Uchaguzi 2020 Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa: Vyama vya Siasa vinavyotaka kushirikiana Uchaguzi Mkuu vimeshachelewa kwa mujibu wa Sheria

..mbona hajazuia ushirikiano wa TLP na CCM.

..tena Nyahoza alikuwepo siku Mzee Mrema alipotangaza chama chake kushirikiana na CCM.
Huo ni ushirikiano sawa na ule wa lisu na maalim. Hautambuliki kisheria.
 
Marekebisho ya sheria yalifanywa ili kukilinda chama cha CCM kisipate upinzani wenye nguvu na hii ni baada ya UKAWA kuleta ushindani mkubwa 2015 na kwa hivyo sheria hii ilikuwa na nia ovu. Sioni kama vyama kushirikiana(cooperation) na kuungana (coalition) kuna madhara yoyote ambayo nia ya sheria ilikuwa inataka kutimiliza(Ku achieve).

Ili kuepuka nia yao hiyo ya kufanya upinzani usipate nguvu, viongozi wa ACT na CHADEMA wakiamua kushirikiana pasipo hata makubaliano ya maandishi wanaweza kufanikisha jambo hili kwa kuwaambia wanachama wao kuwapigia kura wagombea wenye nguvu/wanaokubalika na wananchi pasipo kutaja vyama. Wananchi wanaona na wanaelewa kuwa ni mgombea gani anakubalika na kwa nafasi gani.

Wagombea ambao watajipima kuwa hawana nguvu maeneo yao, wanaweza kupunguza kasi ya kufanya kampeni na hata kuacha pia. Mwananchi atatumia akili yake kuelewa kuwa ampigie nani uchaguzi ukifika.
 
Mwaka huu kwa taarifa yenu watu hawa shirikiani kivyama bali wanashirikiana kiuzalendo,Mtanzania kwanza vyama baadae ,na hivyo kila Mtanzania bila ya kujali itikadi anatoka chama gani,chaguo la kitaifa ni Mheshimiwa Tundu Lisu
 
Msajili hajui tofauti ya coalition na cooperation ?
 
Waambieni hawa watendaji waache double standards sisi wananchi sio wapumbavu
 
Misingi imara ya Amani, chini ya ccm imekuwa tunu kwenye bara Zima. Watanzania wapo tayari, kuilinda hiyo Amani kwa gharama zozote. Hivyo jidanganye kama wewe na vibaraka wenu kama mnaweza kuichafua, uone cha moto.
 
Misingi imara ya Amani, chini ya ccm imekuwa tunu kwenye bara Zima. Watanzania wapo tayari, kuilinda hiyo Amani kwa gharama zozote. Hivyo jidanganye kama wewe na vibaraka wenu kama mnaweza kuichafua, uone cha moto.
Siku zote huwezi jua thamani ya ulichonacho hadi utakapokuwa umekipoteza.
 
Hivi Lyatonga alisema anamuunga mkono nani vile?



CCM oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Huo ni ushirikiano sawa na ule wa lisu na maalim. Hautambuliki kisheria.

..uko sahihi 100%.

..lakini Msajili ameandika barua Sept 18, 2020.

..ktk barua yake inaelekea amekerwa na matukio ya mgombea wa chama "a" kumuombea kura mgombea wa chama "b."

..Naibu Msajili wa vyama alikuwepo ktk mkutano wa CCM ambapo Mzee Mrema alitangaza chama chake kumuunga mkono Jpm.

..Na alionekana kulifurahia tangazo hilo. Sasa wagombea wa vyama tofauti wameanza kufanya kile alichokifanya Mrema, Ofisi ya Msajili imeanza kuleta shida.
 
Huyo msajili yupo sawasawa? Kuna vyama vimesema vinataka kuungana sahizi? Anajibu asichoulizwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpe pole hana uwezo wa kuzuia hata 'baadhi' ya wana CCM kuchagua mwingine badala ya JIWE
 
imepita hio mwaka huu lazima watu wapate tabu
 
Wanaweza wakashirikiana kwa kuwaunganisha wapiga kura wao. Tar 28 wote wa upinzani wakampigia Lissu.
 
Wale wanaotaka kuungana ama kushirikiana wasije wakasema hawakuambiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…