Ommy Dimpoz ajibu kuhusu tuhuma za yeye kuitwa Chakula (Shoga) na Dudu Baya

Ommy Dimpoz ajibu kuhusu tuhuma za yeye kuitwa Chakula (Shoga) na Dudu Baya

Mwanamuziki maarufu nchini Tanzania, Ommy Dimpoz, amejibu rasmi tuhuma na maneno ya kashfa yaliyotolewa dhidi yake na msanii mwenzake Godfrey Tumaini, maarufu kama Dudu Baya, aliyemwita "chakula" (mshoga).

Ommy Dimpoz ameeleza kuwa hana mpango wa kuchukua hatua yoyote ya kisheria au ya kulipiza kisasi, badala yake amechagua kumwachia Mungu na kumsamehe.

Kauli hiyo imekuja kupitia mahojiano maalum ambapo Ommy Dimpoz alifunguka kuhusu namna anavyokabiliana na kashfa hizo zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii. Akifafanua mtazamo wake, msanii huyo alieleza kuwa jamii mara nyingi imekuwa ikiwazingizia watu mambo yasiyo ya kweli, kama vile kuwaita wizi au malaya na wahusika kushindwa kujitakasa, hivyo kuamua kuendelea na maisha yao.

Ommy Dimpoz alibainisha kuwa anamchukulia Dudu Baya kama kaka yake mkubwa na mmoja wa wasanii waliomshawishi kuingia kwenye tasnia ya muziki. Hata hivyo, alieleza kuwa Dudu Baya amechagua njia ya kutafuta umaarufu kwa kuwasengenya na kuwazungumzia wengine vibaya mtandaoni.

"Mimi sina cha kumfanya Dudu Baya kwa sababu anayenijua mimi kiundani ni Mungu tu. Yeye amechagua hayo maisha ya kuzungumzia watu kwa ubaya ili aweze kutrend," alisema Ommy Dimpoz, akiongeza kuwa anamwombea Msamaha kwa Mungu na ataendelea kuangazia maisha na kazi zake za muziki bila kuingizwa kwenye migogoro.
View attachment 3674413
Jamaa amejiweka karibu na wale jamaa wa Yanga,ambao wanasemwa sana kuwabandua vijana wenye tamaa.
 
Ommy kagoma kulipa kiki saafii kabisa..!!

Ni muda sasa apumzishwe kwenye hizo show za Chaka 2 Chaka akaendelee kunywa visungura na vinyuki huko vilabuni..!!
 
Hayo mambo yameanza kuongelewa muda Ina maana muda wote huo hakuna mtu aliyewahi kumgonga kweli? Si watu wangeshapata info na kuweka hadharani? Mm naona hizi habar ni uzushi tu sema Dimpoz ni mtanashati aliyepitiliza ndio maana
 
Yaani niitwe ***** wakati sio halafu nimwachie Mungu?? Haipo hiyo, huyo dudubaya siju dudubwege angenitangaza hadharani alinichokoa lini na wapi, vinginevyo mimi ndio ningemchokoa yeye kwa mbinu yoyote na kumtangaza hadharani. Kuna tuhuma za kumezea ila sio za kuchokolewa, HUYO DIMPOZ ATAKUWA ***** KWELI NDIO MANA AMEAMUA KUMWACHIA MUNGU WAKATI HII ISHU NI YA KISHETANI
Zipo njia 1001 za kuwashughulikia watu jamii ya dudubaya,unaweza dhania game imekwisha kumbe inapelekwa chini chini kimya kimya atatukana watu mpaka lini.
 
Amejibu vizuri.
Hata kama angefungua kesi Dudubaya asingekutwa na hatia sababu alitumia neno "Dimpoz ni chakula"
Hapo Sasa. Ila huyo dudubaya ana matatizo ya akili kabisa kabisa, kwenda kumshambulia mwenzako kwa maneno kama yale lazima tukuone umechanganyikiwa!
 
Hao waandaaji wanaomuweka dudubaya kwenye shoo ifike pahala wamuweke kando!
Mambaz 24 akiwekwa kando mashoga watakuwa wameshinda hii vita, kama wauza madawa walivyomshinda Amina Chifupa.

Haiwezekani watu mkereke pale Dudubaya anapokemea ushoga, na kuwataja mashoga hadharani, ambao sio ninyi. Kitu cha ovyo ni lazima kikemewe, na hakunaga maonyo yanayotolewa kwa kubembeleza.
 
Mambaz 24 akiwekwa kando mashoga watakuwa wameshinda hii vita, kama wauza madawa walivyomshinda Amina Chifupa.

Haiwezekani watu mkereke pale Dudubaya anapokemea ushoga, na kuwataja mashoga hadharani, ambao sio ninyi. Kitu cha ovyo ni lazima kikemewe, na hakunaga maonyo yanayotolewa kwa kubembeleza.
Ccm wakimuonya Mwanchama wao huwa wanasema " Tunampa Onyo Kali"

Kumbe Onyo lazima liwe Kali?
 
Jibu lilikuwa ni moja tu🤣🤣
Maelezo meengi
Na anasema kuwa Dudubaya ameamua kusema watu ili atrend, imekuaje amefikia conclusion kuwa Mambaz anataka trending? Hiyo si ni kauli ya kutaka kudogosha harakati. Mambaz 24 komaa nao hao mashoga. Kalapina nae anaendelea na harakati za kukemea machoko, ameanza na Suma Mnazaleti
 
Na anasema kuwa Dudubaya ameamua kusema watu ili atrend, imekuaje amefikia conclusion kuwa Mambaz anataka trending? Hiyo si ni kauli ya kutaka kudogosha harakati. Mambaz 24 komaa nao hao mashoga. Kalapina nae anaendelea na harakati za kukemea machoko, ameanza na Suma Mnazaleti
Hiyo vita hawezi kushinda, mshaurini huyo Ambazo wenu aachane nayo.

Yesu mwenyewe ilimshinda,
Aliikuta akaiacha.

Huyo mnayemwita Mungu alichoma sodoma na gomora ili amalize kizazi kichafu lakini ilimshinda na sijui hii specie nyingine ilitoka wapi tena
 
Back
Top Bottom