Uchaguzi 2020 Ombi: Tume ya Uchaguzi tunataka mdahalo wa Wagombea Urais

Uchaguzi 2020 Ombi: Tume ya Uchaguzi tunataka mdahalo wa Wagombea Urais

Mwaka 2010 na 2015 kulikuwa na midahalo mingapi? Halafu kukiwa na mdahalao huo, nina wasiwasi Lissu ataumia sana kwa sababu yeye atakwenda kuzungumza kwa hasira dhidi ya Magufuli ambaye amekuwa anamshmabulia kwenye vyombo vya habari vya nje kwa muda mrefu sasa.

Statement zake nyingi huwa ni za kuropoka na wakati mwingi huwa hazina ushahidi. Magufuli atakwenda pale akiwa na takwimu zote kichwani pamoja na vifungu vya sheria vinavyotawala maamuzi yote aliyowahi kufanya halafu na kusisitiza kwa uchungu kuwa hiyo ni kwa ajili ya watanzania maskini wa kawaida, maneno ambayo yanaweza kuwa na effect sana kwa wapiga kura kuliko maneno ya kinadharaia ya kwamba et i"nitajenga demokrasia ya kweli" au kuuliza kwa "nini kamera zilizimwa"

Wakati mwingine kuwa makini na lile uliombalo. Anayeweza kujenga mdahalo mzuri labda ni Mbowe tu; hata Zitto pia huwa hawezi.
Lissu vs JPM

Kwenye mdahalo kumbuka JPM hataweza ku-controll naratives zote. Na Lissu ataweka ushahidi wa madhaifu ya utawala wa JPM. Mfano rahisi ni yeye kupigwa risasi na hakuna aliekamatwa. Huo ni udhaifu mkubwa wa serikali.

Bado mengine mengi, JPM atakimbia mdahalo.
 
..Jpm kumbukumbu zake siku hizo siyo sharp kama wakati alipokuwa waziri.

..pia Jpm anajua sheria mbili tu, sheria ya ardhi, na sheria ya barabara.

..zaidi, Jpm amezoea kuzungumza peke yake, hajazoea na hapendi kuwa challenged.
JPM anaongoza kwa propaganda.

Lissu anaweza kuibua ishu za ufisadi tu kwenye utawala wa awamu ya tano Magufuli akazimia.

Mdahalo wowote ni mgumu kwa CCM.
 
Wakuu habari za jioni poleni kwa kutafuta na mihangaiko ya kutwa nzima. Mimi sina mengi ila nina imani humu kuna watumishi wa tume ya uchaguzi basi wafikishe salamu hizi, tunaomba mdahalo wa wagombea wote watakaoteuliwa kugombe Urais kuanzia, CCM, CHADEMA , ACT - Wazalendo nk ili tuwapime kwa hoja zao tuulize maswali yetu wakiwa pamoja kwenye ukumbi mmoja tupate mgombea ambaye ni cream ili wanachi tuchague Rais makini ambaye atatavusha kwenye umaskini tulionao na kuweka sera zinazotekelezeka kwa weledi na maarifa yaliyotukuka.

Nawasilisha.

View attachment 1527961

View attachment 1527962

View attachment 1527963
Sijui tundulisu ataweza kutueleza miga na ushoga alimaanisha nn
 
JPM anaongoza kwa propaganda.

Lissu anaweza kuibua ishu za ufisadi tu kwenye utawala wa awamu ya tano Magufuli akazimia.

Mdahalo wowote ni mgumu kwa CCM.

..pia kwenye mdahalo Jpm hatakuwa na wapambe wa kum-keep company.

..Kabudi hatakuwepo hapo ili kusherehesha tukio zima.

..Hakutakuwa na viongozi wa dini watakaompamba kuwa yeye ni chaguo la mungu.

..kitakachombeba ni PROPAGANDA baada ya tukio zima.
 
Tunazungumzia mdahalo boss sio ilani...
Upinzani ilani yenu ya uchaguzi imetoka?

Bring forward your election manifesto.

CCM inayo tayari ilani yake ya uchaguzi.

Waleteeni wananchi waichambue ilani yenu ya uchaguzi.

Acheni blahblah zisizo na tija.
 
Ushauri mzuri NEC wasikie.
Katika hilo jengo la mdahalo hakikisheni nje Kuna ambulance, just in case mmoja anaanguka ghafla. Si mnafahamu wagombea wetu ni 60+ na yule ambae ni under 60 ana vyuma mwili mzima.
 
Safi sana umenena vyema
Kwanini kusiwepo na mdahalo wa saa 8 kwa wagombea wote wa kiti cha uraisi maana najua JPM anavitu vya kuongelea ndani ya miaka yake mitano kama Raisi, na wengine watasema wanataka kuchaguliwa ili iweje?.
 
Basi kama ni hivyo akubali haraka sana mdahalo ili kazi iwe nyepesi jombaa
Mwaka 2010 na 2015 kulikuwa na midahalo mingapi? Halafu kukiwa na mdahalao huo, nina wasiwasi Lissu ataumia sana kwa sababu yeye atakwenda kuzungumza kwa hasira dhidi ya Magufuli ambaye amekuwa anamshmabulia kwenye vyombo vya habari vya nje kwa muda mrefu sasa.

Statement zake nyingi huwa ni za kuropoka na wakati mwingi huwa hazina ushahidi. Magufuli atakwenda pale akiwa na takwimu zote kichwani pamoja na vifungu vya sheria vinavyotawala maamuzi yote aliyowahi kufanya halafu na kusisitiza kwa uchungu kuwa hiyo ni kwa ajili ya watanzania maskini wa kawaida, maneno ambayo yanaweza kuwa na effect sana kwa wapiga kura kuliko maneno ya kinadharaia ya kwamba et i"nitajenga demokrasia ya kweli" au kuuliza kwa "nini kamera zilizimwa"

Wakati mwingine kuwa makini na lile uliombalo. Anayeweza kujenga mdahalo mzuri labda ni Mbowe tu; hata Zitto pia huwa hawezi.
 
Vizuri kabisa...ni wazo zuri saana.

Mdahalo uwepo na wagombea watuambie wanaenda kutufanyia nini.
 
Una uhakika na unachokisema..?
1. Hamna haja wala umuhimuwa mdjadala, kwakua hamna la kujadili, Rais Mgufuli aliyoyafanya katik utawala wake yanaonekana na kila mtu, wala haitaji kushawishi umma juuya ubora wa uongozi wake.

2. Rais Magufuli anaweza asiwe muongeaji mzuri, na pia anaweza asiwe mwanasiasa bora, lakini ameonesha kwamba yeye ni kiongozi bora sana. Tanzania inahitaji kiongozi bora, na wala hatuhitaji mwanasiasa bora. JPM ni mtekelezaji kwa vitendo, mara nyingi wale ambao wameonekana kuwa ni waongeaji sana wamekua wakifeli kwenye utendaji.

3. Uchaguzi huu ni mwepesi sana, JPM atashinda kwa kura nyingi sana, tena mapema sana.
 
Nashukuru kwa kutambua kuwa mijadali ya hapa nimeshapitia mingi, ingawa conclusion yako haina basis yoyote. Uliyoongea hapo ni mawazo yako lakini hatujamsikia Lissu akiyasema na wala hatujaona Ilani ya CHADEMA ikiyasema, halafu yote bado ni yamekaa kinadharia tu. Huwezi kusema utapunguza kodi halafu eti utaongza misharara na kutoa huduma za bure; hiyo ni nadharia tupu. Mishahara na huduma zote za bure hutokana na kodi.

Huo ni Uchumi wa Steven Moore tu

Hata wewe uliyoyaongea kuhusu lissu ndio atakyosema ni mawazo yako pia.

Mkuu tambua fedha nyingi sana ya kodi inapotea kizembe,ebu fikiria ile katiba ya warioba ilivyosema ,ilipendekeza baadhi ya vyeo vifutwe maana havina tija yoyote zaidi ya fadhila kwa wana ccm.

Ebu fikiria fedha tunazotumia kununua VX za milioni 300 kwaRC,DC,DEC,RAS na watu wanaofanana na hao ni Tsh Bilioni ngapi? Fikiria Maintanance zake na mafuta kwa mwaka ni mabilioni mangapi? Fedha zipo nyingi sana zinapotea kizembe ,ebu fikiria mkuu wa wilaya,mkoa unaenda kumpangishia nyumba masakai wakati analipwa mshahara huo si utapakanaji wa fedha za umma?

Nenda zanzibar viongozi wake wako simple tu ,jioni unawakatu wanapiga kahawa na wananchi na makazi yake ni ya kitaani tu kawaida,makatibu wa wizara ,mawaziri wapo simple tu hawana complication kama wabara ,cha kushangaza eti DC unampa Kilimo kwanza la milioni 300 halafu unampa nyumba ,unampa mshahara mil6 kwa faida gani anayoiingizia taifa?

Kichuguu fedha TZ ipo nyingi sana sema tunaitapakanya tu,kodi itapunguzwa na mishahara itaongezeka kama kawaida tu.
 
..nadhani unacho-suggest ni kwamba Jpm should prepare like those who CRAM for the exams.

..Mara nyingi watu wa aina hiyo huwa wanachemka wakikutana na situation ambayo hawakuitarajia.

..disadvantage nyingine ni kwamba Jpm anapenda yeye ndiyo awe bosi wakati wote kwa hiyo upo uwezekano wa kutomheshimu moderator.

Kama ulikuwa unajiandaa mitihani kwa kukarii inawezekana hujui nmaana ya kujiandaa. maandalizi maana yake ni kupanga facts zako right. Hata wanasheria humuomba hakimu muda kuwa wanata wajiandae siyo kuwa wanataka kukariri mambo. Mwaka 1995 nyerere akihutubia waandishi pale kilimanjaro hotel aliwaambia kuwa ingawa ana facts nyingine anazotaka kuziongelea lakini alikuwa hakuziandaa vizuri, hivyo akawaambia atayaongelea mambo hayo siku nyingine; siyo kuwa alikuwa anataka kukariri. hata mwalimu anapota kufundisha huwa anajiandaa hata kama alishafundisha mambo hayo kwa miaka 20 bado atajiandaa. kujiandaa siyo kukariri
 
Lissu vs JPM

Kwenye mdahalo kumbuka JPM hataweza ku-controll naratives zote. Na Lissu ataweka ushahidi wa madhaifu ya utawala wa JPM. Mfano rahisi ni yeye kupigwa risasi na hakuna aliekamatwa. Huo ni udhaifu mkubwa wa serikali.

Bado mengine mengi, JPM atakimbia mdahalo.
wewe unachukulia kuwa mjadala maana yake ni kubishana na kushambuliana personally, jambo ambalo lissu anajua sana. mimi naangalia mjadala kua ni uwanja kupambanishana sera na vision ya taif. ukiingia kwene mjadala na ajenda ya chuki, nin wasiwasi kama utakusaidia kupata hata kura moja zaidi zile za base kama wewe
 
Back
Top Bottom