Vijana wanauliza inatakiwa wapewe majibu wajifunze badala ya kuwashambulia, wanataka kujua faida za kupisha watu seat ni zipi, zinathibitika au ni myths tu?
Zingatia mukutadha huu:-
Mpo stand, gari ni nyingi tu ambazo zina nafasi. Kijana kafika stand kaingia kwenye gari lenye nafasi kisha kapoteza muda wake kusubiri gari lijaze ili liondoke, halafu ghafula mzee mmoja anaacha gari zote zenye seat anakuja kwenye hii iliyojaza (kwa kigezo cha kuwa itawahi kuondoka), kitegemea kupishwa na huyu kijana.
Maswali:
1. Huyu kijana ashuke kwenye hiyo gari (kumpisha mzee) arudi kwenye nyingine ambazo hazina watu ili asubiri mpaka zijaze tena? Akitokea mzee mwingine vipi, ashuke tena?
2. Kuna ugumu upi ambao huyo mzee ataupata akiamua kupanda gari ya nyuma (hapo stand) ambayo ina seat, badala ya kufanya makusudi akitarajia huruma? Maana kimsingi binadamu wote tuna haraka.
3. Kijana asimame kwenye safari yenye umbali wa 20KM, kwasababu kuna mzee fulani hakutaka kupanda gari za nyuma zenye seat hapo stand? Haiingii akili hata kidogo.
NB: Binafsi naona kuna mazingira ambayo hatupaswi kuendekeza uzee ili kuwakandamiza vijana.