HOJA Pale Kariakoo tuvunje shule ya Benjamin Mkapa na Uhuru mchanganyiko ili tupate eneo la Parking

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Magorofa mengi Upanga,Oysterbay,Masaki,Mikocheni hayakosi parking basement au kwenye compound kwasababu bila hivyo huwezi kupata wapangaji. Mtu hawezi kulipa $2000 kwa mwezi halafu akose parking.
Ukija Kariakoo kuanzia wanaojenga hadi wapangaji ni local tu ili mradi feremu iko barabarani tu. Ila mipango miji ilitakiwa waweke sheria basement parking ni lazima kama walivyoweka sheria lazima jengo kuanzia ghorofa tatu liwe na lift.
 
Kumbuka hayo magorofa unayoyasemea yalijengwa miako ya 1950s kipindi hiko magari yanahesabika
 
Sheria zipo ni ukaidi wao tu hao wamiliki wa majengo,Tungepata raisi jamii ya magufuli lingetekelezwa ilo jambo,karibia nusu ya majengo ya kariakoo yana basement ila kwao wameona biashara zinaumuhimu kuliko parking................
 
Magorofa ya kariakoo yalijengwa miaka ya nyuma sana 1950s
 
haiwezekani zivunjwe shule ili mje kupaki vi paso na vi ist vyenu watu wenye magari yenye thamani kuanzia mi50+ ndo wadai parking nyie wengine mnaleta jam mjini parking yenu iwe nje ya kkoo
 
haiwezekani zivunjwe shule ili mje kupaki vi paso na vi ist vyenu watu wenye magari yenye thamani kuanzia mi50+ ndo wadai parking nyie wengine mnaleta jam mjini parking yenu iwe nje ya kkoo
Patengenezwe parking ya kutosha hata gari 300,000 kila gari itozwe 2500/- jiji lipate fedha liache kukimbizana na wanyonge mitaani kwa ajili ya njaa!,na kuondosha shuru zenye KERO!...
#Gari zote zinazopaki madukani ndani ya kariakoo zitapaki humo,ili wanunuzi waachane na kero za magari wakiwa madukani!,
Simple calculation italeta
750,000,000/-PER DAY!..(Wanapaki asubuhi jioni wanaondoka wanalipa gatini)
#Bongolala mmepata maarifa?
 
Calculation ya kisomi
 
Wazo la kipumbavu sana hili.
 
Hapana mkuu

Hayo ni madhara ya kutoheshimu longterm plans.

Eneo lile mtu alie na akili angejua tu in 20 years lazima business centre itanuke na ichangamke.
Mkuu, nadhani umegeuza tatizo kinyume. Nina maana kuwa kutoheshimu long term plans ndiyo kumefanya liwe eneo la biashara badala ya lengo lililokusudiwa. Eneo la Karume kwa ujumla lilikusanya viwanja vya mpira, shule na possibly eneo la wazi lenye bustani. Mji ni lazima uwe na maeneo ya wazi. Huu ujinga wa kukusanya kila kitu eneo moja ndiyo hasa umeleta hilo tatizo. BTW tungekuwa na viongozi wenye akili badala ya kamasi sasa hivi Dar ingekuwa imejengwa kwa mpango mpya maeneo kama Bagamoyo na jiji jipya likaunganishwa na la zamani kwa treni/metro za kasi.
 
Najiulizaga wale watoto mule wanasomaje somaje na makelele yake ya kariakoo mara utasikia ya moto moto, mara shanga shanga , mara dawa za nguvu za kiume zinatangazwa yaani fujo tu ..wangeziamisha zile shule pale..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…