Pamoja na kuvurugika kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ni kwanini Waziri Jafo hajiuzulu?

Pamoja na kuvurugika kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ni kwanini Waziri Jafo hajiuzulu?

Jidu hauko serious ndg yangu,!
Unaweza kukataa maagizo ya Mkuu mwenye level ya jiwe hapa Africa?
Sawa mada yako nzuri ila unajifurauisha
Hawawzi kupinga Ma CDF,IGP,DGTISS,PM sembuse ki Jafo?
Acha masihala bana,Namba 1 Tanzania ana nguvu kuliko,leo Kijafo kikatae kutekeleza matakwa yake,!kwani chenyewe hakipendi kupumua au watoto wake waende chooni?
Mkuu madaraka na wananchi ni mambo ya kwenda na tahadhari kubwa sana.
Ushawishi na kukubalika kwa kila linaloamuliwa ni muhimu sana kwaniaba ya wananchi hao hao.
Serikali na vyombo vyake vyote vya ulinzi na usalama haviwezi kufua dafu mbele ya umma uliotofauti na wao.

Kumbuka serikali na vyombo vyake vyote hawawezi fika watu laki tano nchi nzima, lakini kwa Jiji kama DSM hata wakiandamana watu laki tano hakuna wa kuwazuia.

Si mfano mzuri lakini hizi sarakasi zisizo na tija zinaweza kutufikisha huko.

Jana Ujerumani ili adhimisha miaka 30 ya kuvunja ukuta uliotenganisha Ujerumani magharibi na mashariki.

Siku hiyo watu wengi sana waliandamana, na hivyo basi askari kushindwa kupiga risasi kujihami au kushambulia.
Rais wa Ujerumani mashariki Erick Honecker ilibidi tu ajifiche kutoka hasira za wananchi.
Tuliona na tulikuwepo 1989.

Hiyo ndo nguvu ya wananchi wasipokubaliana na msimamo rasmi.
 
Mkuu Jidu hiyo ndo Hali halisi,tangu Zama za Adolf Hitler ni hivyohivyo,huwezi pingana na amri za wakuu hata Kama hupendi,labda use umejiandaa kwelikweli,ama kua muasi,mkimbizi , kufungwa kimizengwe au kuuwawa.
Kama huko mbele Kuna Cha kujibu watu watajibu na Kama ni adhabu hakuna namna,mahakama zikiwa fair haki itatendeka.kijafo hata kikijashitakiwa ni uonevu wa kisheria tu kwa sanabu sheria za duniani haziko fair.
Kama nilivyosema huko nyuma, kulinda INTEGRITY Jafo inabidi kuchukuabuamuzi binafsi na mgumu.

Ama sivyo jina la Jafo linachafuka milele.
 
Bams hua nakuamini Sana,hua siachi kusoma hata komenti yako moja.umeingia kwenye mtego.mtego wa kumsafisha jiwe na hii kadhia.
Je na wewe unaamini kabisa kuwa Jafo ndio kasabisha haya matatizo?
Ana nguvu gani Jafo?
Unaamini Jafo aweza ruhusu uchaguzi huru ili wapinzani washinde?
Jafo!
Utendaji mbaya wa Rais kwenye kuheshimu demokrasia, uhuru na haki za watu unaeleweka ndani ya nchi yetu na nje ya Taifa letu. Kila mmoja anajua kuwa Rais wetu anapendelea na angefurahi kama tungekuwa na mfumo wa kidikteta.

Jafo ana nafasi yake kama binadamu. Nafasi ya kuamua - aendane na katiba afukuzwe au uungane na ushetani ili kupata faida ya tumbo ya leo na kuishi katika ufukara wa hekima, utu, utashi na ubinadamu, milele.

Mimi nimewahi kufuatwa na viongozi wa CCM na serikali, kundi la watu 9, wakinishawishi nijiunge na CCM, na kuwa nikifanya hivyo nitapewa nafasi ya kugombea au kuteuliwa. Ningekuwa ni mtu ninayefurahia faraja ya tumbo ya leo. Sahizi ningekuwa nao. Lakini nilikataa na wala sitarajii tumbo langu liuamlie mwili wangu wote. Nataka kichwa changu kilicho juu kuliko viungo vyote, na dhamira yangu inayoongozwa na Roho wa Mungu, viuongoze mwili wote. Jafo anashindwa nini?
 
Kama nilivyosema huko nyuma, kulinda INTEGRITY Jafo inabidi kuchukuabuamuzi binafsi na mgumu.

Ama sivyo jina la Jafo linachafuka milele.
Kuchukua uamuzi mgumu afrika?,Tanzania? Tena chini ya Mzee huyuhuyu?wewe utakua hauishi Tanzania,unasoma habari mitandaoni.
Hivi unajua! Acha tu kujiuzuru,kukataa tu uteuzi ni kisa na dharau kwa Stoneman.Utafanyiwa figisu Hadi ukome.
Nikuulize swali,hivi kutoka ccm na kujiunga na chama Cha upinzani ni dhambi?
Kuchagua wapinzani ni dhambi?
 
Lee, mpengine mnasahau kirahisi.

Rais Ali Hassan Mwinyi alisha wahi kuchukua uamuzi mgumu tena wakati wa Mwalimu.

Tendo hilo lilimuongezes sifa na INTEGRITY na mwishowe kufikia urais wa Tanzania.
 
Tunamlaumu Jaffo Wakati tunajua tatizo nini watanzania tutakuwa na akili lini ya kugundua tatizo
 
Mleta uzi, naamini kabisa deep dwn unajua Jaffo ni messenger tu, anasimamia na kutekeleza maagizo ya bosi wake.. Aliewaita watendaji wote pale Ikulu hakuwa Jaffo.. Alieawapa amri na viburi hakuwa Jaffo..

Udhaifu pekee ambao tunaweza mlaumu nao Jaffo, ni kukubali kutumika tuu..
Duuh ni ngumu sana kwake kukataa kutumika hasa kwenye utawala wa kiongozi aliyepo... Nguvu hizo za kupambana naye hana so ni lazima aungane naye...
 
Ni aibu kabisa mtu mzima anaweza dhani kuwa kwa haya yanayotokea eti Waziri Jafo anaweza jiuzulu.nyie mnadhani kujiuzuli ni kitu chepesi?

Mnataka akale wapi?na ajiuzulu kwa kosa gani ambalo amekitendea chama?mnawaza mambo ya kijinga sana. Kama mna akili hamwezi hata kuwaza kuwa Jafo anatakiwa ajiuzulu.

Ninyi mmesahau miezi kadhaa iliyopita mlikuwa mkimkuza Jafo na kusema ndo waziri smart? Si mlianza na hivyo hivyo kwa kusema Nape Nnauye ndo Mtu mwenye akili?mkaja mkasema Makamba January kwa Vijembe vyake ni mtu smart? Wapo wapi sasa?

JAFO ENDELEA NA UYAFANYAYO MPAKA WAPINZANI WAPATE AKILI WASIMAME WENYEWE NA KUACHA KUTEGEMEA WATU WA CCM WAWASAIDIE.
 
Utendaji mbaya wa Rais kwenye kuheshimu demokrasia, uhuru na haki za watu unaeleweka ndani ya nchi yetu na nje ya Taifa letu. Kila mmoja anajua kuwa Rais wetu anapendelea na angefurahi kama tungekuwa na mfumo wa kidikteta.

Jafo ana nafasi yake kama binadamu. Nafasi ya kuamua - aendane na katiba afukuzwe au uungane na ushetani ili kupata faida ya tumbo ya leo na kuishi katika ufukara wa hekima, utu, utashi na ubinadamu, milele.

Mimi nimewahi kufuatwa na viongozi wa CCM na serikali, kundi la watu 9, wakinishawishi nijiunge na CCM, na kuwa nikifanya hivyo nitapewa nafasi ya kugombea au kuteuliwa. Ningekuwa ni mtu ninayefurahia faraja ya tumbo ya leo. Sahizi ningekuwa nao. Lakini nilikataa na wala sitarajii tumbo langu liuamlie mwili wangu wote. Nataka kichwa changu kilicho juu kuliko viungo vyote, na dhamira yangu inayoongozwa na Roho wa Mungu, viuongoze mwili wote. Jafo anashindwa nini?
Wewe labda haupo kwenye uongozi /mfumo lakini Jafo yumo.

Akisema anatoa uamuzi wowote kinyume na jiwe hiyo integrity ataisikia tu redioni... Atachafuliwa kila kiungo,
Atakuwa sio raia,
Atakuwa muhujumu uchumi,
Atakuwa mtakatisha fedha,
Atakuwa ametumia vibaya madaraka
Atakuwa fisadi
Muhurumieni tu ana wake na watoto kijiji kizima 😂 😂
 
Waziri wa Tamisemi ni JPM sio Jaffo,

Jaffo ni waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi

Namhurumia Jaffo maana Jiwe anamharibia
 
Watanzania wengi wajinga wanamsukumia zigo Kijana wa watu na kumuacha mhusika
 
Natanguliza kwanza kuweka msimamo, mimi ni kada wa CCM.

Hali ya mkanganyiko usio na tija katika maandalizi na utekelezaji wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa umetia aibu.

Utafikiri maandalizi yake yamefanywa na watu wasio Watanzania tunaojijua tulikotoka.

Kukata majina ya wagombeaji wa vyama vya upinzani haituongezei umaarufu wowote wana CCM. Mbaya zaidi hata mwana CCM anayependwa ataonekana kabebwa na Jaffo.

Jaffo akiwa Waziri kijana mdogo kwenye siasa usikubali kubeba nuksi ya upendeleo wa wazi unaoweza kuleta machafuko na maafa makubwa.

Waliotumwa kukata majina ya wagombea sasa wao mazao yao yanafyekwa.

Hayo ndiyo matayarisho ya mauaji ya kimbari. Huu umchezo wa kuchezea demokrasia tusiuruhusu.

Nachelea kufikiria ati mtu anaambiwa kata jina la mshindani wa upinzani, mtu anakata. Akiambiwa kuua je?
Si ndiyo mwanzo wa kimbari?

Ni aibu. Hasa kwa vijana wadogo kama Jaffo ambao tulitegemea kulinda mshikamano wa nchi.
Nilisikia akisema majina ya waliopitishwa wa upinzani na waliokata rufaa hayatafutwa kwenye ballot papers!
Ina maana ballot papers zilishachapishwa na hayo majina kabla ya mchujo wa fomu za wagombea?
 
Baada ya kuwaengua sasa mnakuja na porojo zisizokwisha.

Baada ya Upinzani kususia ,eti Jaffo anatangaza kuwarudisha wale walioenguliwa.
Hivi mnategemea kweli CCM,chini ya Waziri Jaffo wasimamie uchaguzi huru na haki.

Tunahitaji Katiba mpya ambayo itaondoa ukiritimba huu wa CCM.
 
Jidu hauko serious ndg yangu,!
Unaweza kukataa maagizo ya Mkuu mwenye level ya jiwe hapa Africa?
Sawa mada yako nzuri ila unajifurauisha
Hawawzi kupinga Ma CDF,IGP,DGTISS,PM sembuse ki Jafo?
Acha masihala bana,Namba 1 Tanzania ana nguvu kuliko,leo Kijafo kikatae kutekeleza matakwa yake,!kwani chenyewe hakipendi kupumua au watoto wake waende chooni?
Yatumie madaraja vibaya na utaona matokeo yake.
Rais wa Sudan aligundua hilo, mambo yalipobadilika wale waliotakiwa kumlinda ndio wakamsweka selo hadi leo.
 
Natanguliza kwanza kuweka msimamo, mimi ni kada wa CCM.

Hali ya mkanganyiko usio na tija katika maandalizi na utekelezaji wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa umetia aibu.

Utafikiri maandalizi yake yamefanywa na watu wasio Watanzania tunaojijua tulikotoka.

Kukata majina ya wagombeaji wa vyama vya upinzani haituongezei umaarufu wowote wana CCM. Mbaya zaidi hata mwana CCM anayependwa ataonekana kabebwa na Jaffo.

Jaffo akiwa Waziri kijana mdogo kwenye siasa usikubali kubeba nuksi ya upendeleo wa wazi unaoweza kuleta machafuko na maafa makubwa.

Waliotumwa kukata majina ya wagombea sasa wao mazao yao yanafyekwa.

Hayo ndiyo matayarisho ya mauaji ya kimbari. Huu umchezo wa kuchezea demokrasia tusiuruhusu.

Nachelea kufikiria ati mtu anaambiwa kata jina la mshindani wa upinzani, mtu anakata. Akiambiwa kuua je?
Si ndiyo mwanzo wa kimbari?

Ni aibu. Hasa kwa vijana wadogo kama Jaffo ambao tulitegemea kulinda mshikamano wa nchi.
Kwahiyo mkuu wewe unaamini Jafo kashindwa kisimamia uchaguzi wa serikali za mitaa?
 
Wewe labda haupo kwenye uongozi /mfumo lakini Jafo yumo.

Akisema anatoa uamuzi wowote kinyume na jiwe hiyo integrity ataisikia tu redioni... Atachafuliwa kila kiungo,
Atakuwa sio raia,
Atakuwa muhujumu uchumi,
Atakuwa mtakatisha fedha,
Atakuwa ametumia vibaya madaraka
Atakuwa fisadi
Muhurumieni tu ana wake na watoto kijiji kizima 😂 😂
Blackmail!
 
Kwahiyo mkuu wewe unaamini Jafo kashindwa kisimamia uchaguzi wa serikali za mitaa?
Mkuu mwenye macho haambiwi tazama.
Watu wameanza kufyekeana mazao vijijini, hivi tusubiri watu waanze kuchomeana nyumba na kuchinjana ndio tuelewe kuwa hali si shwari?
 
Back
Top Bottom