Ole Sabaya asomewa Mashtaka Sita (6) kwa Uovu aliotenda Hai. Aenda Rumande hadi Juni 18

Ole Sabaya asomewa Mashtaka Sita (6) kwa Uovu aliotenda Hai. Aenda Rumande hadi Juni 18

Yes. He was loved because he stopped CDM from their stronghold constituent, through evil tricks. Hii ya kuibia watu ni agenda yake sababu yeye ni mwizi. Hao mabaunsa aliwatolea wapi???
Sasa ngoje tuone,kitu kingine ni dharau wewe unagombana na Mkuu wa Mkoa kisa ni mwanamama na siyo chaguo kutoka ccm hivi huo ni utu.
 
Mkuu wa ulinzi na usalama wa wilaya akamate siraha na kufanya uvamizi usiku ni tuhuma kubwa sana. Hivyo mpaka anamfikisha mahakamani basi ushahidi umekamilika.

Achana na unyag'anyi wa kutumia siraha, uhujumu uchumi au kutesa na kupiga watu na utakatishaji pesa ni mashitaka ambayo hayana dhamana.

Lakini kwa kiongozi ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama kufanya makosa makubwa kama haya basi lazima Ocd, Oc-Cid, Dso afahamu anafanya uhalifu. Kama hawafahamu basi ni uzembe. Lakini kama walifahamu kwa miaka mitatu walikuwa wapi kumkamatisha? Watu watasema alilindwa!

Ok, ni mhalifu na anahatia, upelelezi umekamilika. Kwa nini akae rumande? Ilitakiwa Jumatatu asomewe maelezo ya awali, kesi ianze kusikilizwa na apate haki yake.
 
Huyu mtu hachomoki hakika...

Kwamba mpaka tarehe 18/6 wiki mbili zijazo atakuwa anaishi gerezani akinyea ndoo kama Mbowe jamaa yake alivyoishi kwa sababu ya hila za kisiasa tu za "Sukuma Gang" chini ya Mwendazake...??

Duuh, hebu ngoja tuone kama cheo chake cha U - DC na hizo pesa za wizi alizojilimbikizia kama zitakuja kumwokoa atoke gerezani...!!

Alinyanyasa na kuwadhalilisha watumishi wa umma hadharani. Sasa yuko mikononi wa watumishi haohao...

Bahati mbaya kwake, DPP si yule wa Sukuma Gang - Biswalo Mganga...

Mama Samia Mjanja sana. Alimtoa kwanza huyo kisha sukuma gang taratibu mmoja baada ya mwingine anashughulikiwa....!!
 
Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai Ole ngai Sabaya leo tar. 04.05 2021 amefikishwa mahakani akiwa na wenzake watano.

Sabaya peke yake amesomewa mashitaka sita likiwemo la Uhujumu uchumi na utakatishaji fedha pamoja na unyang'anyi kwa kutumia silaha.

Kesi imeahirishwa mpaka June 18 2021 na watuhumiwa wote wamerudishwa rumande kwani makosa hayo hayana dhamana.

Chanzo cha habari: Azam
Vijana tuna cha kujifunza katika maisha ,Muogope Muumba wako kila wakati .

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom