Pamoja na udhaifu wake wote ilionao, ni kwanini CCM inaamini itatawala Tanzania milele?

Pamoja na udhaifu wake wote ilionao, ni kwanini CCM inaamini itatawala Tanzania milele?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Hicho chama kinahusika kwenye kila madudu yanayotokea kwenye nchi yetu. Hakuna jambo baya kwa Watanzania ambalo halijatokana na CCM kuwa madarakani. Lakini CCM wenyewe kwa kujiamini kabisa wanasema kwamba watatawala Tanzania milele?

Haya ni maneno yanayoonesha CCM ina kiburi cha uzima kiasi kwamba inaamini mpaka kyama yenyewe itakuwa inaitawala Tanzania.

Au CCM inawaona watanzania ni mazezeta wasioweza kuwatoa madarakani?
 
Hakuna wapinzani. Watakapotokea CCM watabadilisha msimamo wao.

Upinzani utakaotokana na Watanzania, sio kikundi fulani cha watu wachache, Wenye interest zao na kulazimisha Agenda zao ndio ziwe Agenda za Watanzania.

Siku Watanzania watakapoungana kutetea maslahi yao ndio utakuwa Mwisho wa CCM. Kwa sasa No, waliopo Nje ni wabaya kuliko waliopo ndani.
 
Hakuna wapinzani......
Watakapotokea CCM watabadilisha msimamo wao.
Ili wawe wapinzani wanatakiwa wawe na sifa zipi. Maana ni ajabu kama wanaosema hakuna wapinzani ni CCM wenyewe. Jee CCM kwa muktadha huu wanayo sifa ya kusema kuwa hakuna wapinzani dhidi ya CCM?
 
Kwa sasa ccm sio chama ila ni kikundi fulani cha watafuna nchi wakiwa na marafiki zao, familia zao na watu wanaoamua kuunga nao.

Hiki kikundi kimeamua kushika mamlaka zote nyeti za nchi kwa kuwapa asali na kuwakikisha maisha mazuri wao na familia zao.

Kwa sasa wamefanikiwa kuwashika vyama vya upinzani hususani vinavyoonekana tishio kwenye maslahi yao na kuamua kugawana nao sehemu ya utamu ili kuwafunga mdomo.

Hawa hawataki na hawapendi kusikia yeyote mwenye mawazo mema kuhusu nchi au mawazo tofauti na yao.

Mzizi wa hii kikundi unamwagiliwa kutoka Msoga.
 
Milele maana yake unaielewa. Yaani hata kama dunia itadumu kwa miaka 2000 ijayo, CCM itakuwa madarakani??
Sijui kwa miaka 2000 ijayo. Lakini mimi na wewe tutakufa tutaiacha CCM madarakani, isipokuwa hivyo niite mbwa. Tunza hii comment siku upinzani wakishinda nikumbushe
 
Kwasababu mentality ya watu hata ya kwako ni Kutawaliwa na sio kutumikiwa au kufanyiwa kile mnachotaka...

Hence hakuna mabadiliko hata akija mtawala mwingine ni yaleyale..., So long as kilichopo kwenye Menu ni Kutawaliwa huku chini nothing will change, bali ni watu kubadilishana zamu ya kunyonya jasho la majority...

Thus I have decided since way back kuacha kutumika kama ngazi ya wengine kupanda.... (at-least not voluntarily)
 
Sijui kwa miaka 2000 ijayo. Lakini mimi na wewe tutakufa tutaiacha CCM madarakani, isipokuwa hivyo niite mbwa. Tunza hii comment siku upinzani wakishinda nikumbushe
Umekata tamaa ama wewe ndiye unayekatisha wengine tamaa? Yaani ni kama unasema ni sawa tu nchi kuendeshwa hivi inavyoendeshwa kwa kuwa hakuna mawazo mbadala.
 
Umekata tamaa ama wewe ndiye unayekatisha wengine tamaa? Yaani ni kama unasema ni sawa tu nchi kuendeshwa hivi inavyoendeshwa kwa kuwa hakuna mawazo mbadala.
Sikatishi mtu tamaa, wanaoweza kupambana kuitoa ccm madarakani wafanye hivyo.
Mimi siamini kama wapinzani watakuwa na jipya, siasa hizi kila mtu anaangalia tumbo lake hakutakuwa na jipya lolote. Sichukulii siasa seriously kivile maana nitaishia kuvunjika moyo.
 
sheiza basi kianzishwe chama kingine cha siasa mtakachokiamini kama hivi vilivyopo hamviamini!!
 
Sikatishi mtu tamaa, wanaoweza kupambana kuitoa ccm madarakani wafanye hivyo.
Mimi siamini kama wapinzani watakuwa na jipya, siasa hizi kila mtu anaangalia tumbo lake hakutakuwa na jipya lolote. Sichukulii siasa seriously kivile maana nitaishia kuvunjika moyo.
Wapinzani wanakatisha tamaa, CCM jee haikatishi tamaa!!??
 
Wapinzani wanakatisha tamaa, CCM jee haikatishi tamaa!!??
Kama ina katisha tamaa na hakuna wa kumpindua tufanyeje sasa?
Mfano hai ni hizi siasa zinazoendelea sasa hivi unadhani upinzani watashinda 2025. Mama ameshakubalika anafanya maajabu tunampinga ili iweje? Apewe miaka 10 zaidi
 
CCM ina kiburi ,ila chanzo kinatokana na systems zilizopo as of now, utakuta generals wengi kwa Jeshi ni wanachama CCM , wakuu wengi polisi , wakubwa wa idara nyingi hata za uchumi,sheria na siasa ni wana CCM.
inshort system iliyopo CCM ndiyo nchi na nchi ni CCM ,nje ya hapo options ni chache mno.
kunahitajika dispension ya kuitoa chama , a separation of the state and party.
Unaingiaje kura ambayo election commisioner ni mwana CCM na utarajie fairness.
Food for thought
 
Kwasababu mentality ya watu hata ya kwako ni Kutawaliwa na sio kutumikiwa au kufanyiwa kile mnachotaka...

Hence hakuna mabadiliko hata akija mtawala mwingine ni yaleyale..., So long as kilichopo kwenye Menu ni Kutawaliwa huku chini nothing will change, bali ni watu kubadilishana zamu ya kunyonya jasho la majority...

Thus I have decided since way back kuacha kutumika kama ngazi ya wengine kupanda.... (at-least not voluntarily)
Umefanya jambo la maana kuwa mshabiki wa chama ni kupoteza muda wako
 
Back
Top Bottom