Ombi kwa Rais Samia: Japo wengi wape, wachache pia wasikilizwe, Hoja ya kufanya minimum reforms za Katiba ni hoja ya msingi sana kuliko hata Sheria!

Ombi kwa Rais Samia: Japo wengi wape, wachache pia wasikilizwe, Hoja ya kufanya minimum reforms za Katiba ni hoja ya msingi sana kuliko hata Sheria!

Muda hautoshi, white paper inahitaji ushirikishwaji wa wadau , kwa walau mwaka mzima.

Tuendelee kutoa elimu kwa wadau kwanza waelewe, hasa wananchi, chadema wao wanapigania madaraka na vyeo tu, hawana ajenda za wananchi
🙄🤔
 
Na huyu Pascal Mayalla akumbuke kuwa, "... there's no sweet without sweat.."

Hakuna haki inayokuja pasipo kutoa jasho na wakati mwingine kufa kwanza na baadae kufufuka..

Yesu Kristo aliukomboa ulimwengu (watu na uumbaji wa Mungu) toka ktk mikono ya ibilisi - shetani Kwa gharama ya kumwaga damu na mauti..

Inaeleweka kabisa kuwa, katika harakati za kupambana na hayawani hawa (ma - CCM), damu zilishamwagika nyingi sana mfano kina Tundu Lissu, Mdude Nyangali, Ben Sanane, Alfonce Mawazo na wengine wengi..

Haina budi kabisa wachache waumie na ikibidi wafe au wamwage damu kwa ajili ya wengi kukombolewa..

Ushauri wako ndugu Pascal Mayalla haufai. Mungu muumba siku zote ni Mungu wa haki na huwalinda na kuwapa neema kubwa wenye haki..!
🤔💭
 
Bahati nzuri au mbaya ni kuwa hatuna watafiti wa kisiasa wanaoweza kufanya tafiti kutambua madhara ya kuendelea na utaratibu wa kutumia katiba hii kwa miaka 30 ijayo!
Je, tutakuwa tumepiga hatua kiasi gani katika siasa na maendeleo kwa wananchi wetu.
Je, tutakuwa tumepoteza kuasi gani.
Mambo mengine ukifikiria sana unajikuta unaona aibu mwenyewe. Hivi ni nani anafaidika kwa kuendelea kukumbatia mifumo mibovu ya utoaji wa haki hapa nchini? Na atafaidika hadi lini ili atosheke?

Yaani viongozi wanatambua mifumo mibovu ya utoaji haki nchini ilivyo hadi wakatoa ulaji kwa watu wengine kwa kuanzishi kitu kinaitwa sijui SAMIA NINI KILE.
👍👌👏🙏
 
Duh...!. Dingi na Maza ndio walikuwa huko, sisi tumezaliwa watoto 8, we can't be all 8 wote tuwe watoto wa nyoka!, baadhi yetu ni mijusi tuu!. Mimi ni mjusi!. Ningekuwa ni mtu wa huko ningeweza kupandisha mada kama HII kumwambia boss wangu ambaye amepania sana?.
Usiniogope bure, mimi sio wa huko!
P
🤣🤣🤣
 
Wanabodi,

Kwa sisi tuliokuwepo enzi za Tume ya Jaji Nyalali kukusanya maoni ya Watanzania kuhusu kuendelea na mfumo wa chama kimoja au vyama vingi, asilimia 80% ya Watanzania walitaka tuendelee na mfumo wa chama kimoja, ni asilimia 20% tuu ndio waliotaka mfumo wa vyama vingi, lakini Rais Mwinyi aliongozwa na busara, badala ya wengi wape, wengi akawasikiliza tuu la wachache ndio wakapewa, na Tanzania tukaingia kwenye mfumo wa vyama vingi, bila kubadili katiba, ambapo mpaka leo, mpaka kesho, japo nchi yetu ni nchi ya vyama vingi, lakini katiba ya JMT ya mwaka 1977 bado ni katiba ya chama kimoja, uwanja wetu wa mchezo wa siasa ni uwanja tenge, umelalia upande wa chama kimoja, hivyo wale wengi waliokataa vyama vingi, bado wanaendelea kukichagua chama chao kimoja kile kile mwaka hadi mwaka, na bila mabadiliko ya kweli ya katiba, chama hiki kinaendelea kutawala Tanzania milele!.

Mada ya leo ni kuhusu haki, ya wengi wape, ila wachache pia wasikilizwe. Katiba ndio sheria mama inayotoa haki zote za watu wote wa Tanzania. Hili ni ombi kwa jicho la Rais Samia na sikio la Rais Samia kuziangazia haki tatu kuu kwenye katiba yetu ambazo zimeporwa na serikali zilizotangulia.

Serikali, Bunge, Mahakama, hazina uwezo wala mamlaka ya kupora haki yeyote iliyotolewa na katiba, kwasababu katiba ni supreme na mihimili hiyo yote mitatu iko chini ya katiba!.

Awamu zilizopita, mihimili miwili, Serikali na Bunge zimepoka haki ya Mtanzania kuchagua na kuchaguliwa zilizotolewa na Katiba ya JMT ya mwaka 1977, Serikali yetu na Bunge letu zilipata wapi uwezo na mamlaka ya kuzipora haki hizi?!.

Mpaka hapa ninapoandika haki hizi bado zimeporwa!. Mtanzania hana haki ya kuchagua kiongozi anayemtaka, kwasababu haki ya kila Mtanzania kugombea imepokwa na kakikundi kadogo ka watu wanaoitwa chama cha siasa. Chama cha siasa ndio kimepewa mamlaka ya kuamua nani agombee na sio wananchi!, matokeo yake wananchi wanalazimishwa kuchagua viongozi walioletewa na vyama vya siasa kitu ambacho sio sahihi kabisa!, sio haki na ni dhambi!, usikute ndio sababu karma kila siku inawatafuna baadhi ya viongozi wetu!.

Sasa tunaye Rais Samia Suluhu Hassan. Ujio wa Rais Samia ni fursa kwa Watanzania kurejeshewa haki katiba zilizoporwa. Ila japo Rais Samia ni fursa, iliyokuja kwa kudra tuu za Mwenyezi Mungu, na Rais Samia, analiishi jina lake la Suluhu kwa kauli na matendo kwa kuleta suluhu ya kweli ya mtanziko wa kisiasa unaolikabili taifa letu, na tayari ameonyesha kwa kauli na matendo anataka maridhiano ya kweli ndio maana amekubali kubadili sheria mbalimbali, mabadiliko haya ni fursa ya kuzirejesha haki za msingi za Watanzania zilizoporwa.

sasa kwa vile mzizi wa fitna uko kwenye katiba, jee Rais Samia ataichangamkia hii fursa by practicing what she preach? Au kwa vile aliyezipora haki hizo sio yeye, yeye kaingia kazikuta zimeishaporwa na sasa anachofanya yeye marekebisho cosmetics tuu ya sheria, lakini zile haki porwa za katiba, haziguswi!.

Kufanya mabadiliko ya Sheria mbovu bila kuigusa katiba, je sio inamaanisha she was just paying lip services by not practicing what she preaches?.

Naomba kuanza kwa kurudia kuhusu katiba
  • Katiba ni Nini?. Katiba ni kakitabu kadogo tuu chenye kkurasa kadhaa. Kakitabu haka ndio kila kitu kuihusu Tanzania yetu, hakuna yeyote aliye juu ya Katiba.
  • Katiba ni ya Kazi Gani. Katiba ndio msingi Mkuu na muongozo wa uendeshaji wa nchi yetu, aambapo inatoa haki zote, sheria zote, taratibu zote na kanuni zote, za kufanya kila jambo, lazima zitokane na katiba.
  • Katiba ni ya Nani? Katiba hii imetungwa na Bunge maalum kwa niaba ya Wananchi,kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia.
  • Katiba hii imetoa haki fulani fulanj kwa Watanzania, haki hizo ziko nyingi, lakini haki kuu ni haki 3. Uraia, Kuchagua, na Kuchaguliwa!. mimi nitajikita kwenye haki 3 Kuu za Mtanzania.
  • Haki kuu ya kwanza ni haki ya uraia. Mtu yoyote akizaliwa ndani ya ardhi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mtu huyu anakuwa ni raia wa Mtanzania kwa kuzaliwa, haki hii ni haki ya kwanza ya msingi ambayo ni haki ya kuwa Mtanzania. Haki hii haiwezi kuondolewa na mamlaka yoyote, ila unaweza kuipoteza endapo utaukana Uraia wako. Hivyo ile sheria yetu ya kuwa mtu akichukua uraia wa nchi nyingine yoyote, anaupoteza Utanzania wake, ni sheria batili kinyume cha katiba, ila ubatili huu, haujabatilishwa kwasababu hakuna aliyefungua shauri mahakamani kuipinga. Ijue Katiba ya JMT-1: Katiba ni nini, ya nani, ya kazi gani? Msemo "Katiba ndio kila kitu" Una maana gani? Katiba ina umuhimu gani? Katiba ni mali ya wananchi, "we the people"
  • Haki kuu ya pili ni haki ya kuchagua iliyotolewa na ibara ya 5 ya katiba ya JMT. Haki hii ni kila raia wa Tanzania anapofikisha umri wa miaka 18, ana haki ya kuchagua kiongozi wake. Haki hii inatekelezwa kwa kila mtu kujiandikisha kupiga kura. Haki hii haiwezi kuondolewa na mamlaka yoyote. Kwa Tanzania, haki hii imefinyangwa finyangwa kwa baadhi ya watu kunyamaza haki hii, kwa kufungwa magezani, wagonjwa mahospitalini, na Watanzania walioko nje ya nchi. Kufuatia maendeleo makubwa ya Teknolojia, na andikishaji unaotumia BVR hivyo kwa kutumia biometric data, kitambulisho cha taifa au passport ambavyo vyote vina biometric data, vinaweza kutumika kuwawezesha Watanzania wote popote walipo kumchagua Rais wa Tanzania na rais wa Zanzibar popote pale walipo.
  • Haki kuu ya tatu ni haki kuchaguliwa kupitia ibara ya 21 ya katiba ya JMT kwa mtu mwenye miaka 21, yuko huru kugombea nafasi yoyote ya uongozi kuanzia serikali za mitaa hadi serikali kuu. Haki hii ni haki ya msingi na haiwezi kuondolewa na mamlaka yoyote. Kwa Tanzania, haki hii ya kila Mtanzania ana haki ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi na kuchaguliwa imefutwa kwa kuchomekewa shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa. Shurti hili ni batili!.

Hitimisho
Waungwana wanapotaka jambo lao kubwa, wakakaa pamoja kukubaliana, na kukuta wamepewa kidogo tuu ya kile walichotarajia, hawaziri, hawasusi, wala kutaka kupeleka watu barabarani, waungwana, hupokea kidogo walichopata na kuendelea kuomba kikubwa.

Kwa vile matatizo makubwa ya siasa zetu yako kwenye katiba, tulianza mfumo wa vyama vingi kwa katiba ya chama kimoja, ili kuwatendea haki Watanzania, tunaendelea kumuomba kwa unyenyekevu Rais wetu Samia Suluhu Hassan, aendelee kuliishi jina lake kwa kuleta suluhu ya kweli ya mtanziko wa siasa zetu, kwa kupokea maoni ya wengi, wanaomkubali kwa makubwa na mazuri anayoyafanya, lakini maoni ya wachache wanaotaka tufanye kwanza mabadiliko madogo ya katiba, minimum reforms, pia wasikilizwe ili tufanye mabadiliko ya Sheria ziwe ni sheria za haki kwa wote, wengi wape, wachache pia wasikilizwe.

Mungu Mbariki Rais Samia Aweze.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Naunga mkono hoja
 
Mimi bado najifunza Katiba mpya ya Kenya

Naona Ruto anaipondaponda Mahakama kana Kwamba si Muhimili wa Dola
Kenya ni Kenya na Tanzania ni Tanzania, Wakenya ni Wakenya na Watanzania ni Watanzania.

Kwa wenzetu Kiti cha Jaji Mkuu kikiwa wazi, nafasi inatangazwa, wenye sifa wanaomba, huku CJ, anateuliwa, hivyo unategemea mteuliwa wa hisani, anaweza kusimama wima bila ku bow down kwa mteuzi?. Kenya anaweza!.
P
 
Ta
Muda hautoshi, white paper inahitaji ushirikishwaji wa wadau , kwa walau mwaka mzima.

Tuendelee kutoa elimu kwa wadau kwanza waelewe, hasa wananchi, chadema wao wanapigania madaraka na vyeo tu, hawana ajenda za wananchi
Tangu 1977 Hadi sasa, ni miaka 47,

Muda wote huo haijawahi tosha?

Bila Tume huru ya Uchaguzi na KATIBA mpya, HAPATAFANYIKA UCHAGUZI WOWOTE WA HAKI.

Karibu maandamano ya Amani ya tarehe 24 January.
 
Mkuu ruhi Hiki ulichokisema ni kitu muhimu sana, hatuna kabisa political researchers kabisa hapa Bongo!.

Ile 2010, Tanzania tulikuwa watu milioni 50, wamejiandikisha kupiga kura watu milioni 20, waliojitokeza ni watu milioni 8!, JK akachaguliwa kwa kura milioni 5!, ambayo ni just 10% ya 50 milioni people!.
Hakuna yeyote anayejiuliza!.
P
Kabisa
 
mbowe alikuwa anagombana na viongozi waliochini yake, wengine wakimkosoa na madhiriano yake, ila leo ukiona hadi mbowe kakubali kuwa meza haileti matokeo, basi ni wazi ccm haina nia ya kubadili chochote, inataka kutawala milele kwa mgongo wa old and retired constitition.
kwahyo kupiga magoti na kumuomba "mama" asaidie ni uwongo maana naye pia ni mnufaika.
 
Kenya ni Kenya na Tanzania ni Tanzania, Wakenya ni Wakenya na Watanzania ni Watanzania.

Kwa wenzetu Kiti cha Jaji Mkuu kikiwa wazi, nafasi inatangazwa, wenye sifa wanaomba, huku CJ, anateuliwa, hivyo unategemea mteuliwa wa hisani, anaweza kusimama wima bila ku bow down kwa mteuzi?. Kenya anaweza!.
P
Yule mama CJ wa Kenya ameomba kukaa Meza moja na Ruto wazungumze LAKINI wananchi wamemgomea wakidai anavunja Katiba

Mambo yanachanganya Sana!
 
Yule mama CJ wa Kenya ameomba kukaa Meza moja na Ruto wazungumze LAKINI wananchi wamemgomea wakidai anavunja Katiba

Mambo yanacganganya Sana!
Angalau inaonyesha Strong institutions zinavyoweza kukubaliana au kutokukubaliana hadharani kwa mujibu wa Katiba inavyotaka !!

Na Wananchi wanapata nguvu ya kupaza sauti zao !
 
Back
Top Bottom