Padri Kitima ashambuliwa na watu wasiojulikana. Inadaiwa hali yake ni mbaya

Vipi mlinzi/ walinzi wa eneo hilo wamehojiwa? Ila humu ndani na huko nje sisi na Chadema na bwana Zitto tulishakubaliana kwamba zama zile za giza zilikuwa za hayati JPM wakati huu mama ameiponya nchi,ameifungua nchi,anaupiga mwingi,ni mwanadiplomasia nguli,ni mcha Mungu na anapenda mazungumzo.
 
Ukweli utajulikana vipi kama watuhumiwa na washirika wao ndiyo wapelelezi?!!
Serikali yenyewe ya CCM imegawanyika. Yanayoendelea ndiyo dalili.
Kusema serikali ndo imehusika sidhani,Serikali ya chama cha mapindizi haijafikia huko
Bora hata ww umeweka wazi kuwa uvumilivu wa kuambiwa ukweli kwa serekali una mipaka.

Kutokana na tukio hili, ni dhahiri kwamba sasa Viongozi wa Imani wenye mitazamo huru au kuwa na maoni huru kuhusiana na masuala ya kijamii wameanza kulengwa moja kwa moja na Wadhalimu Wasiopenda Fikra mbadala.
Viongozi wa dini wafuatao kuanzia sasa wanapaswa kuchukua hatua za ziada kuhusiana na suala la Usalama wao binafsi:-
1. Askofu wa KKKT Bw. Benson Bagonza.
Kwa mwendo huu, bila shaka Askofu Benson Bagonza ndiye anayefuatia kukumbwa na USHETANI huu uliozinduliwa leo kwa Padre Kitima.

Chonde chonde Baba Askofu Benson Bagonza tafadhali Sana uchukue tahadhari kubwa sana ili ushetani wa namna hii usikumbane nao.
 
Tabia mlizofundishana za kuumizaumiza watu kisa wako tofauti na misimamo yenu matokeo yake ndio haya sasa, Vijana wenu hawaijui mipaka nakuparamia Kila mtu sasa wakijua wanafurahisha mabwana zao kumbe ndio wanaharibu sasa.

Serikali inapaswa kujua, katika hili hakuna atakayeamini serikali haihusiki na matokeo ya hili ni hatari sana kuliko mnavyofikiria, inawezekana isiwe leo ila in future ni hatari sana, huwa vijana wenu hawapimi wanapofanya huu ujinga bali wanaangalia leo sio Kwa maslahi ya future ya Taifa.

Kumuumiza yule Padri wa Catholic huku Rais akiwa Muislamu na kuungwa mkono na Masheikh, hatari yake ni kubwa kuliko mnavyofikiria, MNAPASWA KUPIMA MATENDO YENU.
Hakuna Mkatoriki atakayeamini hili ni tukio la kawaida bali imani lazima iegamie kwenye serikali na mambo ya kisiasa.
Muwe mnapima kwanza kabla ya kuchukua hatua.
 
Jamani c tulikubaliana JPM Ndo alikuwa katili mpaka watu kufurahia kifo chake na kusema mama ameiponya nchi, hii imetoka wapi tena wakuu 😎
Tunafata legasi ya shujaa. Haya yote yalihasisisiwa na shujaa. Kuanzia risasi 17 mchana kweupe
 
Jesuit brotherhood Vs Wasiojulikana
Ngoja tusubiri hii game of death
 

Mama dhamiria kutupa katiba mpya ila baada ya kuingia madarakani 2025 kwa namna yoyote.

Anajua na Lissu mgombea mwingine uchaguzi huru hatoboi.

Anapanga kumwachia TAL baada ya uchaguzi alioudharimia kwa ajili ya kuhalalisha kujisimika kinunda.

Looh!

Ama kweli madaraka matamu.
 
Kusema serikali ndo imehusika sidhani,Serikali ya chama cha mapindizi haijafikia huko
Serikali hii ndiyo impiga Lissu risasi,ilimpoteza Ben Saanane na Azori Gwanda,iiwapoteza Dionis Kipanya, Soka na wenzake wawili,ilimpoteza Chaula,ilimuua kikatili Ali Kibao,ilmbambikia Mbowe kesi ya Ugaidi, imembambikia Lissu kesi ya uhaini,imewapiga na kuwavunja mikono na miguu wanachama wa Chadema, imeua wagombea wa Chadema kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa,nini isichoweza? CCM ni genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kutawala.
 
Hata swala la Kibao mpaka leo tunasubiri ukweli ujulikane
 

Ukiwa Ndani ya CCM ni lazima uwe mnafiki, aidha uwe unapenda au haupendi. Kuwa mnafiki ndani ya CCM ndio njia pekee ya kuweza kuwa salama, kinyume chake utahesabika kama ni Mtu hatari na Msaliti kwa chama hicho. Nafikiri utakuwa unakumbuka kilichompata yule aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Horace Kolimba pale alipochoka kuendelea kuwa Mnafiki na kisha kuamua kuachana na Unafiki na kuwa Mtu mkweli.
 
Nijuavyo mimi rais akiwa mkristo akishambuliwa sheikh ndio huleta shida. Ila wakristo sio watu wa kujibu mapigo hata wakiuliwa mapadre.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…