Ombi la Rais kuhusu Fei Toto kwa Yanga ni agizo lakini lisivunje kanuni za FIFA

Tufanye assumption wewe ndio Hersi, na umeshashiba pilau la Ikulu, Kataa ombi la raisi kwa kujaza sehemu iliyo wazi.

RAISI WA JMT: Naomba suala la Fei mlimalize.

Hersi:______________________
 
Linavunjaje kanuni za fifa? Yanga ndo mshika mkataba, sio fifa, akiamua kuachilia, hakuna shida.

Ni sawa na wewe ununue eneo utapeliwe, uamue kusamehe usiende mahakamani, hakuna sheria ta nchi imevunjwa
Huwezi kumwachia daudi aende halafu kumzuia masoud asiende kwa kosa au ombi kama lilelile la daudi. Huu ni wakati wa kutoa elimu hata kwa Rais wetu nae ajue namna suala Fei Toto linavyokuwa gumu kulitatua kwa wepesi kama anavyoomba.
 
Huwezi kumwachia daudi aende halafu kumzuia masoud asiende kwa kosa au ombi kama lilelile la daudi. Huu ni wakati wa kutoa elimu hata kwa Rais wetu nae ajue namna suala Fei Toto linavyokuwa gumu kulitatua kwa wepesi kama anavyoomba.
Andaeni press ya kumsahiiisha Rais kuwa alikosea alichosema na sheria za FIFA aziingiliani na serikali...nipo apa apa JF nasubiria mrejesho[emoji16][emoji16]
 
Hata Rais wetu afahamishwe kuhusu utaratibu wa timu kumpata mchezaji mwenye mkataba, labda Kuna watu wamempotosha. Fei Toto akitoka Yanga haendi kuvua samaki baharini bali Kuna timu itamsajili na kucheza mpira. Hiyo "timu" inatakiwa ijitokeze hadharani Sasa ili iuziwe mchezaji mzuri Fei Toto ambae bado Yuko kwenye mkataba na Yanga. Ikumbukwe kuwa Yanga imemuongezea thamani Fei Toto ndio maana hata timu nyingine inamtaka. Wachezaji ni bidhaa kama bidhaa nyingine kwenye tasnia ya mpira.
 
Chagueni kati ya kupewa eneo la kuongezea kujenga uwanja jangwani au mwacheni fei aende zake msimbazi.
Kwa mustakabali wa Yanga, mpira na uongozi ulioko madarakani ni heri kulikosa eneo kuliko kuivuruga Yanga kwa kuweka presidency ya hovyo itakayoivuruga klabu. Ni heri Hersi ajiuzulu kuliko kuivuruga timu.
 
Hata Rais hakuagiza Yanga imwachie Fei Toto aondoke kiholela kwenda Azam au Simba bwerere. Kuna maagizo lazima atampa Fei Toto pia. Kwakuwa Rais wetu anafahamu mambo mengi sana. Inawezekana anamjua hata yule aliyempa Fei sh.100,000,000 za kununulia mkataba wake Yanga.
 
Kwa hiyo assuarance aliyowapa we unadhani watamkatalia hiyo simple request(order).Mbona unakuwa mjinga kiasi hiki,kwani una umri gani.
kwani ukiitwa hasani lazima uwe mpumbavu kiasi hiki et?
 
Muwe Mnasikiliza vizuri.

Rais ALISEMA NYIE mmeniomba na Mimi niwaonbe jambo Moja.

KLABU kubwa kama yanga kuwa na migogoro na wachezaji haipendezo.
Akaomba wamalizane na Toto.

Rais AMETOA Ombi.
Kutoa ombi si AMRI.

HAJA VUNJA KANUNI YOYOTE ILE.
Hakuna ombi pale. Ni lugha rahisi yenye amri ndio maana kaomba apewe mrejesho. Sijuona sababu ya raisi kuingilia hili suala
 
Ni njia rahisi tu ambayo Fei Toto anatakiwa aifate ili aachiwe huru aondoke, nayo ni kwenda yanga kutajiwa thamani yake ambayo kwa upembuzi wa haraka haraka si chini ya milioni 350, alipe aondoke kiroho safi vinginevyo hakuna huruma itakayomuokoa.

Sheria, kanuni na miongozo ya FIFA na CAF iko wazi na sio suala la kihisia au huruma ya mtu!

Eng. Hersi shikilia hapo hapo dawa ya kiburi ni jeuri!
 
ngoja tuone
 
Ukute unakaa kwa Shemeji yako muda huu unasubiria Dada wa kazi akuite unywe chai
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…