Ole Sabaya asomewa Mashtaka Sita (6) kwa Uovu aliotenda Hai. Aenda Rumande hadi Juni 18

Aliyekuwa mkuu DC wa Hai amesomea mashaka yake sita UHUJUMU UCHUMI UJAMBAZI KWA SILAHA KUTAKATISHA FEDHA NK AMEKWENDA RUMANDE MPAKA TAREHE 18/6/2021

View attachment 1808139
View attachment 1808140
View attachment 1808141

=======

Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34) na walinzi wake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha wakikabiliwa na makosa mbalimbali likiwemo la uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kupokea rushwa.

Sabaya ambaye alisimamishwa na Rais Samia Suluhu Hassan Mei 13, 2021 kupisha uchunguzi alifikishwa mahakamani hapo akiwa amefungwa pingu na baada ya wote kushuka kwenye magari ya polisi, walitakiwa kuchuchumaa na kisha kupelekwa katika chumba maalum na baadaye kuingizwa mahakamani.

Waendesha mashtaka wa Serikali, Tumaini Kweka, Abdallah Chaula na Tresla Garvas mbele ya Hakimu Mfawidhi, Martha Mahumbuga na Hakimu Mkazi Mkuu, Salome Mshasha wamesema Sabaya na wenzake walitenda makosa hayo Januari 20 na Februari 9, 2021.

Kweka amesema Sabaya na wenzake watano anatuhumiwa kwa makosa ya kuunda genge la uhalifu, uhujumu uchumi, kujipatia fedha kwa njia ya rushwa na utakatishaji fedha ambapo Sabaya alijipatia Sh90 milioni kutoka kwa mfanyabiashara, Francis Mroso mkazi wa kwa Mromboo ambaye alikuwa anatuhumiwa kwa makosa ya ukwepaji kodi ili amsaidie jambo ambalo ni makosa.

Pia, Sabaya na walinzi wake wawili, Sylivester Nyengu (26) maarufu kicheche na Daniel Mbura (38) wanakabiliwa na makosa mawili ya ujambazi wa kutumia silaha wakidaiwa kuyatenda Februari 9, 2021.

Wanadaiwa walimfunga pingu na kumpiga Bakari Msangi ambaye ni diwani wa CCM kata ya Sombetin na kumuibia Sh390,000 na pia katika eneo la Bondeni jijini Arusha wakitumia silaha, Sabaya na walinzi hao wanatuhumiwa kumpiga, kumtishia silaha na kumpora Ramadhani Ayoub simu na Sh35,000.

Kwa kuwa makosa hayo hayana dhamana watuhumiwa hao walipelekwa mahabusu Gereza Kuu la Kisongo na kesi hiyo kuahirishwa hadi Juni 18, 2021.
Ama kweli dunia duara

Ama kweli binadam wasijisahau kupitiliza kisa ya madaraka, utajiri, cheo, mamlaka au lolote lile.

Ama kweli malipizi ni hapa hapa duniani.
 
Mbona makosa machache watafute na mengine hata yafike 30 hivi.

Hayo anaweza kuchomoka.

Shida ni mahakama za bongo ovyo sana kama Lulu aliua na akatoka utashangaa na huyu kesho tu anakunywa bia mtaani.
 
Aliyekuwa mkuu DC wa Hai amesomea mashaka yake sita UHUJUMU UCHUMI UJAMBAZI KWA SILAHA KUTAKATISHA FEDHA NK AMEKWENDA RUMANDE MPAKA TAREHE 18/6/2021

View attachment 1808139
View attachment 1808140
View attachment 1808141

=======

Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34) na walinzi wake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha wakikabiliwa na makosa mbalimbali likiwemo la uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kupokea rushwa.

Sabaya ambaye alisimamishwa na Rais Samia Suluhu Hassan Mei 13, 2021 kupisha uchunguzi alifikishwa mahakamani hapo akiwa amefungwa pingu na baada ya wote kushuka kwenye magari ya polisi, walitakiwa kuchuchumaa na kisha kupelekwa katika chumba maalum na baadaye kuingizwa mahakamani.

Waendesha mashtaka wa Serikali, Tumaini Kweka, Abdallah Chaula na Tresla Garvas mbele ya Hakimu Mfawidhi, Martha Mahumbuga na Hakimu Mkazi Mkuu, Salome Mshasha wamesema Sabaya na wenzake walitenda makosa hayo Januari 20 na Februari 9, 2021.

Kweka amesema Sabaya na wenzake watano anatuhumiwa kwa makosa ya kuunda genge la uhalifu, uhujumu uchumi, kujipatia fedha kwa njia ya rushwa na utakatishaji fedha ambapo Sabaya alijipatia Sh90 milioni kutoka kwa mfanyabiashara, Francis Mroso mkazi wa kwa Mromboo ambaye alikuwa anatuhumiwa kwa makosa ya ukwepaji kodi ili amsaidie jambo ambalo ni makosa.

Pia, Sabaya na walinzi wake wawili, Sylivester Nyengu (26) maarufu kicheche na Daniel Mbura (38) wanakabiliwa na makosa mawili ya ujambazi wa kutumia silaha wakidaiwa kuyatenda Februari 9, 2021.

Wanadaiwa walimfunga pingu na kumpiga Bakari Msangi ambaye ni diwani wa CCM kata ya Sombetin na kumuibia Sh390,000 na pia katika eneo la Bondeni jijini Arusha wakitumia silaha, Sabaya na walinzi hao wanatuhumiwa kumpiga, kumtishia silaha na kumpora Ramadhani Ayoub simu na Sh35,000.

Kwa kuwa makosa hayo hayana dhamana watuhumiwa hao walipelekwa mahabusu Gereza Kuu la Kisongo na kesi hiyo kuahirishwa hadi Juni 18, 2021.
Kama makosa yenyew ni haya tu jamaa anachomoka asubuhi na mapema sana yaani kabla jogoo hajawika. hapo makosa ni mawili tu akipanchi moja makosa matatu yanadondoka.
 
Dogo mimi ni mtu mwenye msimamo. Unaposema mimi bingwa wa kusifia madhalilu unakosea
Ukiambiwa uthibishe kwa ushahidi kihusu dhalimu utaweza?

Kama Sabaya ana makosa nini kulemba? Kwa nini msianze kusikiliza kesi?
Daah, wewe jamaa boss wako saivi kalala rumande. Ulipandisha nyuzi nyingi sana humu kumsafisha lakini wapi. Pole sana Mlaki
 
Maisha yanakwenda kasi sana,Duu Lengai Ole Sabaya anafikishwa mahakamani,ananyimwa dhamana?,Duuu hii dunia ni dunia ya maajabu sana,ndo hapa unaamini maisha hayana fomula
 
Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai Ole ngai Sabaya leo tar. 04.06 2021 amefikishwa mahakani akiwa na wenzake watano.

Sabaya peke yake amesomewa mashitaka sita likiwemo la Uhujumu uchumi na utakatishaji fedha pamoja na unyang'anyi kwa kutumia silaha.

Kesi imeahirishwa mpaka June 18 2021 na watuhumiwa wote wamerudishwa rumande kwani makosa hayo hayana dhamana.

Chanzo cha habari: Azam
View attachment 1808137
Tuishi na watu (wenzetu) vizuri, sponsor hufariki.
 
Kwa makosa haya sishangai jamhuri kuendelea kupoteza case .....hapo naona makosa hayazidi matatu au mawili kuna kosa moja akilipangua basi ana baki kujibu kosa moja halafu kazi inakuwa imekwisha.
 
Wakati wanatunga sheria ya kuwalinda viongozi, DCs walisahaulika. Huyu mutu makosa anayohukumiwa nayo yametokana na harakati za kutumikia ofisi ya umma...
 
Back
Top Bottom