T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 12,362
- 41,886
Hicho kibastora kiunoni kinazuia mamluki kumdhuru?Nakujibu hoja ya bunduki, huyo aliyekutana nae sio mamluki ni mtu ambaye anamuhitaji wapige kazi, alihakikishiwa usalama wake,
Viongozi wa Africa wote ni vibaraka wa wazungu, hawakawii kukugeuka in a second, hii ipo tangu enzi za ukoloni ni viongozi wa wakati huo ndio waliowauza raia, kwa hiyo anahitaji kujilinda zaidi akiwa Nchini kwake na Africa kwa ujumla kuliko akiwa na mtu kama Putin ambaye sie adui wake,
Una lingine labda.......
Unadhani angejua kuna mamluki na usalama wake mdogo angeenda kisa tu ana kibastora kiunoni? Yani washindwe kutumia MANPADS kudungua ndege, au ATGM au RPG kupiga gari lake, waje karibu yake kumdhuru na walinzi wake washindwe mpaka yeye atumie kibastora chake kujiokoa. Hii ni maajabu.
In case anahitajika kufa, hiyo bastora haina msaada wowote. Wakati anafanya mapinduzi kumuondoa kiongozi wa kijeshi akiyekuwepo, nadhani ni Damiba silaha ya Damiba haikumsaidia kitu.