Ole Sabaya akamatwa pamoja na mabaunsa wake. Ahojiwa na Vyombo vya Dola

Ole Sabaya akamatwa pamoja na mabaunsa wake. Ahojiwa na Vyombo vya Dola

Kamanda Hamduni leo ni siku ya sita(6) toka uthibitishe kumkamata Olesabya na wenzie kwa tuhuma zisizo julikana maana hazijawekwa wazi kabisa. Kwa tuhuma ambazo zimekuwa zikitolewa na watu mbali mbali dhidi ya Ole Sabaya tulitegemea hadi sasa ameshafikishwa mahakamani lakini si kukaa mahabusu...

Kwakuwa zimeshapita siku zaidi ya tatu ni wazi hakuna mlichonacho dhidi ya Sabaya na pengine watu wameshindwa kutoa ushahidi wa kilicho kuwa kinaongelewa na watu. Ni vyema akaachiwa huru msiogope kusema maana Mama kasema wazi msiogope kuachana na case ambazo hazina ushahidi.

Takukuru mnavyomchelewesha Ole Sabya kumfikisha mahakamani mnategeneza mianya ya kumbabikia case maana kwa tuhuma zilizokuwa zinatolewa dhidi ya Sabaya inakuwaje hadi sasa hamjamfikisha mahakamani na watu wanasema wana ushahidi?

Mnakwama wapi? basi muachieni huru.

Tamko la mkurugenzi wa Takukuru

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), Kamishna wa Polisi Salum Hamduni AMETHIBITISHA kuwa wanamshikilia aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya kwa maojiano tangu May 25 mwaka huu. Kamishna Hamduni amesema Sabaya hakukamatiwa Arusha kama vyombo mbalimbali vya habari vilivyoripoti, bali alikamatwa jijini Dar akiwa na watu wawili waliotambuliwa kuwa ni "mabaunsa" wake na wote wapo mahabusu kwa mahojiano. Amesema wanaendelea kuhojiwa na wakipatikana na kesi ya kujibu watafikishwa mahakamani!
 
Taratibu ndugu,wacha atulie ndani aone utamu wa kukaa lock up,iwe fundisho kwa viongozi wengine wanaopenda kuwaweka raia lock up kwa sababu zisizo za lazima.
Wapinzani waliwekwa sana ndani bila sababu za msingi,kipande kimegeuka.
 
Taratibu ndugu,wacha atulie ndani aone utamu wa kukaa lock up,iwe fundisho kwa viongozi wengine wanaopenda kuwaweka raia lock up kwa sababu zisizo za lazima.
Wapinzani waliwekwa sana ndani bila sababu za msingi,kipande kimegeuka.
kwa hiyo tusipiganie haki tena kwa wote ......?
 
Wale wanajamvi wenye uwezo wa kuspy...connect dots kujua zilizokuwa post za Sabaya na majina aliyokuwa anatumia. Kuna majina yaliyokuwa yanamtetea hapa jamvini yamepotea tangu alipokamatwa!
 
Pindi ananituma niwakamate wasichana waliotajwa sikujua Mahusiano Wala ahadi zao za awali, nakiri kuwakamata na kuwapeleka kwake,Kuhusu kulawiti siwezi kutoa ushahidi maana sikuwa Naye ndani"

Denis Mlinzi wa SABAYA Ambaye yupo chini ya TAKUKURU tangu 25 May 2021 kwa Mahojiano
 
Back
Top Bottom