Pambalu utaiondoaje serikali ya CCM bila kushiriki uchaguzi wa October 29, 2025?, Kazi unayo

Pambalu utaiondoaje serikali ya CCM bila kushiriki uchaguzi wa October 29, 2025?, Kazi unayo

Kama kungekuwa na matumizi mabaya shule, hospitali, mikopo ya wanafunzi, reli, barabara, madaraja, mabwawa, umeme nchi nzima, kulipa watumishi, askari, mahakama, majaji, wabunge, maji, meli, viwanja vya mpira, pembejeo kwa wakulima, nk vingegharamiwa na nini? Hayo wadanganye wavuta bangi wenzako kijiweni kuwa hakuna lolote serikali imefanya hela zinaliwa tu. Unadhani watz wote ni wavuta misuba hawajui serikali yao inafanya nini na kodi zetu?

Kama ufaransa wanalalamika hali mbaya sembuse sisi bhana?
Ujinga mtupu,angalia nilichoandika na ulichojibu!Hivi mmelishwa maharagwe ya wapi?
Punguza mihemko,rudisha ubongo wako kichwani ndio uje hapa!
 
Kijana Pambalu alijua kuwa kwakusema vile lazima atakamatwa tu ili asiwepo (ajivunje) wakati wa kukinukisha. Baadae atadai nilikuwa ndani sikuhusiki na vurugu. Lakini sisi tunafahamu yeye alikuwa Kenya kusuka mipango ya kuiondoa serikali ya CCM madarakani kqa njia haramu.
Baseless accusations!Mambo ya kutekana,kuuana na kubambikiziana kesi kisa tofauti za kisiasa ni ushamba,ujinga na ulevi wa madaraka!
 
Baseless accusations!Mambo ya kutekana,kuuana na kubambikiziana kesi kisa tofauti za kisiasa ni ushamba,ujinga na ulevi wa madaraka!
Kama amebambikiziwa kesi au la subiri mahakama itasema nini ndiyo useme kabambikiziwa au la. Utawala wa sheria unatutaka tufanye hivyo. Kama una malalamiko dhidi ya serikali au CCM washitaki mahakamani.
 
Hakuna lolote,mifano hai ni mingi!Mmekuwa mnawabambika wapinzani kesi kubwa kubwa ili muwakatishe tamaa na siasa zao za kutaka mabadiliko Katika mifumo mbalimbali!
Mnawapa kesi ambazo hazina dhamana ili kuwakomoa,it's a shame!
 
Yaani intellegensia yoooote taifa iliyonayo ishindwe kugundua Pambalu, chadema na wale wengine wanawaza na kupanga nini. Unadhani taifa linaongozwa na vilaza kama nyie?

Subiri utaona kazi ya intelijensia yetu ilivyo mahiri.
Nyinyi uvccm mna intelijensia gani zaidi ya ujinga tu. Elimu zenyewe ni za kuunga unga, za hapa na pale, kufoji vyeti, na kusoma QT! Uwezo wenu pekee ni huu wa kubambikia watu kesi na kufanya ufisadi. Hakuna kingine.
 
Intelijensia inayofanywa kazi inaruhusu je mauaji ya October 29 yatokee?????.
Kama kweli inafanyakazi then ndo iliyoratibu mauaji hayo.
 
Hebu tutafakari kidogo tu. Chadema walisusa kushiriki uchaguzi wa 2025. Pambalu kwenye hotuba yake kasema kuwa nia yao chadema ni kuiondoa serikali ya CCM madarakani ili wapate mabadiliko ya kweli.

Utawezaje kuiondoa serikali ya CCM madarakani bila kushiriki uchaguzi?. Pambalu anayo njia gani nyingine ya kuiwezesha chadema kuiondoa serikali ya CCM madarakani ili walete mabadiliko ya kweli?

Je, Ni njia gani nyingine (badala ya kushiriki uchaguzi) walikusudia kuitumia ili kuiondoa serikali ya CCM madarakani?

Je, hotuba yake hii hapa haikutosha kuitishia serikali ya CCM kuanguka?

Je, vurugu za October 29, 2025 ndio njia yao madhubuti mbadala (kuliko uchaguzi) ya kuiondoa serikali ya CCM madarakani?

Je, Kukamatwa na kufunguliwa mashitaka ili akajieleze mbele ya chombo cha haki ameonewa?

View: https://youtu.be/I4aMQbJJoO4?si=zUH3Wxdc3rLVTIpU

View: https://youtu.be/IFI32sm3uK4?si=_Tl8ib4x9iws0-YC

Wakati mwingine, ficha ujinga kidogo,
Utawala huu wa ccm hauna tofsuti na ulivyokuwa utawala wa KANU kule Kenya,
Je Kenya waliwezaje kuiondoa KANU madarakani? Si kwa kushiriki chaguzi ambazo referee kawekwa na KaNU, ni katiba mpya ndio iliwezesha, achaujinga bro, watu wamekuambia vyombo vote vya ulinzi na usalama ni mali ya ccm, yaani intelijensia, jazz, polisi, magereza, ni instruments za chama,utashindanao vipi kwenye u chaguzi, wanaosimamia wenyewe!
Kesi kati ya Simba na swala,hakimu ni Chui!
 
Siyo mbaya nikaazima usemi fulani na kusema serikali inatenda maajabu nashindwa kueleza.

Upande mwingine inahimiza kuridhiana, ila upande mwingine ni inapeleka moto kwa upinzani nonstop. Sielewi kama idea ni kuwapresha waje mezani ama la.

Ila mbona mi naelewa kila mtu ana price? Si kukubaliana tu kwamba unakuja mezani ila utapata 40% instant ya unachotaka 60% itakuja taratibu with time?
 
Baseless accusations!Mambo ya kutekana,kuuana na kubambikiziana kesi kisa tofauti za kisiasa ni ushamba,ujinga na ulevi wa madaraka!
Wewe umebambikiwa kesi ngapi?, umetekwa mara ngapi? Baba yake ametekwa mara ngapi na kubambikiwa kesi lini?. Ongea kama mtu anaejitemea kifikira.
 
Wewe umebambikiwa kesi ngapi?, umetekwa mara ngapi? Baba yake ametekwa mara ngapi na kubambikiwa kesi lini?. Ongea kama mtu anaejitemea kifikira.
Ndio maana niko JF,mawazo yangu haya siwezi kuyatoa nje na hapa kwasababu ya usalama wangu na familia yangu!
Waliojaribu kufanya hivyo hadharani,Wanajua wamayopitia au waliyowahi kupitia!Mifano hai ni mingi!
 
Siyo mbaya nikaazima usemi fulani na kusema serikali inatenda maajabu nashindwa kueleza.

Upande mwingine inahimiza kuridhiana, ila upande mwingine ni inapeleka moto kwa upinzani nonstop. Sielewi kama idea ni kuwapresha waje mezani ama la.

Ila mbona mi naelewa kila mtu ana price? Si kukubaliana tu kwamba unakuja mezani ila utapata 40% instant ya unachotaka 60% itakuja taratibu with time?
CHadema wanafanya siasa za udalali, boss yuko ulaya magharibi. Ndiyo maana kila wakati wanaitaka ulaya ije isuluhishe kama vile serikali haijui kuwa boss wao yuko ulaya.

Kama ulaya wangekuwa mahodari wa kusuluhisha wagombanao kwanini hawaendi kuwasuluhisha Urusi n Ukraine , Israel na waarabu?

Serikali inawabembeleza kwakuwa amani n utulivu ni sera ya CCM. Tunatafuta amani na utulivu si kwa watu wa tz tu bali hata kwa wakimbizi, DRC, Msumbiji, Darful, Lebanon. Tunatafuta amani n utulivu hata kwa wanyama wa Ngorongoro na miti.
 
Ujinga mtupu,angalia nilichoandika na ulichojibu!Hivi mmelishwa maharagwe ya wapi?
Punguza mihemko,rudisha ubongo wako kichwani ndio uje hapa!
Wewe ccm unao ubongo? Umeutoa wapi? nani kakukubalia utumie ubongo? na kama ukijulikana unatumia ubongo utafutwa uanachama na utapotezwa shauri yako!
 
Ndio maana niko JF,mawazo yangu haya siwezi kuyatoa nje na hapa kwasababu ya usalama wangu na familia yangu!
Waliojaribu kufanya hivyo hadharani,Wanajua wamayopitia au waliyowahi kupitia!Mifano hai ni mingi!
WAcha urongo. Mbona Mpina, Zito, Mnyika, Nshala, Dr. SLAA, Lipumba, Maalim Mbatia. SIGIRADA, nk wanakosoa hawakamatwi
 
WAcha urongo. Mbona Mpina, Zito, Mnyika, Nshala, Dr. SLAA, Lipumba, Maalim Mbatia. SIGIRADA, nk wanakosoa hawakamatwi
Nchimbi nae yupo polepole , ben saanane mdude wote wapo kabisa!
 
Kwani CHADEMA wamesema hawatakaa washiriki uchaguzi? Mabadiliko wanayoyataka kitimia, si wanashiriki uchaguzi na kuishinda, hivyo kuiondoa ccm madarakani?
 
WAcha urongo. Mbona Mpina, Zito, Mnyika, Nshala, Dr. SLAA, Lipumba, Maalim Mbatia. SIGIRADA, nk wanakosoa hawakamatwi
Hujui tu historia,nenda kafuatilie hao wote wameshakutana na mambo mangapi kwenye siasa za nchi hii!
 
Wewe ccm unao ubongo? Umeutoa wapi? nani kakukubalia utumie ubongo? na kama ukijulikana unatumia ubongo utafutwa uanachama na utapotezwa shauri yako!
Kama hawana ubongo lakini madaraja marefu sana kuliko yote Afrika wanajenga shida iko wapi? Kama Marekani na ujuaji, usomi na ubongo walionao lakini waliwachagua Trump na Biden basi ubongo hauna maana kuutumia hata kuwa nao.

CCM chama cha kwanza Afrika kusambaza umeme nchi nzima kwa 100%, shule kila kijiji kwa 100%, zahanati kwa 98%. Kwa babaj unatoka Dar hadi Kigoma.
 
Nyinyi uvccm mna intelijensia gani zaidi ya ujinga tu. Elimu zenyewe ni za kuunga unga, za hapa na pale, kufoji vyeti, na kusoma QT! Uwezo wenu pekee ni huu wa kubambikia watu kesi na kufanya ufisadi. Hakuna kingine.
Endeleeni tu na kuishtuashtua CCM isilale usingizi wa pono. Anaeomba vyama vya upinzani vife nchini ni mpumbavu sana, ni sawa na kuombea Simba au Yanga mojawapo itoweke kabisa kwenye ligi.
 
Kama hawana ubongo lakini madaraja marefu sana kuliko yote Afrika wanajenga shida iko wapi? Kama Marekani na ujuaji, usomi na ubongo walionao lakini waliwachagua Trump na Biden basi ubongo hauna maana kuutumia hata kuwa nao.

CCM chama cha kwanza Afrika kusambaza umeme nchi nzima kwa 100%, shule kila kijiji kwa 100%, zahanati kwa 98%. Kwa babaj unatoka Dar hadi Kigoma.
Hao waliomchagua,huyu muuaji hakuchaguliwa na wananchi!
 
Back
Top Bottom