radika
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 20,440
- 32,260
Kama una kumbukumbu vizuri, TLP walitangaza msimamo wao kipindi kipi? Na walitumia njia zipi kumuunga mkono Magufuli? Tuanzie hapa.
Waliandika barua?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama una kumbukumbu vizuri, TLP walitangaza msimamo wao kipindi kipi? Na walitumia njia zipi kumuunga mkono Magufuli? Tuanzie hapa.
Naona umeamua kutumia njia ya kujibu swali kwa kuuliza swali, tutafika kweli?Waliandika barua?
Naona umeamua kutumia njia ya kujibu swali kwa kuuliza swali, tutafika kweli?
Deadline ya lini wewe Mataga?Mrema aliwahi deadline
Muda gani huo Mataga?Ilikuwa ndani ya muda wa kisheria!
Hawawezi,kitanuka ndani na njeWanaweza kumtwanga tena
Hawashindwi mzeeHawawezi,kitanuka ndani na nje
Makubaliano yao waliyapeleka kwa msajili? Je yalipitishwa na mikutano mikuu ya vyama husika?Ilikuwa ndani ya muda wa kisheria!
Halafu wamelewa wanashindwa kujua Kama wako nchi ganiCCM matumbo joto... TL kamwaga pombe; walevi wote wa madaraka tutwatambua mmoja baada ya mwingine...
Unaliwa kisambusaDeadline ya lini wewe Mataga?
Nakumbuka video hiiHawa watu waliopewa........
Hakuna anayeogopa suala ni kufuata sheria na kanuniTume na ccm wanaogopa nini ikiwa wao wanaungwa mkono na tlp? Wanajua msala wake
Naibu wa msajili wa vyama vya siasa Dkt. Nyahoza amesema vyama vya siasa vinavyojipanga kushirikiana vimeshachelewa.
Nyahoza amesema muda uliowekwa kisheria kwa vyama vyenye nia ya kushirikiana kuingia mkataba wa kisheria umeshapita hivyo hakuna ushirikiano utakaoruhusiwa kwa sasa.
======
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA: VYAMA VINAVYOTAKA KUUNGANA, VIMESHACHEWA
Vyama vya Siasa ambavyo vinatarajia kushirikiana wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu bila kufuata Sheria ya Vyama vya Siasa kama ilivyoainishwa kwenye Kifungu Na.11 (a) cha Sheria hiyo vitakuwa vimevunja sheria.
Onyo hilo limetolewa jijini Dodoma na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, wakati alipofanya mahojiano kuhusu msimamo wa ofisi yake kwenye suala la ushirikiano wa vyama vya siasa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Nyahoza amesema kuwa ushirikiano wa vyama hivyo umeratibiwa vizuri kisheria ambapo vyama vinapohitaji kushirikiana vinapaswa kutumia vikao halali vya chama badala ya utashi wa mtu binafsi. Msajili Msaidizi Nyahoza ameongeza kuwa baada ya vikao halali kupitisha azimio la kufanya ushirikiano vyama husika vinapaswa kuwasilisha mkataba wa ushirikiano Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa miezi mitatu kabla ya mchakato wa uchaguzi kuanza.
“Vyama havijakatazwa kushirikiana bali vimewekewa utaratibu ili Tume ya Uchaguzi pamoja na taasisi zote zinazohusika na uchaguzi ziweze kujiandaa vizuri na kuimarisha ulinzi hasa wakati wa kampeni pamoja na kuvisaidia vyama vingine kuelewa wanashindana na vyama vya aina gani” alisema Nyahoza.
Kuhusu ushirikiano wa vyama vya siasa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2020 Msajili Msaidizi Nyahoza ameelezea kuwa mpaka sasa ofisi yake haijapokea mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kutoka kwa chama chochote cha siasa hivyo kwa mujibu wa sheria vyama ambavyo vina nia ya kushirikiana vimeshachelewa.
Aidha, Msajili Msaidizi Nyahoza amesema hadi sasa vyama vyenye usajili wa kudumu ni 19 na chama kimoja kina usajili wa muda na maombi ya vyama 16 bado yanafanyiwa upembuzi.
Maendeleo hayana vyama!