Pamoja na kuvurugika kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ni kwanini Waziri Jafo hajiuzulu?

Mkuu madaraka na wananchi ni mambo ya kwenda na tahadhari kubwa sana.
Ushawishi na kukubalika kwa kila linaloamuliwa ni muhimu sana kwaniaba ya wananchi hao hao.
Serikali na vyombo vyake vyote vya ulinzi na usalama haviwezi kufua dafu mbele ya umma uliotofauti na wao.

Kumbuka serikali na vyombo vyake vyote hawawezi fika watu laki tano nchi nzima, lakini kwa Jiji kama DSM hata wakiandamana watu laki tano hakuna wa kuwazuia.

Si mfano mzuri lakini hizi sarakasi zisizo na tija zinaweza kutufikisha huko.

Jana Ujerumani ili adhimisha miaka 30 ya kuvunja ukuta uliotenganisha Ujerumani magharibi na mashariki.

Siku hiyo watu wengi sana waliandamana, na hivyo basi askari kushindwa kupiga risasi kujihami au kushambulia.
Rais wa Ujerumani mashariki Erick Honecker ilibidi tu ajifiche kutoka hasira za wananchi.
Tuliona na tulikuwepo 1989.

Hiyo ndo nguvu ya wananchi wasipokubaliana na msimamo rasmi.
 
Kama nilivyosema huko nyuma, kulinda INTEGRITY Jafo inabidi kuchukuabuamuzi binafsi na mgumu.

Ama sivyo jina la Jafo linachafuka milele.
 
Utendaji mbaya wa Rais kwenye kuheshimu demokrasia, uhuru na haki za watu unaeleweka ndani ya nchi yetu na nje ya Taifa letu. Kila mmoja anajua kuwa Rais wetu anapendelea na angefurahi kama tungekuwa na mfumo wa kidikteta.

Jafo ana nafasi yake kama binadamu. Nafasi ya kuamua - aendane na katiba afukuzwe au uungane na ushetani ili kupata faida ya tumbo ya leo na kuishi katika ufukara wa hekima, utu, utashi na ubinadamu, milele.

Mimi nimewahi kufuatwa na viongozi wa CCM na serikali, kundi la watu 9, wakinishawishi nijiunge na CCM, na kuwa nikifanya hivyo nitapewa nafasi ya kugombea au kuteuliwa. Ningekuwa ni mtu ninayefurahia faraja ya tumbo ya leo. Sahizi ningekuwa nao. Lakini nilikataa na wala sitarajii tumbo langu liuamlie mwili wangu wote. Nataka kichwa changu kilicho juu kuliko viungo vyote, na dhamira yangu inayoongozwa na Roho wa Mungu, viuongoze mwili wote. Jafo anashindwa nini?
 
Kama nilivyosema huko nyuma, kulinda INTEGRITY Jafo inabidi kuchukuabuamuzi binafsi na mgumu.

Ama sivyo jina la Jafo linachafuka milele.
Kuchukua uamuzi mgumu afrika?,Tanzania? Tena chini ya Mzee huyuhuyu?wewe utakua hauishi Tanzania,unasoma habari mitandaoni.
Hivi unajua! Acha tu kujiuzuru,kukataa tu uteuzi ni kisa na dharau kwa Stoneman.Utafanyiwa figisu Hadi ukome.
Nikuulize swali,hivi kutoka ccm na kujiunga na chama Cha upinzani ni dhambi?
Kuchagua wapinzani ni dhambi?
 
Lee, mpengine mnasahau kirahisi.

Rais Ali Hassan Mwinyi alisha wahi kuchukua uamuzi mgumu tena wakati wa Mwalimu.

Tendo hilo lilimuongezes sifa na INTEGRITY na mwishowe kufikia urais wa Tanzania.
 
Tunamlaumu Jaffo Wakati tunajua tatizo nini watanzania tutakuwa na akili lini ya kugundua tatizo
 
Duuh ni ngumu sana kwake kukataa kutumika hasa kwenye utawala wa kiongozi aliyepo... Nguvu hizo za kupambana naye hana so ni lazima aungane naye...
 
Ni aibu kabisa mtu mzima anaweza dhani kuwa kwa haya yanayotokea eti Waziri Jafo anaweza jiuzulu.nyie mnadhani kujiuzuli ni kitu chepesi?

Mnataka akale wapi?na ajiuzulu kwa kosa gani ambalo amekitendea chama?mnawaza mambo ya kijinga sana. Kama mna akili hamwezi hata kuwaza kuwa Jafo anatakiwa ajiuzulu.

Ninyi mmesahau miezi kadhaa iliyopita mlikuwa mkimkuza Jafo na kusema ndo waziri smart? Si mlianza na hivyo hivyo kwa kusema Nape Nnauye ndo Mtu mwenye akili?mkaja mkasema Makamba January kwa Vijembe vyake ni mtu smart? Wapo wapi sasa?

JAFO ENDELEA NA UYAFANYAYO MPAKA WAPINZANI WAPATE AKILI WASIMAME WENYEWE NA KUACHA KUTEGEMEA WATU WA CCM WAWASAIDIE.
 
Wewe labda haupo kwenye uongozi /mfumo lakini Jafo yumo.

Akisema anatoa uamuzi wowote kinyume na jiwe hiyo integrity ataisikia tu redioni... Atachafuliwa kila kiungo,
Atakuwa sio raia,
Atakuwa muhujumu uchumi,
Atakuwa mtakatisha fedha,
Atakuwa ametumia vibaya madaraka
Atakuwa fisadi
Muhurumieni tu ana wake na watoto kijiji kizima 😂 😂
 
Waziri wa Tamisemi ni JPM sio Jaffo,

Jaffo ni waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi

Namhurumia Jaffo maana Jiwe anamharibia
 
Watanzania wengi wajinga wanamsukumia zigo Kijana wa watu na kumuacha mhusika
 
Nilisikia akisema majina ya waliopitishwa wa upinzani na waliokata rufaa hayatafutwa kwenye ballot papers!
Ina maana ballot papers zilishachapishwa na hayo majina kabla ya mchujo wa fomu za wagombea?
 
Baada ya kuwaengua sasa mnakuja na porojo zisizokwisha.

Baada ya Upinzani kususia ,eti Jaffo anatangaza kuwarudisha wale walioenguliwa.
Hivi mnategemea kweli CCM,chini ya Waziri Jaffo wasimamie uchaguzi huru na haki.

Tunahitaji Katiba mpya ambayo itaondoa ukiritimba huu wa CCM.
 
Yatumie madaraja vibaya na utaona matokeo yake.
Rais wa Sudan aligundua hilo, mambo yalipobadilika wale waliotakiwa kumlinda ndio wakamsweka selo hadi leo.
 
Kwahiyo mkuu wewe unaamini Jafo kashindwa kisimamia uchaguzi wa serikali za mitaa?
 
Blackmail!
 
Kwahiyo mkuu wewe unaamini Jafo kashindwa kisimamia uchaguzi wa serikali za mitaa?
Mkuu mwenye macho haambiwi tazama.
Watu wameanza kufyekeana mazao vijijini, hivi tusubiri watu waanze kuchomeana nyumba na kuchinjana ndio tuelewe kuwa hali si shwari?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…