Orodha ya Watanzania maarufu waliokufa bila kujenga nyumba

Hapo kwa Ray kigosi nimecheka Kama mazuri vile dah😂😂

Ray ana point asikilizwe🤣
1693762372351.jpg
 
Mkuu hapo kwa Prof. Shaba kama siyo kweli vile!
Kuna nyumba ya Prof. Shaba maeneo ya Golani ukitoka Ubungo Msewe unaelekea UDSM.
Labda aligoma kuhama sababu alitaka kuendelea kula upepo wa mjini karibu na bahari.
 
1. Dkt. Omar Alli Juma
Huyu alikuwa VP kipindi cha BWM, baada ya kufariki akiwa madarakani, familia yake ilitakiwa kupisha nyumba rasmi ya VP iliyopo nyuma ya St Peters Oysterbay ili Dkt. Shein VP mteuliwa aweze kuingia humo, wakawa hawana pa kuweka vyombo, hawana nyumba, ikabidi lori la erikali liwatoe kinguvu na kwenda kusitiriwa kwenye magofu ya Serikali

2. Gilman Rutihinda
Huyu alikuwa gavana wa BoT enzi za Mwinyi, tulimzika Buguruni Malapa maana kwao Ngara hakuwa na nyumba bali kijumba.

3.Brigedia Moses Nnauye
Huyu alikufa mwaka 2000 kama sikosei, ilibidi msiba tuupeleke kwa mzee Makamba maana tulikosa sehemu ya kufunga turubai kwenye zile flats za NHC, utafunga turubai kwenye flats?
Aliwahi kuwa brigedia jeshini,Naibu Waziri ulinzi,Mkuu wa wilaya Bagamoyo,mkuu w mkoa Singida,mhamasishaji wa CCM,Katibu mwenezi CCM,naibu katibu mkuu CCM Nk

4. Profesa Shaba
Huyu sijui yupo hai au, anasifika kuufanyia post mortam mwili wa hayati Sokoine, mpaka anastaafu na kumaliza kiinua mgongo hakuwahi kujenga hata choo. Alipostaafu aliigomea Serikali kuachia nyumba iliyokuwa mitaa ya Shaaban Robert karibu na Gymkhkana DSM.

Akiwatisha kuwa ataanika kilichomuua Sokoine if at all they try to vacate him, wakampotezea.

5. Steven Kanumba
Pamoja na kumiliki gari ya mamilioni kadhaa alikufa hajawahi kujenga hata kiosk

6. Ray Kigosi(yuko hai)
Bado anaishi kwa mama yake Sinza hajui hata mfuko wa cement inatoa tofali ngapi

7.

Itaendelea
Kwa Kanumba,sio kweli alikuwa anamalizia kujenga nyumba yake huko Mbezi
 
Apr 18, 2012​

Utajiri wa Steven Kanumba​

  • Ni magari matatu, viwanja kadhaa
  • Mazishi yagharinu mil.52/-
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongea na mwenyekiti
wa kamati ya mazishi Gabriel Mtitu
Moja ya gari tatu zilizoachwa na marehemu Kanumba

Kamati Kuu ya Mazishi ya aliyekuwa msanii mashuhuri wa filamu nchini, marehemu Steven Kanumba, imedai msanii huyo amefariki dunia akiwa maskini, kinyume kabisa cha umaarufu mkubwa aliokuwa nao wakati wa uhai wake.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mtitu Gabriel, alisema hayo wakati akitoa ufafanuzi kuhusu makusanyo na matumizi ya fedha zilizotumika katika maombolezo, kuaga na mazishi ya Kanumba, aliyefariki dunia Aprili 7, mwaka huu na kuzikwa Aprili 10, mwaka huu.
Mbali na Mtitu kutoa ufafanuzi kuhusiana na fedha zilizokusanywa pamoja na matumizi yake, alikanusha taarifa za uvumi kuwa msanii huyo ameacha mali zenye thamani ya Sh. milioni 700.
“Hizi taarifa hazina ukweli ndani yake, ninachojua Kanumba amefariki akiwa na jina kubwa katika sanaa, lakini ni mtu mwenye pesa ya kawaida,” alisema Mtitu. Alisema kinachozungumzwa na watu hakina ukweli.
Mjumbe wa Kamati hiyo, William Mtitu, alisema mali zilizoachwa na marehemu Kanumba ni magari matatu na, viwanja ambavyo hata hivyo, hakutaja idadi yake wala mahali viliko. Kuhusu nyumba aliyokuwa akiishi eneo la Sinza, alisema kuwa ilikuwa ni ya kupanga.
Pia alisema alikuwa akimiliki kampuni inayohusika na uandaaji na utayarishaji wa filamu ijulikanayo kwa jina la “Kanumba The Great” jijini Dar es Salaam.
Kampuni hiyo ambayo inamiliki studio, inaelezwa ina mchango mkubwa wa kuinua vipaji vya wasanii chipukizi, akiwamo Wema Sepetu na Elizabeth Michael, maarufu kama ‘Lulu’.
Hata hivyo, alikataa kueleza kiasi cha fedha alizoacha Kanumba na akaunti zake za benki kwa maelezo kwamba suala hilo ni la familia.
Awali, Gabriel Mtitu alisema wao kama kamati, walipokutana siku ya msiba wa nyota huyo wa filamu, kulikuwa hakuna kianzio chochote cha kufanikisha msiba.
Badala yake, alisema walifanya bidii ya kukusanya fedha ambazo zilitumika wakati wa msiba.
Mtitu alitaja makusanyo ya michango pamoja na matumizi ya fedha zilizotumika katika maombolezo hadi mazishi ya msanii huyo.
Alisema makusanyo ya michango yote ilikuwa ni Sh. 53,252,000 na kwamba, kati ya fedha hizo, zilizotumika ni Sh. 52,102,000.
Mtitu alisema fedha zilizotolewa ahadi ni Sh. 15,500,000, wakati ahadi ya vifaa ilikuwa ni Sh. 18,400,000. Alisema ahadi zilizolipwa ni Sh. 2,850,000.
Mtitu alisema gharama zote za maombolezo hadi mazishi zikiwemo taslimu na ahadi ni Sh. 70,502,000.
“Salio ni Sh. 4,000,000 ambazo zimekabidhiwa na zitaendelea kukabidhiwa kwa mama wa marehemu kadri ya marejesho ya ahadi yatakavyokuwa,” alisema Mtitu.
Alisema wao kama kamati wamekamilisha rasmi shughuli za msiba huo, na kuiachia familia iendelee na taratibu nyingine.
Mtitu alisema ili kuhakikisha wanamuenzi marehemu Kanumba, wanatarajia kuanzisha tuzo ya Steven ambayo itatoa changamoto kwa wasanii kuiga mfano wa utendaji wake wa kazi.
“Tuna mikakati ya kuanzisha tuzo ya Steven ambayo itatoa changamoto kwa wasanii kujituma ili waweze kufikia kiwango alichofikia katika uigizaji wake,” alisema Mtitu.
Akizungumzia malalamiko ya baadhi ya watu kutopewa nafasi ya kuuaga mwili wa marehemu, alisema ilishindikana kutokana na matarajio ya watu waliofika katika mazishi yake yalikuwa kinyume cha makadirio yao.
“Hatukutarajia idadi kubwa ya waombolezaji kujitokeza kiasi kile. Baada ya viongozi wa serikali kuondoka, kulitokea msongomano uliopelekea kamati kuzuiwa watu kuaga,” alisema Mtitu.
 
Mkuu hapo kwa Prof. Shaba kama siyo kweli vile!
Kuna nyumba ya Prof. Shaba maeneo ya Golani ukitoka Ubungo Msewe unaelekea UDSM.
Labda aligoma kuhama sababu alitaka kuendelea kula upepo wa mjini karibu na bahari.
Kuna shaba watatu maarufu,mmoja ni huyu anayeongelewa,mlevi na frustrated,Kuna mwingine alikuwa mke wa jenerali ulimwengu,then kuna mwingine alukuwa udsm
Huyu anayeongelewa hajawahi kujenga hata banda la kuku
 
ishiii.! kumbe baba nape hakuwa na nyumba ni kweli?
Baba Nape na JK wamekula sana bata enzi za ujana wao🤣Jk angekata moto mwaka 95 angekuwa hajaacha nyumba zaidi ya ile ya bagamoyo
 
Mkuu hapo kwa Prof. Shaba kama siyo kweli vile!
Kuna nyumba ya Prof. Shaba maeneo ya Golani ukitoka Ubungo Msewe unaelekea UDSM.
Labda aligoma kuhama sababu alitaka kuendelea kula upepo wa mjini karibu na bahari.
Huyu prof watoto wake wako USA kitambo,itakuwa walimjengea ,maana wana aoartments nyingi sana hapa mjini,watoto wamesoma wana akili na hella ni maarufu sana kule Illinois USA
 
1. Dkt. Omar Alli Juma
Huyu alikuwa VP kipindi cha BWM, baada ya kufariki akiwa madarakani, familia yake ilitakiwa kupisha nyumba rasmi ya VP iliyopo nyuma ya St Peters Oysterbay ili Dkt. Shein VP mteuliwa aweze kuingia humo, wakawa hawana pa kuweka vyombo, hawana nyumba, ikabidi lori la erikali liwatoe kinguvu na kwenda kusitiriwa kwenye magofu ya Serikali

2. Gilman Rutihinda
Huyu alikuwa gavana wa BoT enzi za Mwinyi, tulimzika Buguruni Malapa maana kwao Ngara hakuwa na nyumba bali kijumba.

3.Brigedia Moses Nnauye
Huyu alikufa mwaka 2000 kama sikosei, ilibidi msiba tuupeleke kwa mzee Makamba maana tulikosa sehemu ya kufunga turubai kwenye zile flats za NHC, utafunga turubai kwenye flats?
Aliwahi kuwa brigedia jeshini,Naibu Waziri ulinzi,Mkuu wa wilaya Bagamoyo,mkuu w mkoa Singida,mhamasishaji wa CCM,Katibu mwenezi CCM,naibu katibu mkuu CCM Nk

4. Profesa Shaba
Huyu sijui yupo hai au, anasifika kuufanyia post mortam mwili wa hayati Sokoine, mpaka anastaafu na kumaliza kiinua mgongo hakuwahi kujenga hata choo. Alipostaafu aliigomea Serikali kuachia nyumba iliyokuwa mitaa ya Shaaban Robert karibu na Gymkhkana DSM.

Akiwatisha kuwa ataanika kilichomuua Sokoine if at all they try to vacate him, wakampotezea.

5. Steven Kanumba
Pamoja na kumiliki gari ya mamilioni kadhaa alikufa hajawahi kujenga hata kiosk

6. Ray Kigosi(yuko hai)
Bado anaishi kwa mama yake Sinza hajui hata mfuko wa cement inatoa tofali ngapi

7.

Itaendelea
Jamaa utasababisha jamii forum wavamiwe siku si nyingi na watu wasiojulikana ,Lisa wewe
 
Sasa mbona kuna wengine wako hai na wewe umesema wafu...
 
Looo hakuna mtu wa mkoa wa Kilimanjaro hapo
Ila mtoa mada wewe ni mbea unafuatilia ya watu jiulize Elon Musk tajiri number one duniani ana nyumba?
Mohamed Dewji nina uhakika anayo ila sio kipaumbele chake
wanaojenga nyumba ni watu masikini wasiojiamini na maisha
Wewe hujatembea inaonekana nenda Marekani,Ulaya, na nchi zilizoendelea hakuna mtu eti anajenga nyumba wanachukua lease.Nyumba zinajengwa na real estates companies wewe unanunua
Wewe umesha nunua ngapi? Au unajipa hope tu?
 
yani nipoteze milioni 30 kujenga wakati biblia inasema sisi ni mavumbi..
 
Back
Top Bottom