Orodha ya Watanzania maarufu waliokufa bila kujenga nyumba

Orodha ya Watanzania maarufu waliokufa bila kujenga nyumba

1. Dkt. Omar Alli Juma
Huyu alikuwa VP kipindi cha BWM, baada ya kufariki akiwa madarakani, familia yake ilitakiwa kupisha nyumba rasmi ya VP iliyopo nyuma ya St Peters Oysterbay ili Dkt. Shein VP mteuliwa aweze kuingia humo, wakawa hawana pa kuweka vyombo, hawana nyumba, ikabidi lori la erikali liwatoe kinguvu na kwenda kusitiriwa kwenye magofu ya Serikali


2. Gilman Rutihinda
Huyu alikuwa gavana wa BoT enzi za Mwinyi, tulimzika Buguruni Malapa maana kwao Ngara hakuwa na nyumba bali kijumba.


3.Brigedia Moses Nnauye
Huyu alikufa mwaka 2000 kama sikosei, ilibidi msiba tuupeleke kwa mzee Makamba maana tulikosa sehemu ya kufunga turubai kwenye zile flats za NHC, utafunga turubai kwenye flats?
Aliwahi kuwa brigedia jeshini,Naibu Waziri ulinzi,Mkuu wa wilaya Bagamoyo,mkuu w mkoa Singida,mhamasishaji wa CCM,Katibu mwenezi CCM,naibu katibu mkuu CCM Nk


4. Profesa Shaba
Huyu sijui yupo hai au, anasifika kuufanyia post mortam mwili wa hayati Sokoine, mpaka anastaafu na kumaliza kiinua mgongo hakuwahi kujenga hata choo. Alipostaafu aliigomea Serikali kuachia nyumba iliyokuwa mitaa ya Shaaban Robert karibu na Gymkhkana DSM.

Akiwatisha kuwa ataanika kilichomuua Sokoine if at all they try to vacate him, wakampotezea.


5. Steven Kanumba
Pamoja na kumiliki gari ya mamilioni kadhaa alikufa hajawahi kujenga hata kiosk

6. Ray Kigosi(yuko hai)
Bado anaishi kwa mama yake Sinza hajui hata mfuko wa cement inatoa tofali ngapi

7.

Itaendelea
Naona umemsagia kunguni Ray Kigosi hapo namba 6 😅😅😅
 
Makazi ya milele ni Mbinguni tutafute hela tukajenge huko, hapa duniani tunapita tu
 
Mbona kwenye list sijaona jina la kike?????
 
Jenga nyumba wewe acha porojo,yaani uwe na miradi yote hiyo alafu ushundwe nyumba ya 30 kijijini kwenu,basi utakuwa hujitambui
Mfano mimi Kijinini kwetu(wanakotoka wazazi) kulishajengwa sasa mimi nikajenge nini wakati sitarajii kuishi huko na hata nikifa sizikwi huko? Its all about mindset na belief za mtu, Kwangu Cashflow ni muhimu zaidi kuliko kumiliki nyumba alfu hela ya kula nategemea mikopo ya kwenye Vikoba.
Nitajenga nyumba kwa ajili ya Biashara i kuongeza my cashflow ila siyo kujenga nyumba tu bila kuwa na kipato endelevu.
 
Mfano mimi Kijinini kwetu(wanakotoka wazazi) kulishajengwa sasa mimi nikajenge nini wakati sitarajii kuishi huko na hata nikifa sizikwi huko? Its all about mindset na belief za mtu, Kwangu Cashflow ni muhimu zaidi kuliko kumiliki nyumba alfu hela ya kula nategemea mikopo ya kwenye Vikoba.
Nitajenga nyumba kwa ajili ya Biashara i kuongeza my cashflow ila siyo kujenga nyumba tu bila kuwa na kipato endelevu.
Unajuaje ukifariki hautozikwa sehemu fulani?
 
Upuuzi mtupu huu. Ukijenga nyumba au jumba siku ukifa unazikwa nalo kaburini???

Ndugu yangu, jitahidi sana ujenge mahusiano yako wewe na MUNGU kabla ya kufa. Hilo ni muhimu sana kujenga na siyo nyumba. Jenga roho yako iwe njema, weka hazina yako Mbinguni maana ilipo hazina yako, ndipo na roho yako itakapokuwa.
Sawa mtumishi.. Weka kapu la sadaka tuanze kutoa zaka na fungu la kumi sasa!!
 
Back
Top Bottom