Wakuu habari za jioni poleni kwa kutafuta na mihangaiko ya kutwa nzima. Mimi sina mengi ila nina imani humu kuna watumishi wa tume ya uchaguzi basi wafikishe salamu hizi, tunaomba mdahalo wa wagombea wote watakaoteuliwa kugombe Urais kuanzia, CCM, CHADEMA , ACT - Wazalendo nk ili tuwapime kwa hoja zao tuulize maswali yetu wakiwa pamoja kwenye ukumbi mmoja tupate mgombea ambaye ni cream ili wanachi tuchague Rais makini ambaye atatavusha kwenye umaskini tulionao na kuweka sera zinazotekelezeka kwa weledi na maarifa yaliyotukuka.
Nawasilisha.
View attachment 1527961
View attachment 1527962
View attachment 1527963