Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Wale wasio na uelewa mpana wa mwenendo wa vita wanapima mafanikio ya vita kwa kuwa na ndege nyingi za kijeshi na vifaru na kupiga mabomu mazito kwa mfululizo.
Wanapima pia kwa vikosi vya jeshi fulani kuweza kuingia mpaka ndani ya ngome ya mpinzani kwa muda.
Vitu vinavyotakiwa kupimwa ni zaidi na vingi kuliko hivyo.Miongoni mwao ni jee baada ya kuingia utawezaje kuendelea kubaki hapo na jee utaweza kutoka kwa muda mfupi au mrefu kama utakavyopenda?
Kwa upande wa vita vinavyoendelea sasa baina ya Israel na wapalestina chini ya Hamas huko Gaza kuna ishara nyingi za kuonesha kushindwa kwa Israel na kwamba itaendelea kushindwa kadri siku zinavyokwenda.
Kushindwa kwa mwanzo ni kule kutokufanikiwa kuwanyamazisha Hamas zaidi ya mwezi na kutokujua sehemu wanapoendesha vita,na pia kushindwa kuokoa mateka hata mmoja.Dalili ni kuwa hata wakiwaokoa haitowezekana kuwapata idadi ya kuwaridhisha wanacnhi wanaowasubiri huko majumbani mwao.
Sehemu nyengine ya dalili za kushindwa mbeleni ni kwamba tayari Israel wameweza kuropoka yale waliyokuwa wameyaficha nyoyoni mwao kwamba wanataka wawahamishe wapalestina wote kutoka Gaza na walifikiria kuwapeleka uhamishoni Sinai ndani ya Misri.Hili lilijulikana mapema na kupingwa mapema pia na Misri na wenzake.
Baada ya kuwataka watu wakimbilie kusini kutoka kaskazini ya Gaza viongozi wa kijeshi walisikika wakisema tukimaliza kaskazini tunakuja na kusini.Na kwa papara zao hata haawkusubiri kumaliza huko kaskazini wamekuwa wakipiga kusini na kusababisha maafa takriban nusu ya yale yanayotokea kaskazini.
Kama kweli watafanikiwa kumaliza kaskazini itabidi waanze kupiga kwa nguvu kusini na maafa yataanz kushuhudiwa wazi wazi.
Ukatili utakaoendelea kusini hautokuwa na kisingizio kingine zaidi ya kuonekana ni unyama na nia ya kutaka kuwaangamiza wapalestina kwa faida zao.Wapalestina karika picha ya huruma na kutapatapa wakipigwa na hawawezi kwenda kaskazini wala kusini kutawainua wote wenye nyoyo za kibinadamu
Hapo dunia nzima isipokuwa wachache itasimama kivitendo kuwatetea wapalestina.
Wale waliokuwa wamejizuia miongoni mwa nzhi za kiarabu na kiislamu zitaanza kujitutumua kivitendo kuanza kupigana na Israel kila mmoja kwa atakapoweza.
Nchi za kiarabu na kiislamu zitakaposhindwa kufanya hivyo kivitendo kutazalisha fukuto na chuki miongoni mwa watu wake kuanzia raia wa kawaida mpaka vyombo vya ulinzi kunakoweza kuzalisha mapinduzi na kupatikana serilali zitakazoamua kupigana hadharani kijeshi na Israel wakati huo Israel na mshirika wake US wakiwa wako taabani na kukosa kuungwa mkono na raia zao katika kuendeleza vita
Mwisho wa yote itakuwa ni kusalimu amri kwa Israel na kupanda juu kwa wanamgambo mfano wa Hamas.