Ombi kwa Rais Samia: Japo wengi wape, wachache pia wasikilizwe, Hoja ya kufanya minimum reforms za Katiba ni hoja ya msingi sana kuliko hata Sheria!

Maridhiano yametupiliwa mbali na CCM,

Na Kwakuwa HAKI haiombwi;

Maandamano ya Amani ndo njia pekee ya kuzibua masikio ya Watawala.

Karibu katika maandamano ya Amani Kwa mwamvuli wa PRESS Ili kuzipata hizo HAKI 3 muhimu!!
Na huyu Pascal Mayalla akumbuke kuwa, "... there's no sweet without sweat.."

Hakuna haki inayokuja pasipo kutoa jasho na wakati mwingine kufa kwanza na baadae kufufuka..

Yesu Kristo aliukomboa ulimwengu (watu na uumbaji wa Mungu) toka ktk mikono ya ibilisi - shetani Kwa gharama ya kumwaga damu na mauti..

Inaeleweka kabisa kuwa, katika harakati za kupambana na hayawani hawa (ma - CCM), damu zilishamwagika nyingi sana mfano kina Tundu Lissu, Mdude Nyangali, Ben Sanane, Alfonce Mawazo na wengine wengi..

Haina budi kabisa wachache waumie na ikibidi wafe au wamwage damu kwa ajili ya wengi kukombolewa..

Ushauri wako ndugu Pascal Mayalla haufai. Mungu muumba siku zote ni Mungu wa haki na huwalinda na kuwapa neema kubwa wenye haki..!
 
Mwl Nyerere angetumia ushauri autoao Mayala,

Hadi Leo tungekuwa utumwani.
 
Mkuu Uzima Tele, hili kuhusu haki sio hisani, ni stahiki, na hailetwi kwenye kisahani cha chai, inapiganiwa na sometimes kwa gharama ya machozi, jasho na damu, Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki

Kwa vile Mama ameonyesha kwa kauli na matendo Haki Huinua Taifa! Rais Samia kwa Kauli na Matendo ameonesha ni mtu wa Haki. Akitekeleza hili kama alivyosema, atabarikiwa, Tanzania itabarikiwa
na Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
P
 
Tatizo unayemueleza ana ufahamu huo
Elimu yake inamuwezesha kuelewa hili?
 
Tatizo unayemueleza ana ufahamu huo
Elimu yake inamuwezesha kuelewa hili?
Maza, japo sii mwanasheria, ila yuko vizuri sana kwenye uelewa na nimeeleza hapa Rais Samia Japo Si Mwanasheria, Lakini Anaijua Katiba ni Sheria Mama Yenye Haki Zote Ndani ya JMT. Je Aruhusu Haki Hizi Ziporwe Tena? Au, Azirejeshe?

Na pia nikamuombea msamaha kuhusu huu muswada wa sheria ya uchaguzi wenye ubatili Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi. Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!
P
 
Mambo ya kijitabu!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
S
Awamu zilizopita, mihimili miwili, Serikali na Bunge zimepoka haki ya Mtanzania kuchagua na kuchaguliwa zilizotolewa na Katiba ya JMT ya mwaka 1977, Serikali yetu na Bunge letu zilipata wapi uwezo na mamlaka ya kuzipora haki hizi?!.
Sema ukweli nao utakuweka Huru.

Hongera Pascall.

Nina imani hii ni Voice from Within.
 
Natamani kusikia Rais Samia angejibu nini kwenye hili Swali lako.
 
Sasa sijui kipi kimeshindikana mpaka mambo yamekuwa vile wakaja na miswaada ile isiyo na mbele wala nyuma.

Inawezekana mafisadi wana nguvu sana.
 
Rais Samaia atafanya kitu kuhusu katiba kabla ya uchaguzi serikali za mitaa ili kuleta maelewano ya kitaifa kwa msingi wa 4 R wengine ndani ya CCm wasingependa kwa sababu zao. Taifa linasononeka. Mama tulipofikia okoa Taifa,weka Legacy
 
 

Attachments

  • Screenshot_2023-08-17-16-20-00-45.jpg
    41.8 KB · Views: 2
Sema ukweli nao utakuweka Huru.

Hongera Pascall.

Nina imani hii ni Voice from Within.
Mkuu Bush Dokta, hii sio voices from within, hii ni sauti tuu ya katiba ya JMT ya mwaka 1977. Katiba ndio the supreme law, ndio sheria mama inayotoa haki zote, Serikali, Bunge na Mahakama ziko chini ya katiba, hazina uwezo wala mamlaka kuondoa haki yoyote iliyotolewa na katiba. Katiba ikatoa haki ya kuchagua na kuchaguliwa, Serikali yetu na Bunge letu likaibakiza haki ya kuchagua, lakini zikaipora haki ya kuchaguliwa na kulazimishwa lazima kwanza ujiunge na chama cha siasa, uwe mwanachama wa chama cha siasa, uombe ruhusa kwa chama cha siasa, kikuruhusu, kikudhamini ndipo ugombee uongozi!.
P
 
Pascale hilo la kusema kuwa Mwinyi alitumia busara kuikubali 20% kwenda kwenye mfumo wa vyama vingi siyo kweli kuwa aliamua hivyo kwa hiari yake au mapenzi yake.

Kipindi hicho viongozi wote wa Afrika walikuwa chini ya mbinyo wa jumuia za kimataifa hasa wale wahisani wa maendeleo yetu kiuchumi.

IMF na WB walilazimisha nchi kuingia kwenye mfumo wa kidemokrasia wa vyama vingi.
 
Mimi bado najifunza Katiba mpya ya Kenya

Naona Ruto anaipondaponda Mahakama kana Kwamba si Muhimili wa Dola
Hawezi kuipanda panda bali anajaribu lkn amekutana na wana sheria wapo imara.

Mbona juzi kanyoosha maelezo kwa umma kuhusu mahakama?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…