Hata wewe uliyoyaongea kuhusu lissu ndio atakyosema ni mawazo yako pia.
Mkuu tambua fedha nyingi sana ya kodi inapotea kizembe,ebu fikiria ile katiba ya warioba ilivyosema ,ilipendekeza baadhi ya vyeo vifutwe maana havina tija yoyote zaidi ya fadhila kwa wana ccm.
Ebu fikiria fedha tunazotumia kununua VX za milioni 300 kwaRC,DC,DEC,RAS na watu wanaofanana na hao ni Tsh Bilioni ngapi? Fikiria Maintanance zake na mafuta kwa mwaka ni mabilioni mangapi? Fedha zipo nyingi sana zinapotea kizembe ,ebu fikiria mkuu wa wilaya,mkoa unaenda kumpangishia nyumba masakai wakati analipwa mshahara huo si utapakanaji wa fedha za umma?
Nenda zanzibar viongozi wake wako simple tu ,jioni unawakatu wanapiga kahawa na wananchi na makazi yake ni ya kitaani tu kawaida,makatibu wa wizara ,mawaziri wapo simple tu hawana complication kama wabara ,cha kushangaza eti DC unampa Kilimo kwanza la milioni 300 halafu unampa nyumba ,unampa mshahara mil6 kwa faida gani anayoiingizia taifa?
Kichuguu fedha TZ ipo nyingi sana sema tunaitapakanya tu,kodi itapunguzwa na mishahara itaongezeka kama kawaida tu.