bashite hawajapewa wizara hakika tutakoma.
Sasa hivi nimejikuta nalichukia jeshi letu kuliko hata mshetani ya ccm.

Hatuna jeshi tuna uchafu tu ambao upo kwa ajili ya kuwalinda wadhalimu
 
Leo ndio nmefanikiwa kuona baadhi ya video, nmeumia sana 💔
Sidhani kma kuna mtanzania ambaye hajaumizwa na hizi video zinazoonesha vijana wetu wakiwa wamekatishwa uhai wao, labda mafwele na samia mwenyewe

Naamini kabisa hata wale machawa kindaki ndaki lazima wataanza kumchukia sana samia kwa huu ushetani alioufanya.
 
Kwani Nani kaanza vurugu,Askari au waandamanaji?Nakumbuka Watu walijisifia mitandaoni kwa kuvaa mabuti na sare za Askari,Amani ina umuhimu ikishapotea,Tujifunzeni
Mungu akurehemu shetani mkubwa wewe.

Tangu lini vurugu za watu ambao hawana silaha zikatulizwa na risasi za moto kma unapambana na magaidi?

Unajua hata sheria za umoja wa mataifa za kukabiliana na vurugu za waandamanaji?

Endelea kushabikia ushetani na mauaji, mwishoni wenu uko karibu mashetani wakubwa nyie
 
Aisee mimi nilikuwa mmoja wa magen z ambao tulikiwasha siku hiyo lakini mpaka leo naota ndoto za ajabu kwa yale nilioyashuhudia! Japo huku Tarime hakukuwa na maiti iliyotelekezwa. mpaka sasa hivi siamini kama nilitoka mzima kwenye lile tukio! nimeshuhudia mtu akiibiwa vitu vyake wakati amevunjika mguu na amezimia kwa maumivu!(sijui kama yule jamaa alipona ama alikufa!) aisee sidhani kama nitakuwa sawa kiakili kwa nilioyaona. aisee mniombee maana nahisi kuchanganyikiwa fulani hivi! hasa nikikumbuka almanusura nipigwe shaba wakati nakimbia lakini nilisukumwa na kuanguka. ile nimeanguka tu nasikia kitu kimepita spidi juu ya kisogo changu! kuangalia vizuri naona dogo mmoja ameanguka mita kadhaa mbele yangu akigaragara. haikuchukua muda nikaona ametulia!(nahisi alizimia ila alikufa baadae) mi nilibaki nimeganda kama nimemwagiwa maji ya barafu! bahati yangu ni kwamba mjeda mmoja alifika pale akaniamsha ili aone kama nimedanja au vip!(sisi wajeda kuna muda walitusave hadi waliwazuia mapolisi kutufyatulia risasi!)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…