Padri Kitima ashambuliwa na watu wasiojulikana. Inadaiwa hali yake ni mbaya

Padri Kitima ashambuliwa na watu wasiojulikana. Inadaiwa hali yake ni mbaya

Kanisa katoliki aliendeshwi kwa ushabiki wa waumini wake na linaheshimu serikali.

Msingi wa social engagement ya viongozi wa kanisa ni ‘Canon law’, sasa usidhani ukitafuta ugomvi na serikali ya nchi husika kanisa lita intervene kwa niaba yako.


Kwa nchi kama marekani upande wa Catholic Church rules ni kwamba viongozi wa kanisa ni marufuku kuwa na upande wa siasa.

It’s OK kanisa kuwa na opion ata kuchagua upande wa debate kwenye maswala moral issues (especially church morals).

Vinginevyo uwezi kuwa openly compromised kanisa likutete wanamipaka yao na na kanuni zao za social and political engagement.

Learn the rules Roman Catholic Canon Law

Kanisa aliendeshwi, kusimamiwa au kujiingiza kwenye maswala yasiyo wahusu kwa kukurupuka.

Hope, Kitima will fully recover kama kweli ameshambuliwa usiku huu. Nonetheless it was coming.

Ukijiingiza kwenye siasa ukawa na upande, elewa kabisa upande wa pili wewe ni mpinzani.

JK aliwahi sema hakuna shida viongozi wa dini kuwa wanasiasa, ila kama wanataka siasa wavue majoho yao kwanza. Lakini sio kutumia waumini wao kwenye siasa.

Uvumilivu una mipaka
Bora hata ww umeweka wazi kuwa uvumilivu wa kuambiwa ukweli kwa serekali una mipaka.
 
Hakuwahi kuwa mnafiki Full stop .
Mtu mnafiki ni hatari sana .
Anajifanya yupo mbali kumbe yupo karibu .
Wtakifanya anakipenda kumbe ni adui yako namba moja .

Mnafiki ni hatari sana kwenye ulimwengu huu .
Hizi ni siasa za CCM sio za Magufuli . Tofauti za watawala wa CCM ni kiwango cha unafiki na wizi .
Daah
 

Hofu kubwa imetanda kufuatia tukio la kuvamiwa na kujeruhiwa kwa Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania (TEC) Padri Dkt.Charles Kitima.

Kupitia mitandao ya kijamii, imeripotiwa kuwa watu Wasiojulikana walimvamia Dkt Kitima majira ya saa 3 usiku wa April 30, 2025 na kuanza kumshambulia wakati akiwa kwenye makazi yake yaliyopo Ofisi za Baraza la Maaskofu (TEC) Kurasini, Dar Es salaam.

Mashuhuda wa tukio hilo waliokuwa eneo la tukio lililozungukwa na mgahawa walisema kuwa Padri Dkt Kitima ikiwa ni utamaduni wake wa kupita na kusalimu watu katika mgahawa mmoja eneo hilo, ghafla walitokea watu Wasiojulikana na kuanza kumshambulia kwa sekunde chache na kisha kuondoka.

Padri Kitima alijeruhiwa maeneo mbali mbali ya Mwili maana alikuwa akivuja damu katika sehemu mbalimbali za mwili wake na haijulikani alijeruhiwa na kitu Gani.

Mara baada ya shambulizi hilo, Dkt Kitima amepatiwa matibabu ya awali kwenye Kituo kidogo cha afya cha TEC kilichopo eneo hilo.

=====
UPDATES:

Polisi wadai kumshikilia mmoja: Polisi: Tunamshikilia Mtu mmoja kutokana na tukio la Padri Kitima kushambuliwa

=====
TAARIFA ZA AWALI:

"Tumepokea taarifa muda huu kuwa Father Dr Charles Kitima ameshambuliwa usiku huu nyumbani kwake na kujeruhiwa vibaya - hali yake si nzuri

Tunaendelea kufuatilia hii taarifa ila ieleweke kuwa shambulio kama hii hatuwezi kuchukulia kama bahati mbaya "

Ameandika hivyo Maria Sarungi kupitia mtandao wa X.

Ikumbukwe Padre Charles Kitima ni Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

Kama hizi ni taarifa za kweli, ni nini hatima ya hali hii inayoendelea nchini?

CCM mnataka kutupeleka wapi kama taifa?

View attachment 3321209

View attachment 3321207
Wanzanzibari waliopenyezwa kwenye mfumo ndio wanaopanga na kutekeleza mauaji huku tanganyika
 
Hii ni hatari kubwa sana, ni Habari mbaya sana hii.
Endapo kama Habari hii ni ya kweli, basi Serikali inapaswa kufanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha kwamba inauthibitishia Umma kwa vitendo kwamba yenyewe Kamwe haihusiki kwa namna yoyote ile na shambulizi hilo.
Serikali inapaswa ifanye hivyo kwa UAMINIFU MKUBWA ili kuondokana na mashaka yoyote yale kutoka kwa Umma.

Ikumbukwe kwamba: Watu bado hawasahau kabisa kuhusiana na suala la Marehemu Mzee Kibao na suala la jaribio la Mauaji dhidi ya Tundu Lisu ambaye yupo mahabusu gerezani sasa hivi.

Hata kama tukio hilo limetekelezwa na Maadui zake binafsi huyo Padre Kitima, bado Serikali ndiyo itakayonyoshewa kidole zaidi. Hii ni kutokana na Ukweli mchungu Sana kwamba Mazingira halisi yaliyopo hivi Sasa hapa Tanzania Kati ya huyo Padre na Watawala yanaonekana kuwa 'yamekorogeka vibaya sana.'
Very bad timing for the execution of such a satanic action!
Serikali yenyewe ya CCM imegawanyika. Yanayoendelea ndiyo dalili.
 

Hofu kubwa imetanda kufuatia tukio la kuvamiwa na kujeruhiwa kwa Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania (TEC) Padri Dkt.Charles Kitima.

Kupitia mitandao ya kijamii, imeripotiwa kuwa watu Wasiojulikana walimvamia Dkt Kitima majira ya saa 3 usiku wa April 30, 2025 na kuanza kumshambulia wakati akiwa kwenye makazi yake yaliyopo Ofisi za Baraza la Maaskofu (TEC) Kurasini, Dar Es salaam.

Mashuhuda wa tukio hilo waliokuwa eneo la tukio lililozungukwa na mgahawa walisema kuwa Padri Dkt Kitima ikiwa ni utamaduni wake wa kupita na kusalimu watu katika mgahawa mmoja eneo hilo, ghafla walitokea watu Wasiojulikana na kuanza kumshambulia kwa sekunde chache na kisha kuondoka.

Padri Kitima alijeruhiwa maeneo mbali mbali ya Mwili maana alikuwa akivuja damu katika sehemu mbalimbali za mwili wake na haijulikani alijeruhiwa na kitu Gani.

Mara baada ya shambulizi hilo, Dkt Kitima amepatiwa matibabu ya awali kwenye Kituo kidogo cha afya cha TEC kilichopo eneo hilo.

=====
UPDATES:

Polisi wadai kumshikilia mmoja: Polisi: Tunamshikilia Mtu mmoja kutokana na tukio la Padri Kitima kushambuliwa

=====
TAARIFA ZA AWALI:

"Tumepokea taarifa muda huu kuwa Father Dr Charles Kitima ameshambuliwa usiku huu nyumbani kwake na kujeruhiwa vibaya - hali yake si nzuri

Tunaendelea kufuatilia hii taarifa ila ieleweke kuwa shambulio kama hii hatuwezi kuchukulia kama bahati mbaya "

Ameandika hivyo Maria Sarungi kupitia mtandao wa X.

Ikumbukwe Padre Charles Kitima ni Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

Kama hizi ni taarifa za kweli, ni nini hatima ya hali hii inayoendelea nchini?

CCM mnataka kutupeleka wapi kama taifa?

View attachment 3321209

View attachment 3321207
Wamegusa pabaya sana. Yaani usicheze na VATICAN, hawa watu wanaisaidia sana nchi yetu kwenye mambo ya usalama na wapo kila Kona ya nchi hii, Hadi jeshini wapo. Sasa wameligoroga. Narudia Tena: WAMELIGOROGA NA WATALINYWA" mwisho wa kunukuu.
 
Back
Top Bottom