Bush Dokta
JF-Expert Member
- Apr 11, 2023
- 42,525
- 74,605
Hii ni tetesi kwako?Ndugu yangu MAXENCE MELLO mmiliki wa JAMIIFORUM unatukosea sana JF Members. Haiwezekani tetesi zenye nia mbaya kama hizi ukaendelee kuziacha tu zikienea kwa kasi kwa mwamvuli wa JF.
@moderators ondoeni hii thread hapa jamvini
Vipi mlinzi/ walinzi wa eneo hilo wamehojiwa? Ila humu ndani na huko nje sisi na Chadema na bwana Zitto tulishakubaliana kwamba zama zile za giza zilikuwa za hayati JPM wakati huu mama ameiponya nchi,ameifungua nchi,anaupiga mwingi,ni mwanadiplomasia nguli,ni mcha Mungu na anapenda mazungumzo.
Hofu kubwa imetanda kufuatia tukio la kuvamiwa na kujeruhiwa kwa Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania (TEC) Padri Dkt.Charles Kitima.
Kupitia mitandao ya kijamii, imeripotiwa kuwa watu Wasiojulikana walimvamia Dkt Kitima majira ya saa 3 usiku wa April 30, 2025 na kuanza kumshambulia wakati akiwa kwenye makazi yake yaliyopo Ofisi za Baraza la Maaskofu (TEC) Kurasini, Dar Es salaam.
Mashuhuda wa tukio hilo waliokuwa eneo la tukio lililozungukwa na mgahawa walisema kuwa Padri Dkt Kitima ikiwa ni utamaduni wake wa kupita na kusalimu watu katika mgahawa mmoja eneo hilo, ghafla walitokea watu Wasiojulikana na kuanza kumshambulia kwa sekunde chache na kisha kuondoka.
Padri Kitima alijeruhiwa maeneo mbali mbali ya Mwili maana alikuwa akivuja damu katika sehemu mbalimbali za mwili wake na haijulikani alijeruhiwa na kitu Gani.
Mara baada ya shambulizi hilo, Dkt Kitima amepatiwa matibabu ya awali kwenye Kituo kidogo cha afya cha TEC kilichopo eneo hilo.
=====
UPDATES:
Polisi wadai kumshikilia mmoja: Polisi: Tunamshikilia Mtu mmoja kutokana na tukio la Padri Kitima kushambuliwa
=====
TAARIFA ZA AWALI:
"Tumepokea taarifa muda huu kuwa Father Dr Charles Kitima ameshambuliwa usiku huu nyumbani kwake na kujeruhiwa vibaya - hali yake si nzuri
Tunaendelea kufuatilia hii taarifa ila ieleweke kuwa shambulio kama hii hatuwezi kuchukulia kama bahati mbaya "
Ameandika hivyo Maria Sarungi kupitia mtandao wa X.
Ikumbukwe Padre Charles Kitima ni Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).
Kama hizi ni taarifa za kweli, ni nini hatima ya hali hii inayoendelea nchini?
CCM mnataka kutupeleka wapi kama taifa?
View attachment 3321209
View attachment 3321207
😀😀😀Ningekuwa mimi ni member wa Jesuit hili lisingepita hivi hivi.
Ukweli utajulikana vipi kama watuhumiwa na washirika wao ndiyo wapelelezi?!!
Serikali yenyewe ya CCM imegawanyika. Yanayoendelea ndiyo dalili.
Kusema serikali ndo imehusika sidhani,Serikali ya chama cha mapindizi haijafikia huko
Bora hata ww umeweka wazi kuwa uvumilivu wa kuambiwa ukweli kwa serekali una mipaka.
Pabaya ndio PazuriTunaelekea kubaya.
Tunafata legasi ya shujaa. Haya yote yalihasisisiwa na shujaa. Kuanzia risasi 17 mchana kweupeJamani c tulikubaliana JPM Ndo alikuwa katili mpaka watu kufurahia kifo chake na kusema mama ameiponya nchi, hii imetoka wapi tena wakuu 😎
Hofu kubwa imetanda kufuatia tukio la kuvamiwa na kujeruhiwa kwa Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania (TEC) Padri Dkt.Charles Kitima.
Kupitia mitandao ya kijamii, imeripotiwa kuwa watu Wasiojulikana walimvamia Dkt Kitima majira ya saa 3 usiku wa April 30, 2025 na kuanza kumshambulia wakati akiwa kwenye makazi yake yaliyopo Ofisi za Baraza la Maaskofu (TEC) Kurasini, Dar Es salaam.
Mashuhuda wa tukio hilo waliokuwa eneo la tukio lililozungukwa na mgahawa walisema kuwa Padri Dkt Kitima ikiwa ni utamaduni wake wa kupita na kusalimu watu katika mgahawa mmoja eneo hilo, ghafla walitokea watu Wasiojulikana na kuanza kumshambulia kwa sekunde chache na kisha kuondoka.
Padri Kitima alijeruhiwa maeneo mbali mbali ya Mwili maana alikuwa akivuja damu katika sehemu mbalimbali za mwili wake na haijulikani alijeruhiwa na kitu Gani.
Mara baada ya shambulizi hilo, Dkt Kitima amepatiwa matibabu ya awali kwenye Kituo kidogo cha afya cha TEC kilichopo eneo hilo.
=====
UPDATES:
Polisi wadai kumshikilia mmoja: Polisi: Tunamshikilia Mtu mmoja kutokana na tukio la Padri Kitima kushambuliwa
=====
TAARIFA ZA AWALI:
"Tumepokea taarifa muda huu kuwa Father Dr Charles Kitima ameshambuliwa usiku huu nyumbani kwake na kujeruhiwa vibaya - hali yake si nzuri
Tunaendelea kufuatilia hii taarifa ila ieleweke kuwa shambulio kama hii hatuwezi kuchukulia kama bahati mbaya "
Ameandika hivyo Maria Sarungi kupitia mtandao wa X.
Ikumbukwe Padre Charles Kitima ni Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).
Kama hizi ni taarifa za kweli, ni nini hatima ya hali hii inayoendelea nchini?
CCM mnataka kutupeleka wapi kama taifa?
View attachment 3321209
View attachment 3321207
Serikali hii ndiyo impiga Lissu risasi,ilimpoteza Ben Saanane na Azori Gwanda,iiwapoteza Dionis Kipanya, Soka na wenzake wawili,ilimpoteza Chaula,ilimuua kikatili Ali Kibao,ilmbambikia Mbowe kesi ya Ugaidi, imembambikia Lissu kesi ya uhaini,imewapiga na kuwavunja mikono na miguu wanachama wa Chadema, imeua wagombea wa Chadema kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa,nini isichoweza? CCM ni genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kutawala.Kusema serikali ndo imehusika sidhani,Serikali ya chama cha mapindizi haijafikia huko
Hata swala la Kibao mpaka leo tunasubiri ukweli ujulikaneTetesi za kushambuliwa kwa Padri Kitima na kuhusishwa kwa serikali hazipaswi kuchukuliwa kama ukweli bila ushahidi. Serikali haina sababu ya kumlenga kiongozi wa dini ambaye hana uhasama wowote wa moja kwa moja nayo. Katika mazingira ya sasa, si ajabu kuona tukio la uhalifu likigeuzwa ajenda ya kisiasa. Tuwe makini na propaganda, tusubiri ukweli ujulikane.
Hakuwahi kuwa mnafiki Full stop .
Mtu mnafiki ni hatari sana .
Anajifanya yupo mbali kumbe yupo karibu .
Wtakifanya anakipenda kumbe ni adui yako namba moja .
Mnafiki ni hatari sana kwenye ulimwengu huu .
Hizi ni siasa za CCM sio za Magufuli . Tofauti za watawala wa CCM ni kiwango cha unafiki na wizi .
Nijuavyo mimi rais akiwa mkristo akishambuliwa sheikh ndio huleta shida. Ila wakristo sio watu wa kujibu mapigo hata wakiuliwa mapadre.Tabia mlizofundishana za kuumizaumiza watu kisa wako tofauti na misimamo yenu matokeo yake ndio haya sasa, Vijana wenu hawaijui mipaka nakuparamia Kila mtu sasa wakijua wanafurahisha mabwana zao kumbe ndio wanaharibu sasa.
Serikali inapaswa kujua, katika hili hakuna atakayeamini serikali haihusiki na matokeo ya hili ni hatari sana kuliko mnavyofikiria, inawezekana isiwe leo ila in future ni hatari sana, huwa vijana wenu hawapimi wanapofanya huu ujinga bali wanaangalia leo sio Kwa maslahi ya future ya Taifa.
Kumuumiza yule Padri wa Catholic huku Rais akiwa Muislamu na kuungwa mkono na Masheikh, hatari yake ni kubwa kuliko mnavyofikiria, MNAPASWA KUPIMA MATENDO YENU.
Hakuna Mkatoriki atakayeamini hili ni tukio la kawaida bali imani lazima iegamie kwenye serikali na mambo ya kisiasa.
Muwe mnapima kwanza kabla ya kuchukua hatua.
Hii ni tetesi kwako?
View: https://www.instagram.com/p/DJGavXLM40G/?igsh=YzljYTk1ODg3Zg==
Chama kimekuwa cha mapangaHiki chama kimepoteza dira