Orodha ya walioachwa Ukuu wa Wilaya

Orodha ya walioachwa Ukuu wa Wilaya

Ila hii nchi bana utaratibu wa kupata viongozi ni wa hovyo sana, kipindi flani nikiwa Mzumbe University- Morogoro tukaletewa mgeni rasmi mmoja hivi mdada ilikua ni siku ya 'ujasiriamali' pale chuoni. Mgeni rasmi alikua ni mkuu wa wilaya ya Mvomero ee bana yule mkuu wa wilaya sijui aliokotwa wapi akapachikwa kwenye hicho cheo. Uchangiaji wa kale kadem ilikua ni aibu kumsikiliza yani tangu siku hiyo sina imani na mwana ccm yeyote hata huyo mnamuita mama.
Mie nilichoka Kwa Juliana Shonza kuwa naibu waziri. Afrika jamani
 
Naona watu wanamsema sana Jerry Muro, mtashangaa anakuja kuukwaa ukuu wa mkoa . Nchi ngumu sana hii.
Kweli kabisa sitashangaa.
Jerry anajua sana siasa za maji taka na kwa ccm ni mtu muhimu sana kwa majira flani.

Imagine kipindi cha magu kampeni ngaramtoni aliyokuwa ametumwa pinda Jerry na sabaya walikuwa wamelewa chakariiii hadi wanayumba na hakukuwa na wakuwafanya kitu na wapo mbele kule
 
Tanzania ni ulafi tu na njaa ila nafasi za ukuu wa mkoa na nafasi za ukuu wa wilaya sijui wale jamaa wanazipendea nini kweli hata kama zina hela na marupu rupu lakini ni kazi za stress na lazima uwe mchawi kweli kweli tena kigwagula yaani mtu anaweza amka tu asubuh umeshatumbuliwa.

Sent from my SM-N950F using JamiiForums mobile app
Zinapendwa kwa kuwa sio kazi za kitaalamu. Wengi wetu kwa vile hatuna uwezo wa taaluma tulizonazo kudeliver, hiyo nafasi inatufaa sana kwa u "empty head" wetu.
 
Kama yapo naombeni Radhi na Kwao pia kwani huenda niliupitia tu Mkeka kwa haraka haraka.

Naomba kujua aliyekuwa DC wa Mwanga Abdallah Mwaipaya na aliyekuwa DC wa Ikungi Jerry Muro wamehamishiwa Wilaya gani?

Nitawashukuruni.
Mwaipaya kabaki Mwanga
 
Ukiona unasemwa saana jua hupendwi,kwa hili nimegundua muro ana maadui wengi mno kama ilivyokuwa kwa ali hapy,alipopigwa chini wengi sana walifurahi.
Nafikiri Jerry hapendwi na watu wengi sababu ya kuongea sana haswa alipokua Utopoloni, ni sawa na Haji Manara yeye anadhani watu wanampenda kumbe hawampendi haswaa.. Watu wengi wanafurahia kuanguka kwa watu wenye BIG MOUTH ......Sometimes Low key is better than publicity.
 
Back
Top Bottom